Kwanini Lowassa anaiponda CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Lowassa anaiponda CHADEMA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIM KARDASH, Jan 24, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kauli iliyotolewa hivi karibuni na mbunge wa monduli bwana Edward Lowassa ni ya kufedhehesha na kusikitisha sana. Ni kauli iliyojaa dharau kubwa kwa wanyonge wanaolazimika kutumia nguvu ya sauti yao kudai stahili zao.Kauli hiyo pia inamuonyesha mheshimiwa mbunge kama ni kiongozi muoga asie na ujasiri wa kukabiliana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi.

  Kasoro ya kwanza katika kauli hiyo ya Lowassa aliyoitoa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya kanisa la FCTP huko Bigabiro, mkoani Kigoma, ni kuyaeleza matumizi hayo ya nguvu za umma kuwa yanaendeshwa na CHADEMA.

  Kwa nini Lowassa hayuko sahihi katika hili? Hivi chama kisicho na dola kama CHADEMA kinawezaje kulazimisha utashi wa wananchi kushiriki kwenye harakati hizo? Kumshawishi mlalahoi akatishe siku yake shambani akahudhurie maandamano yanayokihusisha chama cha siasa ni suala gumu mara kadhaa ya urahisi alionao Lowassa kuwakusanya marafiki zake matajiri kumwaga fedha kwenye harambee zao.

  Hivi Lowassa anadhani wananchi wanaojitokeza kwenye maandamano au harakati nyingine kushinikiza masuala mbalimbali wanafanya hivyo kama anasa, hasa ikizingatiwa kuwa wanafahamu fika uwezekano wa kulala rumande kama si kufunguliwa mashtaka pindi Jeshi la Polisi likijisikia kuwanyanyasa?

  Tunaweza kumhurumia Lowassa katika hili kwa vile sidhani kama ameshawahi kulazimika kutumia nguvu kudai haki yake. Yeye ni miongoni mwa kikundi kidogo cha wateule wachache ambao miaka nenda miaka rudi wapo madarakani, huku mahitaji yake yakishughulikiwa na wasaidizi wake.

  Raha ya kuwa na wasaidizi, wapambe na watoa huduma ni kwamba kwa kiasi kikubwa jukumu la kuhakikisha kila jambo lipo sawa kwa ‘bosi' linakuwa mikononi mwa watu hao.

  Katika hotuba yake kwenye harambee hiyo Lowassa alikaririwa akidai (namnukuu) "Nguvu ya umma tunayoshuhudia kwenye maandamano ya chadema, ingekuwa inatumika kwa kiwango kile kile kufanya kazi za kujitolea kwenye miradi ya maendeleo kama ujenzi wa sekondari zetu, hakika taifa lingepiga hatua kubwa ya maendeleo, lakini linapokuja suala la kufanya kazi nguvu ya umma hutoweka."

  Kwa lugha nyingine Lowassa anahitimisha kuwa mahala pekee ambapo nguvu ya umma inatumika ni kwenye maandamano ya baadhi ya vyama vyetu. Huyu ndiye ambaye licha ya kuwa Waziri Mkuu huko nyuma ameshika nafasi kadhaa za uongozi serikalini na ndani ya CCM kwa miaka kadhaa.

  Je, ni kweli hajawahi kuona nguvu inayotumika na Watanzania kujiletea maendeleo yao licha ya kukwazwa na majambazi wanaotumia fursa zao kuwafisadi?

  Moja ya mambo yanayotufanya Watanzania tuendelee kumlilia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ni jinsi alivyotuunganisha bila kutumia dini au urafiki na matajiri kuhamasisha maendeleo ya jamii na nchi yetu kwa ujumla.

  Nyerere alitambua umuhimu wa nguvu ya umma katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa hususan kukiwa na usimamizi mzuri usioambatana na maslahi binafsi.

  Uhuru wetu kutoka kwa mkoloni ulipatikana kutokana na wanyonge wa Tanganyika kuchoshwa kunyanyaswa na kukandamizwa na wakoloni na kuunganisha nguvu zao wakihamasishwa na Nyerere na wapigania uhuru wenzie na hatimaye tukapata uhuru wetu. Leo hii Lowassa anabeza harakati zenye mwelekeo kama huo.

  Historia imetuonyesha jinsi nguvu ya umma ilivyoweza kuangusha tawala mbalimbali za kidhalimu, mifano mizuri ikiwa ni huko Afrika Kusini walivyopambana na utawala wa makaburu na Ulaya ya Mashariki walivyokabiliana na udikteta wa kikomunisti.
  Na hivi karibuni tumeshuhudia nguvu ya umma ikiwang'oa madikteta Hosni Mubarak wa Misri, Ben Ali wa Tunisia na Muammar Gaddafi wa Libya.

  Lakini kwa kile kinachoweza kutafsiriwa kama unafiki wa Lowassa ni ukweli kwamba yeye alikuwa miongoni mwa waliopongeza nguvu za umma nchini Misri huku akishauri watawala wetu kujifunza katika kilichojiri nchini humo. Ikumbukwe kuwa harakati za Misri zililenga zaidi kuutokomeza utawala wa kidikteta wa Mubarak ilhali nguvu ya umma huko nyumbani imeelemea zaidi kwenye kudai haki za msingi sambamba na kukemea maovu, hususan ufisadi. Sijawahi kusikia kuwepo kwa maandamano yenye wito wa kumng'oa Rais Kikwete madarakani kwani kwa mujibu wa sheria zetu kufanya hivyo ni uhaini pasipo mjadala.

  Lakini licha ya kupongeza nguvu za umma huko Misri, ingekuwa miujiza kwa Lowassa kuunga mkono harakati kama hizo huko nyumbani kwani yeye ni miongoni mwa waathirika wake. Nguvu ya umma ikihamasishwa na CHADEMA ilimtaja mwanasiasa huyo kwenye orodha ya mafisadi (list of shame) na hadi leo hajachukua hatua za kisheria kudai amekashifiwa.

  Tukiweka kando kauli hiyo ya Lowassa, labda tujiulize kidogo kuhusu hayo mamilioni yanayochangwa na marafiki zake kwenye hafla mbalimbali makanisani. Hivi Watanzania wenzetu hao wenye uwezo wa kutoa sadaka za mamilioni wanatoa wapi fedha hizo?
  Na katika hili ninayalaumu sana makanisa yanayoweka mbele fedha pasipo kujiuliza fedha hizo zinazomwagwa kwao zinatoka wapi.
  Wakati wa uhai wake, Baba wa Taifa alionyesha upinzani mkubwa kwa wanasiasa wenye utajiri wa kupindukia lakini usio na maelezo ya kutosheleza. Ifahamike kuwa utajiri si dhambi iwapo umepatikana kihalali.

  Lakini kila mwenye uelewa anaweza kupatwa na wasiwasi kuona mwanasiasa mmoja akizunguka huku na kule kumwaga mamilioni ya shilingi makanisani. Huyu mtu ana fedha kiasi gani? Amepata wapi?

  Lowassa kama muumini yeyote yule ana uhuru wa kutoa michango ya fedha nyingi na marafiki zake matajiri. Kadhalika, ni haki yake ya kikatiba kuongea lolote lile alimradi havunji sheria za nchi. Sasa kama yeye ana uhuru wa kumwaga mamilioni makanisani na kukemea walalahoi wanaotumia nguvu ya umma kushinikiza mambo mbalimbali, kwa nini basi asitambue kuwa walalahoi hao wanaotumia haki hiyo hiyo anayotumia yeye?

  Wanasema uhuru bila nidhamu ni uhuni, na kwa msingi huo japo ninatambua uhuru alionao Lowassa kuzungumzia masuala ya kisiasa kwenye nyumba za ibada, uhuru huo unaweza kuwa na madhara makubwa katika taifa letu. Kama walalahoi anaowakemea Lowassa ni werevu na wanafanya harakati zao nje ya nyumba za ibada basi ni vema wanasiasa wetu nao wakaepuka kugeuza sehemu hizo takatifu kuwa majukwaa ya kisiasa.
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  chama cha kususa na kuandamana kina tabu sana aisee..ngoja na nyie mpate dola tutawaona kama mtayapenda maandamano yasiyo na msingi,watu hamfanyi kazi kuuutwa barabarani kuandamana na kususa plus kupinga pinga kila jambo halafu mnategemea shilingi eti iwe strong...kwa uzalishaji upi?
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Jina la Lowassa limekuwa kubwa sana kiasi kwamba lolote analotamka linapewa tafsiri nyingi tofauti. Kwa jinsi nilivyomuelewa, Lowassa hakuelekeza kauli zake kwa Chadema, bali kwa wananchi pale akihimiza kwamba nguvu ya umma sio njia sahihi ya kujiletea mabadiliko/maendelo, bali kufanya kazi ya kujenga uchumi, kwa bidii.

  Sasa kosa lipo wapi hapo? Huu ni mtazamo sahihi, kwani matatizo yanayotukabili taifa sasahivi ni pamoja na uwepo wa serikali legelege, isiyo na dira yoyote wapi inataka kuipekeka nchi. kama hilo ndio tatizo, kabla ya kufikia matumizi ya nguvu ya umma, kwanini tusijishughulishe na ujenzi wa taifa na kusubiri mwaka 2015 ambapo wananchi wanakuwa na fursa ya kuchagua chama gani kikamake madaraka?

  Inaweza ikawa Chadema, inaweza ikawa CCm, lakini kutokana na siasa zetu holela, inaweza ikawa coalition ya vyama vya sasa, au pengine chama kipya kabisa. Pale ambapo itabainika wananchi wameporwa haki yao ya kuchagua chama na viongozi wanaowataka mwaka 2015 ndipo suala la nguvu ya umma linaweza kuwekwa mezani kama mjadala.

  Sio sasa. Vinginevyo, Lowassa anaweza kuwa na mapungufu yake lakini katika hili ni kukuza tu mambo kwa sababu aliyetamka ni Lowassa.
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lowassa anaogopa sana nguvu ya umma kwa sababu anategemea sana nguvu ya pesa na pesa bila umma/watu ni kazi bure! Kwa hiyo ni lazima ajikanyage kwa kuwapondea CHADEMA ambacho kimekuwa ni kimbilio la watanzania na ni tishio kwa mafisadi kama Edward Lowassa!
   
 5. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Na wale mnaowahofia maofisini na kuwapiga mkwara wasijuhusishe na siasa maofisini nao hawafanyi kazi nini?uoga umewajaa!tuachane na hayo mama,vipi ile tape yako ya xxx rated na ray J inapatikana wapi?
   
 6. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo kama 2015 wananchi wataporwa haki yao tena na serikali itakayokuwepo madarakani kuendelea kuwepo legelege itabidi wasubiri tena mpaka 2020 au?kiasi nakubaliane nawe kuhusu kufanya kazi na kujipatia maendeleo,lakini nani wanaotakiwa kuweka mipango madhubuti na dira kwa wananchi wao kujiletea maendeleo kama sio serikali?unasema nguvu ya umma sio njia sahihi ya kujiletea mabadiliko/maendeleo,ila mimi naona nguvu ya umma ni njia sahihi ya kujiletea mabadiliko/maendeleo kama serikali ni dhalimu,kiziwi na legelege
   
 7. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kwani mara ya mwisho kuandamana ni lini?,kususa ilikuwa uchaguzi wa Igunga,naona tumeanza kubadilika na ikulu tumeenda mara mbili,tumegundua watz mnapenda amani

   
 8. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Utakula ban ya kujitakia wewe kijana halafu uanze kulia lia...hiyo kwanini usiipeleke chit-chat?hapa tunaongea politiki dogo!kuhusu maofisini sawa,lakini nchi haijengwi maofisi peke yake na kwanza toka lini watu wa maofisni wakawa na muda wa kuandamana barabarani,sana maandamano yenu ni humu jf!
   
 9. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  pole sn mrembo, mwisho wa yote 2015
   
 10. +255

  +255 JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Anaiponda CDM kwa sababu yeye ni CCM
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Isitoshe siku hizi amekuwa mleviiiiii? Nyagi kibao hadi fahamu zimeanza kupungua kwa kasi.

  Source
  mimi.
   
 12. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo kwa akili yako unataka kutuambia kuwa viwanda vyetu vimekufa kutokana na maandamano? Sababu kubwa ya shilingi kushuka thamani ni kwa kuwa hatuzalishi vya kutosha kuuza!!
  Tuambie japo jambo moja tu zuri na lenye manufaa kwa watanzania lililopingwa kwenye maandamano?
   
 13. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Shilingi haiporomoshwi na Maandamo, shughulikieni kwanza wizi (Ufisadi) mnaoufanya ndipo hayo maendeleo mnayohubiri yatakuja.

  Sijawahi kumsikia Lowassa akizungumzia ufisadi hadharani, mbona hivyo? Leo iweje anapinga nguvu ya umma kudai haki zao.
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  chadema + nguvu ya umma ni msumari wa sumu kwa Lowassa
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Wacha upigwe ban kwanza, ukirudi uje kwa heshima
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa kwenye safu ya washauri wa Lowassa ningemuonya asiongee kitu chochote cha kuwaudhi CHADEMA. Pamoja na hija ya kwa Nabii Joshua Lowassa amekuwa na nafuu kutokana na kutokejeli CHADEMA lakini sasa naona anaanza kujitia kitanzi. CHADEMA inamekuwa inafanya maandamano kwa issues mbalimbali, hivyo mtu yoyote akikashifu maandamano kwa vyoyote vile atakuwa analenga CHADEMA. Kwa Lowassa kuanza kujiingiza kwenye hii list ya waropokaji ni 'risky' sana. Itakula kwake!
   
 17. Msusu

  Msusu Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  you are very right. no comment
   
 18. M

  Mchomamoto Senior Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuhusu neno legelege nimelikubali lakini mengine Hovyoooooooooooooooooooooooooo!!!!
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ukirusha jiwe gizani atakaepiga kelele ujue limempata.
   
 20. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwani rwanda ina viwanda vingapi ambavyo tanzania haina?au visiwa vya shelisheli,madagascar n.k. wana viwanda vingapi?angalia pale arusha kipindi cha zile vurugu kile kiwanda chao cha utalii kiliathirika kiasi gani na tulikosa pesa ngapi za kigeni?huo ni mfano mmoja tu nimekupa ili upanue fikra zako kidogo,sio lazima u export product ndio upate foreign currency,u can sell service na ukapata mamilioni ya dola kama shelisheli na madagascar..
   
Loading...