Kwanini Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA?

RABIN GHYOOT

Member
Sep 17, 2014
10
2
Kuna mtu anaitwa Salum kuna siku hapa alituelimisha juu ya hili. Nimemnukuu (copy n paste) hapo chini:

Uzuri wa Mbowe ndio huo huo ubaya wa Mbowe na uzuri wa Shibuda ndio huo huo ubaya wa Shibuda. Tuliya nitakufafanulia.

Faida ya Mbowe kuwa mwenyekiti wa CHADEMA ni kwamba CHADEMA inakuwa na uhakika wa kuungwa mkono na wachaga, na hichi ni kitu muhimu. Ukweli kwamba mwenye mamlaka ya juu ndani ya CHADEMA, mwenye control ndani ya CHADEMA ni Mbowe umewezesha chama hicho kuungwa mkono na wachaga kwa kiasi kikubwa. Kumbuka chama hiki kimeshawahi kuongozwa na mwenyekiti (Makani) ambaye sio mchaga na katika kipindi hicho kilikuwa hakina strong support ya wachaga.

Wachaga wanaelewa hata ikitokea Rais wa Nchi ni Dr. Slaa na Mwenyekiti wa CHADEMA ni Mbowe, katika mazingira hayo anayetawala Nchi ni Mbowe. Mwenyekiti wa chama chenye wabunge wengi anaweza kusababisha Rais akapigiwa kura ya kutokuwa na imani na yeye, na hivyo akapoteza Urais. Mwenyekiti wa Chama anaweza kuhakikisha awamu ya pili anapitisha jina la mgombea Urais mwingine, na hivyo Rais aliyekuwepo madarakani akaongoza kipindi kimoja. Ukweli huu ndio uliyoifanya CCM ikatae kofia mbili; wakasema mgombea Rais atakayepitishwa na chama lazima pia awe mwenyekiti wa chama.

Faida ya chama cha siasa kuungwa mkono na wachaga sio ya kupuuzwa. Wachaga wanadesturi ya kujitolea kwa hali na mali. Chama kikiungwa mkono na wachaga kina uhakika wa kupigiwa debe kwa sababu ni desturi ya mchaga kutetea chenye faida kwake. Eneo lolote la utawala ambapo mwenye madaraka ni mchaga basi hapo ujuwe CHADEMA wana-uhakika wa kupata msaada kisiri siri. Tembelea mikoani uangalie wafanya biashara wa kichaga wanavyojitolea kusaidia CHADEMA. Huko mikoani Mkuu wa kituo cha polisi akiwa mchaga basi CHADEMA wanauhakika wakupata msaada kisiri siri.

NCCR MAGEUZI miaka ya nyuma ilishawahi kupata hii strong chaga support wakati huo ikiongozwa na Mrema; katika uchaguzi wa mwaka 1995 kilikuwa cha pili.

Hata kama NCCR-MAGEUZI imepata mchaga mwingine (Mbatia) sasa hivi, na TLP inaonekana kuongozwa na mchaga (Mrema) hii haitoshi kufanya wachaga waviunge mkono hivi vyama kwasababu zifuatazo: Kuna kipindi kirefu hawa watu walikuwa hawana jukwaa la kufanya siasa nikimaanisha walikuwa sio wabunge. Ubunge unakupa jukwaa, unachoongea kinapewa uzito. Kuna kipindi kirefu hawa watu walikuwa wanaonekana ‘CCM B’, hata uteuzi wa Mbatia na dada yake ndani ya bunge la katiba na la afrika mashariki uliimarisha imani kwamba Mbatia ni ‘CCM B’ mpaka pale alipowageuka CCM na kuungana na UKAWA. Mrema kwa upande wake kuna swala la afya na kutokuwa ambitious.

Nieleweke vizuri; sisemi kuungwa mkono na wachaga inatosha kufanya chama cha siasa kushinda uchaguzi na kuunda serikali; ninachosema hapa ni vigumu kuwa na chama cha upinzani chenye nguvu Tanzania bara bila ya kuungwa mkono na wachaga.

Ubaya wa Mbowe ni kwamba siku CHADEMA ikipata mwenyekiti ambaye sio mchaga, huu ungwaji mkono wote kutoka kwa wachaga utafifia au utatoweka kabisa. Na mfano mzuri ni kumbuka NCCR-MAGEUZI pale Mrema alipoonekana hana Control ya chama, wachaga waliacha kuunga mkono hicho chama.

Ubaya wa Mbowe ni kwamba huu ungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wachaga umefanya watanzania kutoka kabila zingine kushindwa kutofautisha CHADEMA na uchaga. Imekuwa vigumu kukutana na mchaga ambaye hashabikii CHADEMA. Na hii imefanya watanzania kutoka kabila zingine kujiuliza hivyi mapenzi ya wachaga na CHADEMA yanahusiana na sera (policy) au utambulisho (identity); Kwamba utambulisho wako kama mchaga ni kushabikia CHADEMA. Tabia hii ya wachaga imeibua maswali mengi; Je wachaga ambao vipau mbele vyao ni kuwa matajiri kifedha wanaamini watafaidika nini juu ya uwepo wa Mbowe kama mwenyekiti wa CHADEMA? Haya ni maswali ambayo watanzania kutoka kabila zingine wanajiuliza.

Uzuri wa Shibuda ni kutokuwa na bei, kuwa na ujasiri na uwezo wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana na viongozi wake. Ujasiri huu ndio uliomfanya vyama vya upinzani wampende alipokuwa yuko CCM, kwasababu alikuwa akiwakosoa CCM wenzie.

Kutokuwa na bei ndiko kulikomfanya asielewane na Makamba. Ikumbukwe Makamba alikuwa timu ya pesa (yaani Lowasa na Rostamu). Ujasiri huu ndio ulikuwa unamfanya Shibuda amuunge mkono Spika wa bunge wakati huo mzee wa standard and speed, Samuel Sitta bila ya kujali alikuwa anapambana na nguvu ya pesa (yaani Rostam na Lowasa). Lakini mwisho siku nguvu ya pesa iliweza kushinda kupitia Makamba, kwa kuhakikisha jina la Shibuda halipitishwi na CCM kugombea ubunge. Hii ilimfanya kuhamia CHADEMA.

Chama chochote Shibuda atakachokwenda atakwenda na wasifu au tabia yake ile ile ya kutokuwa na bei, ujasiri na uwezo wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana na viongozi wake.

Ubaya wa Shibuda ni kwamba hawezi kuacha tabia yake kwasababu tu kahamia CHADEMA. Kama alivyokuwa CCM alikuwa na ujasiri wa kuthubutu kutangaza kugombea dhidi ya Mwenyekiti (kikwete) wake ambaye pia ni Rais wa Nchi, kama aliweza kupingana na timu ya pesa (makamba, rostam, lowassa), kama hakuweza kuogopa kuondoka CCM chama tawala chenye fursa zote za kutengeneza pesa, huwezi kutegemea ndani ya CHADEMA atakuwa mtu wa kusema “ndio bwana mkubwa”. Hilo haliwezekani.

Ubaya wa Shibuda ni ameingia CHADEMA akaendeleza wasifu wake ule ule wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana na viongozi wake.

Wakati CHADEMA imekataa matokeo ya Urais na kukataa kumtambua Kikwete kama Rais, yeye Shibuda alikubali matokeo ya Urais na kumtambua Kikwete kama Rais, ingawa CHADEMA baadae walikuja kuchukua msimamo huo huo wa Shibuda na kukubali kumtambua Kikwete kama Rais.

Wakati CHADEMA walipinga kulipwa posho yeye SHIBUDA aliunga mkono ulipwaji wa posho akaita “ujira wa mwiha”. Na mpaka sasa hivi hakuna ushahidi kwamba CHADEMA hawapokei posho. Hivyo inawezekana CHADEMA wamechukua msimamo wa SHIBUDA wa “ujira wa mwiha”.

Wakati kipau mbele cha CHADEMA katika kurekebisha KATIBA ni kupatikana kwa serikali tatu, yeye Shibuda anaona kipau mbele iwe ni kulinda na kuboresha haki za wakulima na wafugaji ndani ya katiba. Inawezekana baadae CHADEMA wakachukua mtazamo/msimamo wa Shibuda kama walivyofanya huko nyuma.

CHADEMA inapomtumia Kasulumbayi na vyombo vya habari ili kupambana na Shibuda ni umakini wa hali ya juu. Tundu Lissu baada ya kumtishia Shibuda kwa kusema atamchukulia hatua kali kwa kuwepo kwenye bunge la katiba, kila akiulizwa swali na waandishi wa habari (waliotumwa na CCM) juu ya Shibuda anasema sitaki kumuongelea huyo mzee. CHADEMA wameona ni vizuri, umakini na sahihi kupambana na Shibuda kupitia msukuma mwingine kuliko mchaga au mtu wa kabila nyingine. Hawataki wasukuma wawe na mtazamo hasi juu ya CHADEMA. Hawataki wakulima na wafugaji wawe na mtazamo hasi juu ya CHADEMA. Hapa unazungumzia kabila na kundi la watu lenye idadi kubwa ya watu kuliko kabila au kundi lingine lolote Tanzania.

Wakati mbinu hii ya CHADEMA inawezekana ikawa sahihi, lakini labda Kasulumbayi sio msukuma sahihi wa kumpambanisha na Shibuda. Nasema hivi kwasababu ambayo nimeshaitaja hapo juu; historia na rekodi ya Kasulumbayi katika siasa haionyeshi anao ujasiri na uwezo wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana na viongozi wa chama chake; historia na rekodi ya Kasulumbayi haionyeshi ni mtu asiye na bei kwasababu hajawahi kupingana na watu wenye pesa nyingi (Makamba, Rostam, lowassa, Mbowe). Kwa lugha nyepesi Kasulumbayi bado hajaji-thibitisha kwa wakulima na wafugaji na wala kwa wasukuma wenzake. Ukiongea na msukuma wa kawaida huko Maswa mashariki anakwambia Kasulumbayi uhai wake kisiasa uko kwenye vyombo vya habari na waandishi walio nunuliwa na CHADEMA lakini sio kwenye jimbo la Maswa mashariki.

Wakulima, Wafugaji na Wasukuma wamemuamini Shibuda baada ya kuona hana bei, anao ujasiri na uwezo wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana na viongozi wake. Sio tu Wakulima, wafugaji na wasukuma wanahitaji mtu wa aina hii kusimamia masilahi yao, kundi lolote katika jamii linahitaji mtu wa aina hii kusimamia masilahi yake.

Kuna maneno yanatumika kama nyenzo ya kupambana na Shibuda. Maneno hayo ni msaliti, pandikizi, katumwa na CCM. Lakini ukiangalia kwa umakini unagundua hata uongozi wa CHADEMA hawaamini wanachokisema pale wanaposema Shibuda katumwa na CCM.

Huyu Shibuda kama alikuwa katumwa na CCM kuiangamiza CHADEMA alikuwa na nafasi nzuri ya kufanya hivyo pale ugomvi wa Zitto na Mbowe ulipokuwa umepamba moto, pale Kitilia Mkumbo na Mwigamba wanafukuzwa CHADEMA, pale wafuasi wa Zitto na Mbowe walipokuwa wanapambana nje ya mahakama huku wakiwa wameshika mabango. Pale waislamu walikuwa wanaona Zitto anafukuzwa CHADEMA kwasababu ni Muislamu. Lakini Shibuda badala ya kuungana na Zitto katika kipindi hiki ambacho kilikuwa kinatoa nafasi nzuri ya kuiangamiza CHADEMA, yeye Shibuda aliamua kuwa mtazamaji. Na hata waandishi wa habari walipomuuliza kwanini hamuungi mkono Zitto yeye akasema kila mtu atabeba mzigo wake. Viongozi wa CHADEMA wanajuwa Shibuda ni mwanasiasa mjanja na mzoefu ambaye anatambua wakati muafaka wa kufanya jambo; angekuwa na nia mbaya na CHADEMA angetumia kipindi hicho kuishambulia CHADEMA, lakini hakufanya hivyo kwasababu hana nia mbaya na CHADEMA.

Usalama wa Taifa unaelewa ni hatari kwa afya ya CCM na Taifa kama itatokea kabila lenye idadi kubwa ya watu, wasukuma (force of number) na kabila lenye ari, wachaga (aggressive force) watakuwa na mpango mmoja na vile vile kama itatokea hawaelewani. Lakini kwa vile imeshatokea wachaga kujitambua wao kama CHADEMA unaitaji nguvu upande wa pili itakayo wamudu wachaga na nguvu hiyo ni wasukuma. (Because Chagas [aggressive force] have already identified themselves as CHADEMA, you need another force to counter that, and that force is Wasukuma [force of number]). Hatari inayojaribu kuepukwa hapa ni ile iliyotekea Kenya, pale Odinga na Kibaki walipoungana, pale wajaluo na wakikuyu walipoungana na kuitoa KANU (CCM) na Rais Moi.

Ninachojaribu kusema hapo juu ni kwamba usalama wataifa walifanya kila linalowezekana Kuhakikisha Shibuda na CHADEMA hawawi na mahusiano mazuri pale tu Shibuda alipoingia CHADEMA. Majungu, fitina na uchawi wa kila aina ulitumika kuhakikisha Shibuda na CHADEMA hawawi na mahusiano mazuri. Lakini pia katika upande wa pili wa shilingi yeye Shibuda anaelewa mfumo unavyofanya kazi kwasababu amekuwa katika mfumo huo mda mrefu. Shibuda alielewa akiingia tu CHADEMA usalama wa taifa utaanza kumlenga na asipokuwa makini hata usalama wake utakuwa hatarini.

Ni kisema maisha ya Shibuda yalikuwa hatarini na anao ujasiri wa hali ya juu ili unielewe lazima ukumbuke Kolimba na Chacha Wangwe.

Shibuda kwa kuelewa usalama wake unaweza kuwa hatarini ilibidi alipoingia tu bungeni kwa tiketi ya CHADEMA atengeneza mazingira rafiki na serikali ya CCM. Na hii ndio iliyopelekea yeye kuwa wa kwanza kukubali matokeo ya uchaguzi na kumtambua Rais Kikwete kabla ya CHADEMA kukubali kufanya hivyo. Hii ni siasa ya hali ya juu, inaweza kufanywa tu na mtu anaelewa mfumo unafanya kazi vipi. Ndio maana unapoona mtu anamlinganisha Shibuda na Kasulumbayi unaona ni utani uliokithiri.

Shibuda anao upeo wa kujuwa kwamba CHADEMA yenye nguvu ndio inayofanya CCM watake kumtumia Shibuda. A powerful CHADEMA is what makes Shibuda relevant to CCM. Kwa hali hii Shibuda atapendelea CHADEMA inayoisumbua CCM ili aendelee kuwa na umuhimu kwa CCM. Ndio maana si kushangaa alipoacha kumuunga mkono Zitto Kabwe. Akasema kila mtu atabeba mzigo wake.

Hakuna kitu kinachomfanya Shibuda asieleweke kwa mwanachama wa kawaida wa CHADEMA kama kuonekana katika majukwaa ya CCM wakati yeye ni CHADEMA. Nakumbuka huko nyuma alionekana jukwaa moja na Kinana na Nape wakati CCM ilipoenda kuhutubia wakulima na wafugaji karibu na jimbo lake. Na alipoulizwa kwa nini alikuwepo kwenye mkutano wa CCM, alisema wasukuma wangu wanamatatizo yaliyo kithiri na serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, hawa ndio wako kwenye nafasi nzuri ya kutatua hali mbaya za wakulima na wafugaji. Alisema ukijuwa matatizo ya wasukuma yalivyo makubwa utajuwa jambo la msingi na kipau mbele ni kupata utatuzi wa matatizo yao na sio siasa za mimi naonekana wapi au naonekana na nani. Siasa sio kipau mbele changu bali utatuzi wa matatizo.

Majibu ya Shibuda hapo juu yalinikumbusha governor wa New Jersey, Chris Christie alipokuwa anajaribu kutatua matatizo ya watu wake walipokumbwa na mafuriko katika kipindi cha uchaguzi Marekani. Kipindi hiki Obama alikuwa anaandamwa na shutuma juu ya shambulizi la ubalozi wa Marekani, Benghazi, Libya. Kura za maoni zilikuwa zinaonyesha Obama yuko chini kidogo ya Romney. Lakini pamoja na hali hii governor kupitia chama cha Republican, Chris Christie alikubali kuonekana na Obama na kumsifia Obama jinsi anavyosaidia watu wake wakati wa mafuriko. Hii iliwachukiza wanachama wenzie wa Republican kwasababu ilimnyanyua Obama kwenye kura ya maoni na kumfanya mgombea wa Republican, Romney awe chini. Alipoulizwa indirect question na waandishi wa habari kwanini anamsaidia Obama wakati sio mgombea wa chama chake alisema, "I've got a job to do here in New Jersey that's much bigger than presidential politics, and I could care less about any of that stuff."

Ndio, kuna wakati siasa za vyama inabidi zisiwe kipau mbele; kipau mbele iwe ni utatuzi wa matatizo ya watu kama Shibuda anavyosema, kama Chris Christie anavyosema.


 
Bingwa soma Nipashe la leo, gazeti la mchaga mwenzao. Hichi kinachozungumzwa hapa utakiona.

Huyo Mengi aliyesaidiwa na Sitta katika kesi yake na Waziri Malima sasa hivi kamgeuka Sitta; kaamua kutekeleza Chaga Conspiracy.
 
Suala la ukabila kwenye cdm halina mjadala lipo wazi kabisa..tusubiri kuna mengi yatatokea
 
Gazeti lenyewe la wachaga na mbowe mchaga unategemea nini.
 
Suala la ukabila kwenye cdm halina mjadala lipo wazi kabisa..tusubiri kuna mengi yatatokea

Tena yapo karibu sana yaja kwa speed kubwa sana chaka hiki cha chadema ukabila umejisimika kwa mizizi mikuu.
 
Bingwa soma Nipashe la leo, gazeti la mchaga mwenzao. Hichi kinachozungumzwa hapa utakiona.

Huyo Mengi aliyesaidiwa na Sitta katika kesi yake na Waziri Malima sasa hivi kamgeuka Sitta; kaamua kutekeleza Chaga Conspiracy.
wewe kiazi!! Mengi ni wa kumuogopa Malima!!!?? Eti sita 'akamsaidia" kwa taarifa yako alimsaidia Malima. Kama huelewi kamuulize Lawrence Masha alichokipata kwa kubahatisha kupambana na mengi hadi kwenye sakata la kumwekea mtoto wa mengi "sembe'. Muulize Masha kilichompata 2010 hadi Mende (Wenje) kuangusha kabati (Masha).
 
Back
Top Bottom