Kwanini Lowassa anatolewa Sadaka?

Kwanini Lowassa anatolewa Sadaka?

Kikwete kuwa fisadi hakumfanyi Lowassa msafi. Hivyo anastahili anachofanyiwa. Ikifika zamu ya JK naye afanywe vivyo hivyo. Period.

Dada/Kaka Ukifata badiko langu sijasema Lowassa ni msafi, lakini ufisadi wa Lowassa unamuhusu JK, na matunda ya huo ufisadi JK kayaona na kuyatumia, Swali liko palepale kwa nini Lowassa anatolewa sadaka
 
Lowassa hawezi kuwa Raisi hata siku moj,jina lake limeshachafuka mno,Ninachomuomba ni kwamba asikubali kuchafuka mwenyewe kwa sababu alikuwa anachora michoro ya kuiba fedha EPA na DOWANS,RICHMOND ili kumsaidia rafiki yake Jakaya ahakikishe akinq'oka anaq'oka na Jakaya ili kuhakikisha nchi inakuwa salama badala ya kuendesha mambo chini chini wakimkabidhi barua aitishe press conference kuomba wenyekiti wa CCM ajiuzulu
 
kuna jambo moja muhimu la kuelewa hapa .mtu anaweza kuwa maarufu kwa mambo mazuri au mabaya!! na haiwezekani yote yakajitokeza kwa pamoja. hapa hoja ni kupata kiongozi mwenye maadili atakayejali maslahi ya watanzania si ya cdm,cuf,nccr,ccm nk nchi kwanza! kuna umuhimu wa kuwafahamu mapema hao wanaoonyesha nia ya kuwania hiyo nafasi ya juu nchini.tuchambue sifa na maadili yao na pia utayari wao wa kuwatumikia watanzania na kuwaneemesha.suala la tuhuma ni dosari kubwa kwa mtu anayewania uongozi wa juu wa nchi.watanzania wenye uwezo na wasio na dosari wapo na hakuna sababu ya kuendelea kuwajadili kina edward. kuna fursa nyingi ikiwemo kuwa mfanyibiashara mkubwa kwa vile huko ndiko ameelemea toka ujana wake.
 
nikisema JK anamwandaa Hussein Mwinyi sidhani kama ntakuwa nakosea
 
we sadak unazijua kwanza??au mbabeli
kuna sadaka za

1)UJENZI
2)HIARI
3)EMERGENCY
4)ZAKA

LOWASA ANATUMIKIA YA NGAPI
 
Rostam Aziz, Andrew Chenge na Edward Lowasa mapacha watatu kwa kifupi RACHEL msikilizeni kijana wenu wa UVCCM sisi huku CHADEMA tulishasema toka pale Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar-es-Salaam:
 
Last edited by a moderator:
Mafisadi 17 wameshatajwa na Dr. Wilbroad Slaa. Kwa nini wasitimuliwe wote 17 ndani ya CCM na ndani ya serikali kwa ujumla na mali zao zitaifishwe?
 
Mafisadi 17 wameshatajwa na Dr. Wilbroad Slaa. Kwa nini wasitimuliwe wote 17 ndani ya CCM na ndani ya serikali kwa ujumla na mali zao zitaifishwe?

uamuzi mwingine serikali waombe wanamaombi wawaombeee ukitaifisha mali za lowasa umetaifisha mitaa ya UPANGA yote sasa uoni unarudi kwenye ubinfsishaji..ni kweli lazima maamuzi magumu yajirudie
 
Ameondolewa kwenye chama si kwasababu ya ufisadi epa, richmond et...hiyo adhabu yake ilikuwa kujiuzulu na wanachama tungemwacha apumzike kama tulivymfanya malecela..ok

Anaondolewa kwasababu amewapa chadema (in particular Mbowe) milion 200...ili kuchafua chama chet kwa ajili ya umaarufu binafsi

Chadema kama mnataka mchukueni ...naona Mbowe na Slaa wameshaanza mikakati ya kumtetea ok.
 
JK na Lowasa hawakukutana barabarani..ila tatizo la Lowassa ni kula tunda la mti wa katikati ndiyo maana wanamtosa!
 
afadhali aachiliwe Baraba kuliko Lowassa
 
Kikwete anahofia Lowassa ana miondoko ya Ki Sokoine, yaani full power na cleaner, pia Lowassa ana hasira baada ya kutuhumiwa badala ya kupongezwa kitendo chake cha kujiuzulu mwenyewe ili achunguzwe, ndio demokrasia ya kweli.
Mungu ajalie tumpate kiongozi kama Lowassa, au basi angalu Asharose japo atakuwa hawajui wazembe wa TZ,
Mwinyi akagombee kwa Zanzibar,
Mwandosya kama Waziri mkuu ni safi,
Sumaye sijui baada ya kutoka Havard chuoni alichosomea Obama, Chenge, Clinton na wakuu wengine, sijui kama ana jipya? lakini kazi aliyoifanya bosi wake Mkapa ni safi sana...[/QUOTE

Kweli watanzania tumeshusha std zetu sana. Ni sababu vipi zinatufanya tuwaone hawa watu (EL, Sumaye etc) waliotajwa hapo juu wanafaa? Hivi Asharose Migiro hawezi kulitumikia taifa mpaka awe raisi? Asijegeuka Tibaijuka maana ameshuka chati kwa kasi ya ajabu sana. Afadhali angebaki kulekule "Habitat for Humanity." I might be wrong: let us wait and see.
 
Najaribu Kuangalia kiundani, ni sababu gani kubwa ya Lowasa na wenzie kuzalilishwa na chama chao, huku mwenyekiti wake ambaye pia ni swahiba wake mkubwa akiwa kimya?, nasema kuzalilishwa na chama chake (nje ya CCM ni hatua iliyopaswa kufanywa na hata vyombo vya sheria vilipaswa kumshtaki/kuwashitaki),

Lowasa alitumia nguvu nyingi binafsi kumuweka mwenyekiti wa CCM kwenye uongozi wa nchi, lakini sasa inakuwaje MWENYEKITI ANASHINDWA KUMTETEA? Na kama ni UFISADI basi hata JK mwenyewe yumo kundini, lakini kwa nini Lowassa
nikijaribu kupambanua napata hoja moja tu URAIS WA 2015,

Nadhani katika historia ya CCM uchaguzi wa 2015 utakuwa ni uchaguzi ambao haujawahi kutokea, ni uchaguzi ambao unaweza kukiua kabisa CCM
Mpaka sasa naona kuna wagombea sita ambao wana nguvu kubwa ndani ya CCM na ambao wameshaanza Kampeni za kichinichini na za kwenye public kutafuta popurarity
1) Lowassa
2) Membe
3) Hussein Mwinyi
4) Mark Mwandosya
5) Fredirick Sumaye na
6) Asharose Migiro

6: Migiro
Hana Influencial sana labda ataingia kwenye mchakato na kupata nguvu kwa sababu ya Jinsia

5: Sumaye
Kambi yao kwa muda mrefu imekuwa ikidhoofishwa na sasa wamejipanga/wanajipanga ili waweze kurudi na Sumaye ndio anaonekana kuwa ni potential akitegemea nguvu za Mkapa, Mramba, Apson nk, japokuwa haonekani kama yupo imara lakini kwa ndani/chinichini yupo kwenye kampeni nzito

4: Mwandosya
Kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuingia Magogoni lakini ameonekana kuwa hana Mvuto sana na kwa kweli alikuwa ameshapoteza kutokana na siasa za kutengwa (Kupewa wizara zisizo na kelele za kupata popularity), Lakini kwa Uchaguzi uliopita na siasa za mbeya zilivyo, Mwandosya ndio anaonekana kuwa ni miongoni mwa watu muhimu katika kukijenga chama Mbeya na kiukweli Mwandosya-akiwa na Mboma anajitahidi sana kurudi kwenye chati ili ifikapo 2015 awe na sauti ndani ya NEC

3: Hussein Mwinyi
Alikuwa Mbunge Tanzania Bara, swali la kujiuliza imekuwaje aende kugombea Zanzibar, lakini kiukweli huo ulikuwa ni mpango madhubuti wa CCM na labda UWT, kama Kelele za wazanzibar zikiwa Raisi wa 2015 ni lazima atoke Zanzibar basi Hussein Mwinyi atakuwa ndio Chaguo la CCM, kwa hiyo yeye yupo hapo kama spare tyre tu

2: Membe
Kwa Mtazamo wangu Nadhani huyu ndio chaguo la ****** na labda UWT, nina sababu lakini nitaziweka baadae

1: Lowassa
Nadhani kila mtu anamzungumzia huyu Bwana, na yeye mwenyewe alishajiweka kwenye hiyo class ya Presidential Material, Nyendo zake, nguvu zake na hata kampeni zake zilikuwa zinaelekeza hivyo, amejenga nguvu kubwa ndani ya CCM na labda serikalini pia,

Swali Linabaki kwa nini CCM wanamtoa Lowassa sadaka kama ndio mwenye nguvu kuliko wote tunaowategemea kutoka CCM?
Kwa mtazamo wangu Lowassa sio Chaguo la ****** na wala UWT (japo ni maswahiba wakubwa), Kwa mambo JK aliyofanyiwa na Lowassa kuanzia 1995 na mpaka anaupata urais kwake ni vigumu sana kumtosa Lowassa akiwa macho makavu, njia pekee ni hii iliyotumiwa sasa ya kupitia Chamani-NEC na ili kumtolea uwezo wake alionao ndani ya NEC basi ilipasa wamtoe kwa nguvu, na kwa sababu Lowassa ana nguvu ya RA na Visenti basi ilibidi wote watolewe ndani ya chama (kwa gia ya ufisadi) ili asiwe (Lowassa) na uwezo wa kufurukuta 2015,

Ni mtizamo wangu tu
Huo kweli ulikuwa mtazamo wako ambao hauna tofauti na wacheza kamari wa sport pesa! Kumbe kweli nimeamini ndoto za mchana zina bundi nyuma yake!
 
Kikwete anahofia Lowassa ana miondoko ya Ki Sokoine, yaani full power na cleaner, pia Lowassa ana hasira baada ya kutuhumiwa badala ya kupongezwa kitendo chake cha kujiuzulu mwenyewe ili achunguzwe, ndio demokrasia ya kweli.
Mungu ajalie tumpate kiongozi kama Lowassa, au basi angalu Asharose japo atakuwa hawajui wazembe wa TZ,
Mwinyi akagombee kwa Zanzibar,
Mwandosya kama Waziri mkuu ni safi,
Sumaye sijui baada ya kutoka Havard chuoni alichosomea Obama, Chenge, Clinton na wakuu wengine, sijui kama ana jipya? lakini kazi aliyoifanya bosi wake Mkapa ni safi sana...
Clinton hakusoma Havard, wacha kulisha watu matango pori hapa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom