Ninafanana tabia na Rais Magufuli, naelewa sana anaposema anapenda kusifiwa

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
Watu wengi wamekuwa wakishangaa kauli za Rais wetu.
nyingi ni za kawaida sana kwa aina ya kundi ambalo Rais yupo. hawa watu wanahitaji akili nyingi sana kuwaelewa
Mimi nimeona kwenye mambo mengi nashabihiana naye sana tabia kwa hiyo namuelewa sana na ningependa kuwapa ujuzi wa kumuelewa Rais ili tumfanye afanye zaidi na nchi yetu isogee

Mungu hakuumba bnadamu wa aina moja dunia nzima. Tuko sawa kwa maana ya kushi na kufa lakini kitabia tunatofautiana sana. Rais Magufuri yuko kwenye kundi la watu wambao ni wachache na ni wagumu sana kuwaelewa. Mara nyingi unaweza kuishia kumchukia na kufikiri ni mkatiri sana. lakini watu hawa huwa ni wapole sana tena wana huruma nyingi
Udhaifu mkubwa wa watu wa namna yetu ni mmoja, kutokana na kupingwa sana sababu ya kutoeleweka vizuri huwa wanakata tamaa. Lakini huwa nasema ni aina ya watu ambao ukiwapa kazi itakwenda ingawa wanaweza kuathiriwa na kukatishwa tamaa.

dawa kubwa ni kuwatia moyo kwa kuona juhudi zao
mfano yapo mambo ambayo Rais bila hiana anastahili kusifiwa
1. umeme, siku hizi mgao haupo tena, ebu jiulize mgao wa zamani uklikuwa unatoka wapi, twende REA nyumba nyingi sana zimeunganishwa tena kwa gharama ndogo. service charge hazipo tena lakini umeme unaendelea vizuri
2. maji. dar karibu yote inaunganishwa sasa kwa nini asisifiwe kwa kazi nzuri
3. mabarabara kila mahali hadi njia kumi na mbili mbezi to kibaha. kwa nini wengine hawakufanya na huyu kafanikiwa.
4. elimu bure sijaona ikitetereka. mimi nimesoma shule zote za kayumba. naelewa umuhimu wa elimu bure. wengi wamesoma shule nzuri lakini kama sio shule za serikali labda ningekuwa mchoma mkaaa
5.ndege mpya, wapo watu wanasema hakukuwa na uharaka wa kununua cash. mimi nasema Rais kafanya uamuzi mzuri sana maana kununu kwa mkopo unaongeza riba sasa nani anataka kulipa zaidi.
7. umangimeza siku hizi umeisha. ni rahisi sana kumwona mkuu wa mkoa, katibu , mkuu au mku wa wialaya. zamani hawa walikuwa kuwaona ni shidaa.
8 utulivu wa kijamii kwa maana ya usalama. yapo matukio ya siyofurahisha lakini kwa ujumla usalama ni mkubwa sana. jamii yetu inaweza kustawi panapokuwa na utulifu haswaa wa kijamii. kwa hili naona hatuna shida kabisa
9. upande wa afya kila wilaya imepewa pesa za kujenga kituo cha huduma ya afya. hivi tunataka maendelea kwenye vitu vipi haswaa. maendeleo ni ustawi wa jamii na sio watu kuwa na pesa.

nasema ukweli sikumpa kura mheshimiwa ila kwa utendaji wake ananishawishi na ninaimani kama atatatua changamoto mbili kwangu nitampigia hata kampeni
changamoto ambazo rais ninejiona kwake kitabia angezitatua ni swala la watumishi na wastaafu na kukaa meza moja na wapinzani ili taifa liwe moja. pamoja na kutuwekea katiba nzuri ili mambo mema anayofanya yawe milele

nampongeza Rais wetu, anastahili pongezi kwa kazi nzuri tena sana na mweye macho na akili anaona.
nina imani tukimuunga mkono na kuendelea kummwagia pongezi nyingi kwa mema anayofanya tutamfanya atufikishe mbali

