Kwanini Madikteta hupenda sana kusifiwa?

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,137
2,000
Katika nchi nyingi za kiafrika ambazo watu wanauawa hovyo, kutekwa, majanga kama mafuriko, wakulima hawana masoko wafanyakazi mishahara duni biashara kudorola halafu unakuta Television ya taifa hilo kila uchao linapiga nyimbo za kumsifia rais.

Nchi hizi hutegemea fedha za Mabeberu ktk kukopa na wananchi ndio wanalipa madeni hayo yenye riba kubwa. Lakini wakipata pesa kutoka kwa Mabeberu utasikia eti Rais katoa pesa kujenga barabara. Pesa wametoa Mabeberu kwa mkopo halafu yana jitukuza eti ni Rais katoa wakati yeye mwenyewe analipwa mshara na malupulupu na wananchi wanyonge wa nchi hizo. Kwa nini madikteta hupenda sana kusifiwa?

Madikteta hupenda kujionesha yako jirani na watu na yanapendwa. Utayaona yanaigiza kula chakula au kunywa chai wakiwa na watu na wakiwa wanakula lazima tukio hilo litangazwe ili watu waone kuwa Dikteta amekula na watu au amekunywa chai na watu.

Kule Kenya nakumbuka Rais Moi vyombo vya habari vilikuwa vikimuita Mtukufu Rais Daniel Araph Moi. Nyimbo katika radio zilikuwa zinamsifia yeye na KANU tu. Kumbe watu huku wakimuimbia nyimbo za sifa Moyoni wanamng'ong'a hiloo linapenda sifa.

Leo KANU ya Moi iliyokuwa ikisifiwa na kutukuzwa tunajua ilipo.

Maendeleo hayana vyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta kitabu kinaitwa dictator's mind kimeelezea yote,kuhusu chanzo cha udikteta, tabia zao,hulka zao,nk.
Kiufupi chanzo cha udikteta unaanzia kwenye malezi mabovu muhusika aliyopata au masaibu yoyote aliyopata dikteta utotoni yakaathiri brain yake wengine walishuhudia wazazi wao wakiuliwa kikatili mbele yao,wengine wazazi waliachana utotoni,wengine walitelekezwa utoto,ni jumuisho la matendo yote ya ukatili waliyopitia utotoni mfano shida,umasikini, dhiki,vikapelekea brain kujaa sumu.

Nini tiba yake ni hadi muhusika apate uponyaji wa ndani utakapelekea kuachilia kusamehe yote aliyopitia ili aanze upya.Asipopata uponyaji wa ndani ugeuka kuwa mnyama katili,mlipa kisasi hapa Mara nyingi wanaolipwa visasi au fanyiwa ukatili huwa sio wahusika yaani wengine ndio wanathirika na sio wasababishi wa kumuumiza dikteta utotoni. Kwann wanapenda kusifiwa na kuabudiwa jibu ni walikosa upendo utotoni yaani wariruka stage za ukuaji awakupata upendo utotoni hivo ikawapelekea usugu.

Thus tunashauriwa watoto wadogo tuwe na tabia za kuwabeba na kuwakumbatia vifuani hii ni tiba tosha inawafanya wajihisi salama kwa ajili ya kukuza brain zao na kuleta mizania ya balance.Usimtese mtoto,usimbeze mtoto,usimpuuze mtoto akiwa analia inatakiwa umbembeleze usipofanya hivo unamjengea usugu na hali ya ukosefu wa utu akiwa mkubwa kama akikosa muongozo sahihi mfano dini na elimu chance ya kuwa dikteta ni kubwa.

Wenzetu wamefanikiwa kupata viongozi bora sababu wanafatilia historia ya utoto wa MTU,thus wao wanasonga tu awafail wanapata viongozi bora tofauti na Africa. Pia Africa mifumo yetu ya kimalezi imejengwa kwenye mifumo dume
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,137
2,000
Wanapenda sana kujionyesha wapo karibu na wananchi hasa maskini..
Wengine wanapenda kufanya vitu vya ajabu ajabu mfano kulala kwenye mawe kaa kenge.
Inaitwa smoke camouflage yaani kujifanya uko pamoja na jamii ili udrawa attention ya kuteka akili zao kisiasa
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,137
2,000
Wanaweza kuwa watu wazuri na ni mfano wa mungu, maana mungu nae anapenda kusifiwa na mapambio kila siku.
Mfano wa Mungu utenda ya Kimungu ya kumpendeza Mungu.Je Mungu anapenda kuuwa watu,kuletea umasikini watu, kutesa watu,kufunga watu?
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,137
2,000
Dikteta ninaemfahamu vizuri ni Nduli Iddi Amini tu. Nae sikumbuki kama kuna mtu aliwahi kumsifia kwa matendo mazuri, ila utemi wake ulikomeshwa na Watanzania. Hao wengine mfano wa huyo uliemtaja unaweza kuwaita madikteta uchwara, kwa kuwa hawajafikia kile kiwango cha utemi, uonevu na ubabe kama cha Nduli Idd Amini. Na uzuri wa hawa madicketa uchwara huwa kuna mambo mazuri wanayafanya na yanaonekana yanapelekea kupata misifa
Dikteta is a dictator, kuna cold blood dikteta na pure blood dikteta. Zipo factor za kupima huyu ni dictator au sie vinatazamwa mfano

Idadi ya watu uliouwa,kiwango cha ubinafsi ulichonacho,Mali ulizojilimbikizia,matumizi mabaya ya madaraka, maamuzi uyafanyayo,nk.Udikteta na umasikini ni pacha madikteta wote upendelea maendeleo ya vitu kuliko watu.
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
8,492
2,000
Pengine wewe ni mdogo . Lakini tuliokuepo kipindi cha Idi Amin Dada ni kiongozi aliyependa kusifiwa sana. Chochote alichofanya isipokuwa kwenda chooni ilikuwa ni habari .

Kinachowaponza na dictator karibu wote. Ni ile kujiona wao ni wazalendo kuliko wengine.

Odhis *
Na kulazimisha ionekane wanajua kila kitu kuliko yeyote
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,137
2,000
Lituye
Acha tu wajitukuze maisha ni mafupi. Madikteta wote wana life style inayofanana, hizo principle zinasomwa kama wewe ulivyosoma taaluma yako darasani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes pia 80% ya madikteta wote duniani ni wakristo. Wote ufanana tabia,wezi,waongo,wabinafsi,visasi,chuki,makatili,washirikina,wazinzi,wafujaji,wajuaji lkn ni empty kichwani,wapenda sifa,wapenda propaganda ofisi zao ziko kwenye macamera dikteta yuko radhi kumdhalilisha MTU mbele ya camera ili apate sifa.
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,137
2,000
Wewe haupendi kusifiwa?
Kusifiwa ni utoto sifa za kike.MTU matured na civilized na anaejiamini akamilishwi kwa kusifiwa au kuabudiwa.Ujikamilisha mwenyewe bila msaada toka nje ya utashi wake wa ndani isipokuwa kwa uncivilized na unmatured
 
GEMBESON

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
581
1,000
Dikteta is a dictator, kuna cold blood dikteta na pure blood dikteta. Zipo factor za kupima huyu ni dictator au sie vinatazamwa mfano
Idadi ya watu uliouwa,kiwango cha ubinafsi ulichonacho,Mali ulizojilimbikizia,matumizi mabaya ya madaraka, maamuzi uyafanyayo,nk.Udikteta na umasikini ni pacha madikteta wote upendelea maendeleo ya vitu kuliko watu.
Kuna ka ukweli kiasi. Pia Madikteta huwa hawako tayari kutoka madarakani kirahisi labda hadi wapinduliwe. Huwa wanafanya shughuli zao nyingi kwa kutumia mashushushu. Pia wanatumia nguvu kubwa ya jeshi kufanya chochote wakitakacho.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
3,549
2,000
Kuna watu kama kambona waliwahi kumshutumu Nyerere kwa udikteta, lakini hajawahi kutokea rais mwenye outstanding character na ushawishi kama mwalimu, maana yake ni kwamba kwa asili yetu, namna tunavyoendesha mambo, IQ za watu wetu, fikra na mitazamo yetu kiujumla yanaakisi namna viongozi wetu wanavyo behave na kuonekana na watu wengine kama madikteta
 
Sang'udi

JF-Expert Member
May 16, 2016
2,399
2,000
Kusifiwa ni utoto sifa za kike.MTU matured na civilized na anaejiamini akamilishwi kwa kusifiwa au kuabudiwa.Ujikamilisha mwenyewe bila msaada toka nje ya utashi wake wa ndani isipokuwa kwa uncivilized na unmatured
Too irrelevant explanations... Jibu swali.
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
2,429
2,000
Katika nchi nyingi za kiafrika ambazo watu wanauawa hovyo, kutekwa, majanga kama mafuriko, wakulima hawana masoko wafanyakazi mishahara duni biashara kudorola halafu unakuta Television ya taifa hilo kila uchao linapiga nyimbo za kumsifia rais.

Nchi hizi hutegemea fedha za Mabeberu ktk kukopa na wananchi ndio wanalipa madeni hayo yenye riba kubwa. Lakini wakipata pesa kutoka kwa Mabeberu utasikia eti Rais katoa pesa kujenga barabara. Pesa wametoa Mabeberu kwa mkopo halafu yana jitukuza eti ni Rais katoa wakati yeye mwenyewe analipwa mshara na malupulupu na wananchi wanyonge wa nchi hizo. Kwa nini madikteta hupenda sana kusifiwa?

Madikteta hupenda kujionesha yako jirani na watu na yanapendwa. Utayaona yanaigiza kula chakula au kunywa chai wakiwa na watu na wakiwa wanakula lazima tukio hilo litangazwe ili watu waone kuwa Dikteta amekula na watu au amekunywa chai na watu.

Kule Kenya nakumbuka Rais Moi vyombo vya habari vilikuwa vikimuita Mtukufu Rais Daniel Araph Moi. Nyimbo katika radio zilikuwa zinamsifia yeye na KANU tu. Kumbe watu huku wakimuimbia nyimbo za sifa Moyoni wanamng'ong'a hiloo linapenda sifa.

Leo KANU ya Moi iliyokuwa ikisifiwa na kutukuzwa tunajua ilipo.

Maendeleo hayana vyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
ahahahhaa jiwe gizani
 
Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,137
2,000
Kuna ka ukweli kiasi. Pia Madikteta huwa hawako tayari kutoka madarakani kirahisi labda hadi wapinduliwe. Huwa wanafanya shughuli zao nyingi kwa kutumia mashushushu. Pia wanatumia nguvu kubwa ya jeshi kufanya chochote wakitakacho.
Dikteta huwa anatolewa kwa kupinduliwa,kuuliwa,kufurushwa ukimbizini haijawahi tokea dikteta kufia madarakani.Kila mwanadamu yyeto ni lzm alipwe uovu wake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom