Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 242
Mkuu, ni kweli hata mimi sijamsikia akitoa comment zozote kuhusu ufisadi uanoitafuna nchi. Ni tofauti kabisa na wanaodaiwa kuwa mahasimu wake -- kwa mfano Sitta au Mwakyembe. Lakini siyo Membe, Membe naye ni kama EL, huwa hazungumzii ufisadi vile vile.
Nimetafakari sana suala hili na kugundua kuwa mtu kama Sitta hana mali zozote za kutisha, hana tuhuma za ufisadi. Natoka naye mkoa mmoja, -- hana kitu ukilinganisha na wengine wanaotajwa -- akina Vijisenti, Ngeleja, Maige, EL mwenyewe, et al. Nadhani hata Mwakyembe, mwenye data za tuhuma za Mwakyembe aziweke hapa, angalau moja. Nadhani naye hana kitu.
Ukweli unabakia pale pale -- kwamba mtu fisadi humuwia ugumu sana kulizungumzia suala hilo kwa nguvu zote. Anaweza akataja tu kwa kupita lakini siyo kwa nguvu sana.
Nakubaliana nawe kwamba EL akiingia Ikulu, basi tushuhudie miaka kumi mingine ya danadana tu na ulimbikzaji mali kwa vigoigo wa CCM -- a.k.a. hasa wale wanaokula bila kunawa.
Kwenye red: Umemsahau Magufuli. Huwa anazungumzia sana ufisadi, lakini kwa kiini macho tu.Mkuu, ni kweli hata mimi sijamsikia akitoa comment zozote kuhusu ufisadi uanoitafuna nchi. Ni tofauti kabisa na wanaodaiwa kuwa mahasimu wake -- kwa mfano Sitta au Mwakyembe. Lakini siyo Membe, Membe naye ni kama EL, huwa hazungumzii ufisadi vile vile.
Mnampandisha Lowassa tu, kwanini tusifikirie tofauti kidogo? Ndio maana hata watoto wa wanasiasa hawa wanajiona kuwa watoto wa wafalme na kuamini kuwa 'Ninyi watanzania ni wa kutawaliwa tu'. We need to change this attitude.Kwanza kabisa as certain as next sunrise, EL akitinga Ikulu 2015, lile gamba lililoamua kulivua gamba lake (RA) atarudi ulingoni kwa kishindo! Kwa hiyo business as usual!
Hapa Mungu mnamwonea tu, hata mimi ningekuwa Mungu, ningewaangalia tu. Mnaamshwa, hamtaki kuamka. Mnamwagiwa maji yenye ubaridi mwingi, mnashtuka na kukung'uta vichwa, mnajipangusa nyuso kisha mnarejea usingizini.Hivi lini Mungu atasikia kilio cha Watz?
Kwenye red: Umemsahau Magufuli. Huwa anazungumzia sana ufisadi, lakini kwa kiini macho tu.
Kwa mfano, atasema wizara yake imejaa mafisadi, lakini hata siku moja hatujasikia yeyote kafikishwa mahakamani.
Kwenye red: Umemsahau Magufuli. Huwa anazungumzia sana ufisadi, lakini kwa kiini macho tu.
Kwa mfano, atasema wizara yake imejaa mafisadi, lakini hata siku moja hatujasikia yeyote kafikishwa mahakamani.
Anafahamu nini kinachoendelea katika chama chake CCM Chama Cha Mafisadi sio mnafiki kama walivyo viongozi wengi ndani ya CCM wanasimama majukwaani kukemea ufisadi na rushwa,wakati vitendo,maisha na kauli zao hazioani.Kusimama majukwaani na kuhubiri vita dhidi nya ufisadi wakati sera ya CCM kivitedo ni ufisadi ni unafiki.Ni swali ambalo huwa linanitatiza sana, labda wadau mnaweza kunikumbusha ni lini, tuseme tangu baada ya uchaguzi mkuu uliopita au hata kabla huyu mjamaa ambaye inadaiwa anautaka urais kwa udi na uvumba, amezungumzia ufisadi.
Ni katika kikao, mkutano au hafla gani amewahi kulizungumzia suala hilo ambalo majority ya Watz linawakera na linaashiria kutuletea machafuko huko tuendako.
Jibu la mara moja linaloonekana ambalo ni plausible ni kwamba mtu huyu binafsi kaguswa na ufisadi, ni mtuhumiwa wa kansa hiyo, hivyo hawezi kulizungumzia kwa kulikemea kwa nguvu zote, labda wakati anafanya hivyo, macho yake ayaelekeze chini.
Wasiwasi wangu ni kwamba akitiunga Ikulu, hawezi kulishughulikia suala hilo, atakuwa kama huyo mwenzake aliyepo sasa hivi. Ni nadra sana JK kuzungumzia ufisadi katika hafla za hadhara, hata katika kampeni zake za 2010, mada hii alikuwa anaikwepa sana. Tusisahau alikwepa midahalo na akina Slaa na Lipumba bila shaka kukwepa suala la ufisadi ambalo lazima lingeibuliwa.
Hivyo EL akitinga Ikulu, ina maana kwamba kwa miaka 20 suala la ufisadi hapa nchini halitakuwa linapiganwa kwa dhati.
What a waste of time. Watz tuamke, tusidanganyike hapa.
Nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu sana hotuba na kauli za Lowassa akiwa sehemu mbali mbali hapa nchini na kuonyesha kero zake katika masuala mbali mbali katika jamii ambayo anayaona hayaendi vizuri. Mfano ni ajira kwa vijana, elimu duni na kadhalika.
Yote hayo ni sahihi, lakini mwanasiasa huyu mkongwe inabidi ajiulize kwa nini masuala hayo yamekuwa ni chagamoto kubwa kwa jamii ya Tanzania. Jee hataki kukubali kabisa kwamba ufisadi katika ngazi za juu za uongozi wa serikali inayoongozwa na chama chake ndiyo kwa kiasi kikubwa unachangia serikali hiyo kushindwa kutatua masuala hayo?
Haamini kwamba sehemu kubwa za bajeti zinazopangiwa sekta mbali mbali za maendelea zinaishia mifukoni mwa wachache? Haamini kwamba mikataba ya siri ya makampuni ya uchimbaji wa madini, mafuta na gesi ni ufisadi mtupu na ndiyo maana iko siri?
La mwisho: Lowassa haziamini kabisa habari kwamba wapo vigogo wachache waliowekewa fedha katika mabenki ya Uswisi na makampuni ya nje yanayojishughulisha na utafutaji/uchimbaji wa gesi hapa nchini -- na kwa nini hata siku moja hazungumzii suala hilo ambalo wananchi wengi wanachukizwa nalo? Haoni kwamba serikali inapiga danadana tu katika kuwabaini akina nani hao na kudai kuzirejesha?
"Tunataka tuwasaidie hawa vijana wetu, maana ni nguzo kubwa sana katika maendeleo ya taifa. Ilani ya CCM inasema lazima watu wawezeshwe kiuchumi.
"Kwa maana hiyo katika nchi yetu kila mtu lazima ale. Na kula kwenyewe tunatofautiana, huyu anakula mkate na huyu anakula hiki. Na ili amani iwepo lazima RPC au OCD na wafanyabiashara wawathamini machinga," alisema Lowassa.
Yaani hapo kwa tathmini yako EL ameongelea kukerwa kwa ufisadi? hata kama ameoingea ki-mafumbo, sijalibaini fumbo lenyewe.
Siku atakapoongelea ufisadi -- hasa ufisadi wa ngazi za juu (siyo rushwa za matrafiki na manesi) nitampa kura yangu bila kufikiri mara mbili -- iwapo atagombea urais.