Tusisubiri afe ndio tuone wema weka. pia tusiwe miongoni mwa wale ambao historia itawahukumu kwa kupinga mambo mema yanayoletwa na mtu aliyejitolea. tusikatishe uzuri na utendaji wake kwa kushindwa kumpa haki yake nayo ni ndogo tu kumpa pongezi na sifa tele kwa kazi nzuri

viva magufuri viva presizaa na tunaomba pia uangalie watumishi na kuwaleta ndugu zetu wapinzani mezani mnywe chai.
tunaielewa sana kazi yako
 
Bandiko nzuri mkuu ila nadhani issue ya katiba raisi amedhatolea ufafanuzi mara kadhaa kwamba hicho sio kipaumbele chake, kwa hili hata mimi huwa namuunga mkono sababu kana katiba hii hii ambaye wengine walishindwa kudhibiti wizi serikalini na kwenye madini raisi Magufuli kaweza sasa hapo shida ni katiba au shida ni aina ya viongozi tunaowapa dhamana.

Swala la wapinzani sidhani kama raisi anaugomvi na na upinzani, nadhani wanapopishana ni aina ya democracia upinzani wanayoitaka, democracia yakufanya mikutano nchi nzima wakati sio kipindi cha kampeni. Embu fikiria kwa aina ya upinzani tulionao wanaopenda kuzusha mambo ukawaruhusu wazunguke chi nzima kufanya mikutano si wataanza kupinga ununuzi wa ndege, ujenzi stiggler's george na SGR kwakuwaamisha wananchi kwamba hivyi sio vipaumbele vyetu. Ikiwa waliweza kuzusha kwamba kuna upotevu wa
1.5trl unadhani watashindwa kuzusha mambo mengine?

Swala la watumishi wa uma na wastaafu hilo nakuunga mkono japo nakumbuka Maymosi iloyopita raisi alisema kwa sasa nchi inatekeleza miradi mikubwa kwa hyo ni vema ikamalizika kwanza then mishshara ikipanda itapanda kwa kiasi cha kuridhisha.
 
Ni kweli magufuli asifike kabisakwanza niongezee kafanikiwa kuleta WASIOJULIKANA Woote waliopita awamu nne pamoja na kukatishwa tamaa ila walivumilia na kukubali yote pili!!!Nampa hongera mahakamani wanasiasa wameongezeka
 
Huwa sipendi kutoa kutoa sifa kwa binadamu wanapotekeleza wajibu wao lakini kwa utendaji wake mheshimiwa rais anasthili kila aina ya sifa kwa haya anayoyasimamia na kuyatekeleza mwenyezi mungu amlinde sana saana yani.
 
Bandiko nzuri mkuu ila nadhani issue ya katiba raisi amedhatolea ufafanuzi mara kadhaa kwamba hicho sio kipaumbele chake, kwa hili hata mimi huwa namuunga mkono sababu kana katiba hii hii ambaye wengine walishindwa kudhibiti wizi serikalini na kwenye madini raisi Magufuli kaweza sasa hapo shida ni katiba au shida ni aina ya viongozi tunaowapa dhamana.

Swala la wapinzani sidhani kama raisi anaugomvi na na upinzani, nadhani wanapopishana ni aina ya democracia upinzani wanayoitaka, democracia yakufanya mikutano nchi nzima wakati sio kipindi cha kampeni. Embu fikiria kwa aina ya upinzani tulionao wanaopenda kuzusha mambo ukawaruhusu wazunguke chi nzima kufanya mikutano si wataanza kupinga ununuzi wa ndege, ujenzi stiggler's george na SGR kwakuwaamisha wananchi kwamba hivyi sio vipaumbele vyetu. Ikiwa waliweza kuzusha kwamba kuna upotevu wa
1.5trl unadhani watashindwa kuzusha mambo mengine?

Swala la watumishi wa uma na wastaafu hilo nakuunga mkono japo nakumbuka Maymosi iloyopita raisi alisema kwa sasa nchi inatekeleza miradi mikubwa kwa hyo ni vema ikamalizika kwanza then mishshara ikipanda itapanda kwa kiasi cha kuridhisha.
Zero brain at fully
 
Mkuu ingebadilishwa katiba ili kuondoa uhuru wa kukusanyika kwa maana ya mikutano ya hadhara,maana ni takwa la kikatiba!
Pia unapotoka sana unaposema wapinzani watazunguka nchi nzima kuwaaminisha ununuzi wa ndege sio kipaumbele cha taifa,hiyo ndiyo kazi haswa ya siasa!Kila mtu anakuwa na maoni yake,kama anaamini sio kipaumbele kwanini asiwaambie wananchi hoja hiyo ili kuwashawishi kujiunga na chama chake?
Hatari ipo kama siku kila Rais ataamua kuwa na vipaumbele vyake halafu akazuia wananchi kukusanyika kujadili kwakuwa wanaweza kupingana naye!
Yaani imefikia mahali mawazo ya mtu mmoja ndio sahihi kuliko ya watanzania wote!
Jielimishe kwanza juu ya masuala ya kisiasa!
Mfano,kama isingekuwa awamu ya nne kutoa uhuru wa mikutano ya hadhara,wananchi wasingehamasika kuona ufisadi unalitafuna sana taifa hivyo kuilazimu ccm kujipanga kudeal na ufisadi japo mafanikio yake bado si sana!
Awamu hii inaficha mapungufu yake ili ionekane safi na kwa hilo wanafanikiwa kuwahadaa wananchi kuwa ufisadi umekwisha!
 
Acha maneno mengi sema tu tuna Rais mwenye tabia za kibinafsi, muoga na Mkatili

Vile alishaapa tutalimia meno tunasubiri wakati ufike.
 
Mkuu ingebadilishwa katiba ili kuondoa uhuru wa kukusanyika kwa maana ya mikutano ya hadhara,maana ni takwa la kikatiba!
Pia unapotoka sana unaposema wapinzani watazunguka nchi nzima kuwaaminisha ununuzi wa ndege sio kipaumbele cha taifa,hiyo ndiyo kazi haswa ya siasa!Kila mtu anakuwa na maoni yake,kama anaamini sio kipaumbele kwanini asiwaambie wananchi hoja hiyo ili kuwashawishi kujiunga na chama chake?
Hatari ipo kama siku kila Rais ataamua kuwa na vipaumbele vyake halafu akazuia wananchi kukusanyika kujadili kwakuwa wanaweza kupingana naye!
Yaani imefikia mahali mawazo ya mtu mmoja ndio sahihi kuliko ya watanzania wote!
Jielimishe kwanza juu ya masuala ya kisiasa!
Mfano,kama isingekuwa awamu ya nne kutoa uhuru wa mikutano ya hadhara,wananchi wasingehamasika kuona ufisadi unalitafuna sana taifa hivyo kuilazimu ccm kujipanga kudeal na ufisadi japo mafanikio yake bado si sana!
Awamu hii inaficha mapungufu yake ili ionekane safi na kwa hilo wanafanikiwa kuwahadaa wananchi kuwa ufisadi umekwisha!

Hii ndiyo akili kubwa, ccm hawaweza kuliona hili, mtu ambaye anaamini jiwe yuko sahihi katika maamuzi yake basi mtu huyo ni mzigo hata kwa familia yake
 
s
Haiwezekani ukawa kaskazini wewe,hata kuandika hujui.
sawa sijui lakini nina imani wazo langu umelipata. lakini pia ukaskazini hauji sababu ya kujua kuandika unakuja sababu ya kuishi na kuwa na damu ya huko. labda utoe damu yangu unipe nyingine mkuu
 
Back
Top Bottom