Kwanini Madikteta hupenda sana kusifiwa?

unprejudiced

JF-Expert Member
Jan 27, 2017
2,359
2,000
Katika nchi nyingi za kiafrika ambazo watu wanauawa hovyo, kutekwa, majanga kama mafuriko, wakulima hawana masoko wafanyakazi mishahara duni biashara kudorola halafu unakuta Television ya taifa hilo kila uchao linapiga nyimbo za kumsifia rais.

Nchi hizi hutegemea fedha za Mabeberu ktk kukopa na wananchi ndio wanalipa madeni hayo yenye riba kubwa. Lakini wakipata pesa kutoka kwa Mabeberu utasikia eti Rais katoa pesa kujenga barabara. Pesa wametoa Mabeberu kwa mkopo halafu yana jitukuza eti ni Rais katoa wakati yeye mwenyewe analipwa mshara na malupulupu na wananchi wanyonge wa nchi hizo. Kwa nini madikteta hupenda sana kusifiwa?

Madikteta hupenda kujionesha yako jirani na watu na yanapendwa. Utayaona yanaigiza kula chakula au kunywa chai wakiwa na watu na wakiwa wanakula lazima tukio hilo litangazwe ili watu waone kuwa Dikteta amekula na watu au amekunywa chai na watu.

Kule Kenya nakumbuka Rais Moi vyombo vya habari vilikuwa vikimuita Mtukufu Rais Daniel Araph Moi. Nyimbo katika radio zilikuwa zinamsifia yeye na KANU tu. Kumbe watu huku wakimuimbia nyimbo za sifa Moyoni wanamng'ong'a hiloo linapenda sifa.

Leo KANU ya Moi iliyokuwa ikisifiwa na kutukuzwa tunajua ilipo.

Maendeleo hayana vyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida ni kujua kama unachowazA Wewe ndo wanavyowaza hao unaowaita madikteta. Kuhusu kusifiwa hata wewe unasubiria kusifiwa kwa pumba ulizoandika hapa. Dunia nzima unazungumzia Corona, wewe unakuja na mada ya kijinga ambayo haina impact yoyote kwa jamii na Shida zake. Wewe Itakusaidia nini kujua Mbowe amekuwa mwenyekiti wa kudumu. Au kuhusu ruzuku ya chama. Itakusaidia nini kujua JPM Yuko likizo ya Pasaka home. So tell us more about how a simple Tanzanian can be responsible in protecting not only him or herself against COVID-19 but more so people around him or her ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,057

Kwahiyo wewe ndo una akili sana kuliko Jiwe aliye kwambia Msitishane huko Lumumba kwaajili ya Corona?. Hebu ficha ujinga wako jibu swali kwa nini Madikteta hupenda sana kusifiwa? Halafu mbona umepanik wewe? Kwani kuna jina la dikteta limetajwa hapo unaye mfaham umeina sifa hizo zinaringa na sifa za dikteta unalo lifahamu? Au wew ndio kibaraka wa hilo dikteta unalipigania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,333
2,000
Mi namkumbuka mwenyekiti wa chama fulani hapa nchini. Yeye hakuna kitu anachukia kama mwanachama mwenzake anajitokeza kugombea nae nafasi ya mwenyekiti. Kugombea nae inamaanisha hakubaliki. Hivi juzi alimtisha Mgombea mmoja kuwa "sumu haionjwi kwa kuilamba"!
 
Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
2,871
2,000
Kweli kabisa imefikia mpaka aliyetaka kuchukua fomu ili apambane nae kuvuliwa uanachama na kusema kosa la kimaadili
Mi namkumbuka mwenyekiti wa chama fulani hapa nchini. Yeye hakuna kitu anachukia kama mwanachama mwenzake anajitokeza kugombea nae nafasi ya mwenyekiti. Kugombea nae inamaanisha hakubaliki. Hivi juzi alimtisha Mgombea mmoja kuwa "sumu haionjwi kwa kuilamba"!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom