Kwanini Lowassa anatolewa Sadaka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Lowassa anatolewa Sadaka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kituko, Apr 27, 2011.

 1. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Najaribu Kuangalia kiundani, ni sababu gani kubwa ya Lowasa na wenzie kuzalilishwa na chama chao, huku mwenyekiti wake ambaye pia ni swahiba wake mkubwa akiwa kimya?, nasema kuzalilishwa na chama chake (nje ya CCM ni hatua iliyopaswa kufanywa na hata vyombo vya sheria vilipaswa kumshtaki/kuwashitaki),

  Lowasa alitumia nguvu nyingi binafsi kumuweka mwenyekiti wa CCM kwenye uongozi wa nchi, lakini sasa inakuwaje MWENYEKITI ANASHINDWA KUMTETEA? Na kama ni UFISADI basi hata JK mwenyewe yumo kundini, lakini kwa nini Lowassa
  nikijaribu kupambanua napata hoja moja tu URAIS WA 2015,

  Nadhani katika historia ya CCM uchaguzi wa 2015 utakuwa ni uchaguzi ambao haujawahi kutokea, ni uchaguzi ambao unaweza kukiua kabisa CCM
  Mpaka sasa naona kuna wagombea sita ambao wana nguvu kubwa ndani ya CCM na ambao wameshaanza Kampeni za kichinichini na za kwenye public kutafuta popurarity
  1) Lowassa
  2) Membe
  3) Hussein Mwinyi
  4) Mark Mwandosya
  5) Fredirick Sumaye na
  6) Asharose Migiro

  6: Migiro
  Hana Influencial sana labda ataingia kwenye mchakato na kupata nguvu kwa sababu ya Jinsia

  5: Sumaye
  Kambi yao kwa muda mrefu imekuwa ikidhoofishwa na sasa wamejipanga/wanajipanga ili waweze kurudi na Sumaye ndio anaonekana kuwa ni potential akitegemea nguvu za Mkapa, Mramba, Apson nk, japokuwa haonekani kama yupo imara lakini kwa ndani/chinichini yupo kwenye kampeni nzito

  4: Mwandosya
  Kwa muda mrefu amekuwa akitamani kuingia Magogoni lakini ameonekana kuwa hana Mvuto sana na kwa kweli alikuwa ameshapoteza kutokana na siasa za kutengwa (Kupewa wizara zisizo na kelele za kupata popularity), Lakini kwa Uchaguzi uliopita na siasa za mbeya zilivyo, Mwandosya ndio anaonekana kuwa ni miongoni mwa watu muhimu katika kukijenga chama Mbeya na kiukweli Mwandosya-akiwa na Mboma anajitahidi sana kurudi kwenye chati ili ifikapo 2015 awe na sauti ndani ya NEC

  3: Hussein Mwinyi
  Alikuwa Mbunge Tanzania Bara, swali la kujiuliza imekuwaje aende kugombea Zanzibar, lakini kiukweli huo ulikuwa ni mpango madhubuti wa CCM na labda UWT, kama Kelele za wazanzibar zikiwa Raisi wa 2015 ni lazima atoke Zanzibar basi Hussein Mwinyi atakuwa ndio Chaguo la CCM, kwa hiyo yeye yupo hapo kama spare tyre tu

  2: Membe
  Kwa Mtazamo wangu Nadhani huyu ndio chaguo la ****** na labda UWT, nina sababu lakini nitaziweka baadae

  1: Lowassa
  Nadhani kila mtu anamzungumzia huyu Bwana, na yeye mwenyewe alishajiweka kwenye hiyo class ya Presidential Material, Nyendo zake, nguvu zake na hata kampeni zake zilikuwa zinaelekeza hivyo, amejenga nguvu kubwa ndani ya CCM na labda serikalini pia,

  Swali Linabaki kwa nini CCM wanamtoa Lowassa sadaka kama ndio mwenye nguvu kuliko wote tunaowategemea kutoka CCM?
  Kwa mtazamo wangu Lowassa sio Chaguo la ****** na wala UWT (japo ni maswahiba wakubwa), Kwa mambo JK aliyofanyiwa na Lowassa kuanzia 1995 na mpaka anaupata urais kwake ni vigumu sana kumtosa Lowassa akiwa macho makavu, njia pekee ni hii iliyotumiwa sasa ya kupitia Chamani-NEC na ili kumtolea uwezo wake alionao ndani ya NEC basi ilipasa wamtoe kwa nguvu, na kwa sababu Lowassa ana nguvu ya RA na Visenti basi ilibidi wote watolewe ndani ya chama (kwa gia ya ufisadi) ili asiwe (Lowassa) na uwezo wa kufurukuta 2015,

  Ni mtizamo wangu tu
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  lowasa anavuna alichokipanda..! tho ni mchapa kazi
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Aaaaahhh............unatuchanganya bwana sisi tupotupo kwanza tunajivua magamba kwanza hayo mengine baadaye.............
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kudhalilishwa badala ya kuzalilishwa, Influency badala ya Infleuncial na mengine, hebu pitia tena hata hivyo hayo ndio maigizo na uhuni wa CCM ambao ukiangalia kwa undani hautofautiani sana na ule wa Inzi kunawa kwa mbawa zake huku akiwa kwenye kinyesi au uchafu
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kudhalilishwa badala ya kuzalilishwa, Influency badala ya Infleuncial na mengine, hebu pitia tena hata hivyo hayo ndio maigizo na uhuni wa CCM ambao ukiangalia kwa undani hautofautiani sana na ule wa Inzi kunawa kwa mbawa zake huku akiwa kwenye kinyesi au uchafu, LINGINE NI POPULARITY BADALA YA POPURARITY....
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Ukizumngumza Lowassa huwezi kumwacha JK, huyo jamaa kaangaika sana na JK katika harakati zao za mmoja wao kuingia magogoni, sasa iweje leo yeye fisadi na JK sio?
   
 7. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kikwete anahofia Lowassa ana miondoko ya Ki Sokoine, yaani full power na cleaner, pia Lowassa ana hasira baada ya kutuhumiwa badala ya kupongezwa kitendo chake cha kujiuzulu mwenyewe ili achunguzwe, ndio demokrasia ya kweli.
  Mungu ajalie tumpate kiongozi kama Lowassa, au basi angalu Asharose japo atakuwa hawajui wazembe wa TZ,
  Mwinyi akagombee kwa Zanzibar,
  Mwandosya kama Waziri mkuu ni safi,
  Sumaye sijui baada ya kutoka Havard chuoni alichosomea Obama, Chenge, Clinton na wakuu wengine, sijui kama ana jipya? lakini kazi aliyoifanya bosi wake Mkapa ni safi sana...
   
 8. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  kuna watanzania wanafuatilia matukio kweli, niko pamoja nawe mzee kituko
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  jibu muruuuuuuuuuuaaaaaaaa
   
 10. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  WEE BRAZA UNA AKILI SANA,LAKINI KUNA KITU KINANISUMBUA,KWA NINI TUNAONGELEA SANA MAMBO YA CCM?SIO KUWAPA UMAARUFU ZAIDI?HIVI TUKIWAPUUZA NA KUJIFANYA HAWAPO ITAKUWAJE:A S 39::A S 39::A S 39::frusty::frusty::frusty::frusty:
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukisema hivi nakumbuka siku ile Lowassa alivyompa lifti Kikwete kwenye wagombea urais kurudisha fomu za zenye sahihi za wadhamini mikoani.

  Nasema nakumbuka pia pale huyu Waziri Mkuu, kuwahi kujiuzulu kwa kashfa ya KUSANYA KODI ZA WALALAHOI WA TANZANIA, aliposema kwa kinywa kipana Kwamba hawakukutana njiani JK hivyo hata sasa naamini ya kwamba wala hawako jilari kuachana njiani.

  Ndio, haya yooote ni Vijigiliba tu ambavyo walivijadili na kupanga kwenye mazungumzo na Kikwete Chamwino muda mfupi kabla Joka CCM hakijajitangazia aina na unene gani wa gamba wanaloinuia kujivua na kiasi gani kibakie.

  Lakini katika haya yoote, Nguvu ya Umma dawa yake iko jikoni huku tukiendelea kukoleza moto na kuja kuonyesha njia sahihi zaidi baada ya ngonjera yooote hiyo kumalizika.

   
 12. BongoLogik

  BongoLogik JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani ni lnfluence badala ya influency
   
 13. A

  Aman Member

  #13
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wizi wake umemponza!.
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Katika wizi si hata JK alikuwemo, mbona yeye hawajampa muda wa siku 90, nadhani kuna point tunaikosa hapa
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...Sidhani kama EL anaonewa...watanzania tusidanganyike na hii falsafa ya kujivua gamba ya CCM.Hawa jamaa bado wapo pamoja na ndio maana JK aongei chochote kuhusu hii falsafa ya kujivua gamba ambayo ni kiini macho...
   
 16. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kituko umeuliza swali zuri sana na ambalo linahitaji unbiased and neutral observation. Swali nalopenda watu wajiulize ni swali nalo jiuliza mimi always:
  Ni nini kikubwa kibaya Lowasa alichofanya kinacho offset mazuri yake yote kiasi cha kumwogopa na kumchukia hivyo! Tunasema "ni fisadi ILA CHAPAKAZI!" Ukiweka kwenye mizani upande upi ni mzito zaidi.
  Msianze kutukana, tuelimishane,nauliza ili kujua sio kutetea mtu.
   
 17. k

  kayumba JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kweli ni mtizamo wako...!
   
 18. k

  kayumba JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wote waliovuliwa kweli ni magamba ila hata karibia wote waliobaki nao ni magamba!

  Nasubiri watanzania siku wakiamka nakujivua haya magamba yaani kwa kuiondosha ccm madarakani.
   
 19. h

  hoyce JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kikwete kuwa fisadi hakumfanyi Lowassa msafi. Hivyo anastahili anachofanyiwa. Ikifika zamu ya JK naye afanywe vivyo hivyo. Period.
   
 20. m

  mwahajoseph Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usipozungumzia CCM utazungumzia nini sasa wakati ndicho chama kongwe,dumee yan ukigusa CCM tuu ama chochotee yawe maswala ya kiuchumi,kiutamaduni, na kisiasaa CCM haiepukikiii aiseee,poreee alaf tangiapo ni maarufu sanaaa tuu si ajabu hata kabla ujazaliwa enzi za babu zakoo na hata kikitoka leo umaarufu ake hautaishaa kitabaki kwenye historia
   
Loading...