Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by saggy, Jun 17, 2011.

 1. s

  saggy Senior Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa mawzo yake kwakuwa ana utashi wake binafsi so naomba nitoa mtizamo wangu na sitatoa maoni ili kumfurahisha mtu humu ndani ya Forum ni maoni yangu na nina haki ya kuwa tofauti au sawa kimawazo na mtu yoyote.EL anaifaa Tanzania kwa sababu zifuatazo:-

  Ni Kiongozi huyu shupavu,jasiri na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali kwa upande wa serikali hili linadhihirika aliposhika nyazfa mbali mbali kama:-

  a.Kusimamia Sekta ya Elimu ambayo ndiyo Uti wa mgongo wa maendeleo ya Taifa lolote hapa Duniani.Alisimamia kwa ukakamavu kutekeleza mpango wa kupanua Elimu ya Sekondari na alihimiza kwa nguvu zake zote ujenzi wa Shule za Kata Nchi nzima ili kuwapa Fursa Mamilioni ya Watanzania wenzetu waishio Vijijini kupata Fursa ya Elimu.

  Zoezi hili lilihitaji uwekezaji mkubwa sana na Tukumbuke kwamba Taifa letu ni Maskini sana,changamoto zilizo ikabili Sekta ya Elimu kama Ukosefu wa vifaa vya maabara,Nyumba za Walimu,Madarasa ya Kutosha na upungufu wa Vitabu si kosa la mtu Fulani bali umaskini wa Taifa letu ndio maana WB na IMF hutoa misaada kwa nchi maskini kusaidia maendeleo ya Elimu kwakuwa ni Sekta inayohitaji uwekezaji mkubwa kifedha na Rasilimali zingine.

  EL ni mtu anayeamini katika Elimu ndi maana motto wake ni tofauti kidogo na Motto wa Chama chake na anasema '' ELIMU KABLA,KILIMO KWANZA'' Ni kweli kabisa kwamba hakuna linaloweza kufanikiwa bila Elimu,Unaweza kuwaambia watu wasio na Elimu ya kutosha Walime Kilimo cha Kisasa?Me I agree kwamba Elimu KABLA na Kilimo Kwanza.

  Mataifa Makubwa yaliondelea leo Duniani yalifanya uwekezaji Mkubwa kwanza katika Elimu,hasa Elimu ya Msingi(Kwa mfano China,Brazil na USA) na Baadaye kufanya Mapinduzi Makubwa ya Kilimo,baadaye Viwanda Vidogo na baadaye Viwanda vikubwa ambavyo vilichochea kukua kwa kasi kwa Sekta za Huduma na kupelekea mfumuko wa nafasi kibao za ajira kwa Vijana!!!

  b.Kuwafukuza bila woga hadi kuwasindikiza Airport wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya City Water hadi kuwapandisha ndege uwanja wa
  Taifa:

  Akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo ,EL alitekeleza wajibu wake kwa umahili mkubwa na bila uwoga na moja ya mambo ambayo yatakumbukwa ni kufukuzwa kwa wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya Kitapeli ya City Water ambao walishindwa kutekeleza wajibu wao,aliwatimua na kuwasindikiza hadi Airport!EL ni Kiongozi Shupavu sana na asiyeogopa mtu!

  c.Kiongozi Mwajibikaji na asiyeogopa kufanya maamuzi magumu hata kama yatamuuza

  Kujiuzulu kwake kutoka katika Wadhfa wake wa Uwaziri Mkuu kufuatia Kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond inachukuliwa na wengi kama kuhusika kwake katika Saga hilo.Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba Waziri Mkuu ndiye mtendaii Mkuu wa Shughuli za Serikali na mtekelezaji wa Maagizo ya Baraza la Mawaziri ambacho kimsingi ndicho chombo kikubwa cha Utendaji wa serikali (Govt. Machine) na hivyo kama kuna Kosa linafanyika basi Linatosha kuiangusha Serikali nzima so katika SAGA ile ilibidi Serikali Nzima akiwa ni Pamoja na Rais wajiuzuru lakini EL akubali mwenyewe kwa ajili ya kulinda heshima ya Chama chake na Serikali, huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa Waafrika wote.

  Siku zote tatizo letu waafrika ni kukosa kuwajibika pale inapobainika uzembe umefanyika,ukweli umebaki kuwa wazi mpake leo hii NCHI IPO GIZANI migao ya Umeme inaendele kama kawaida na dada wa Richmond ambaye ni Dowans Mitambo yake inawashwa na tumerudi pale pale!! Mimi nasema kwa kosa la Richmond,Serikali nzima ilikuwa imeanguka.

  d.Mfuatiliaji na asiyechoka kufuatilia kero za na hakai ofisini kungoja taarifa
  Wakati wa janga la Njaa lilisababishwa na ukame kwa msimu wa mwaka 2007/08 ni huyu EL alikuwa akishirikiana na Wakuu wa Wilaya zote zenye njaa na wakati mwingine alishiriki yeye mwenyewe kupita nyumba kwa nyumba kusimamia zoezi la ugawaji wa chakula kwenye Familia zenye njaa ili kuhakikisha kwamba azma ya serikali ya kwamba hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa inatimizwa ni huyu huyu EL.


  Mtu hawezi kukosa mapungufu hata siku moja,nakubali ana mapungufu yake lakini EL ni embe dodo lililoiva tayari kuvunwa na Watanzania Mwaka ukifika 2015.


  Nawaleteeni EL
   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hata aingizwe kwenye washing machine hasafishiki huyo..................
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  kweli ndugu.........
   
 4. s

  saggy Senior Member

  #4
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jenga hoja sio kukimbilia kusema anasafishwa,jenga hoja hapa,hii sio Forum ya Udaku!
   
 5. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #5
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  kuna mambo mengi sana yanaendelea nyuma ya pazia ambayo watanzania hatuyafahamu... We unasema EL anafaa kuwa raisi wa Tanzania, yeye mwenyewe anasemaje anautaka huo Uraisi??
   
 6. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hata akisamehewa 7[SUP]70
  [/SUP][HR][/HR][HR][/HR]Ameshachafuka kutokana na yeye kumfichia siri boss wake na sasa hataki kukubali atulie,
  analialia tu njiani mara samunge mara Nigeria mpaka na yeye eti kieleweke...ha..ha.ha.te.te...
   
 7. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hebu nimwombe Lowasa asifiche siri, awaambie watanzania ukweli uliofichika. Namuunga mkono na sasa namsemea ila asifiche siri, atuambie ili awe safi, najua si fisadi ila alitumiwa kuficha siri kisha akaachwa, anafaa kuwa rais lakini si kwa CCM. Wenzie wakubwa wamemwacha pekee na Chenge na Rostam wanaangikwa msalabani huku wao wanapeta. 3 Boys please tell us the story behind ..Mkichelewa mnamalizwa haraka kama Balali yule aliyekufa ingawa yu hai..heee hhheeee heee heeee eee
   
 8. s

  saggy Senior Member

  #8
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona hatuna hoja ya kujenga?kwanini tunatumia Forum hii kurushiana maneno,toa ufafanuzi ni kwanini haiwezekani,na kiongozi mwema hajitangazi.
   
 9. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hafagiliwi mtu hapa,ina maana TZ bila Lowasa haiwezekani! na je akifa leo nchi hii itayumba!,huyo hawezekani hata akienda Nigeria hakuna wa kumpa kura,na ukitaka CCM ife wamsimamishe huyo Lowasa wao,wako watanzania wengi sana wenye uwezo mkubwa zaidi ya huyo lakini hawapewi nafasi kwa sababu ya kuminywa na huyo fisadi,hizo pesa alizokusanya akazilie Monduli asije kutuchanganya nazo,anataka kutukaanga kama samaki kwa mafuta yake sasa nimegundua kisa cha kuiba pesa nyingi kiasi kile.na tutabanana mpaka kieleweke.
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na huyu jamaa kwamba eti Lowasa anasafishwa, si kachafuliwa kwa nini tusimsafishe? Kumbuka kuwa mwana mwenye bidii hakosi mtu wa kumuosha ikiwa kachafuka. Lowasa hakujichafua, anachafuliwa na wana mtandao kwa ajili ya uchaguzi 2015. Cha msingi atuambie ukweli ili njia yake ya kwenda magogoni 2015 iwe wazi. Nani asiyemjua Lowasa kwa kazi na ujasiri? Hilo nalo unauliza ila mie naona ahame chama aongeze nguvu Chadema hata akipewa umakamo wa rais ama uwaziri mkuu inatosha. JK anamuandaa yule mama aliyewahi kuwa waziri wa nje na sasa mkuu wa kimataifa ili aingie magogoni.
   
 12. s

  saggy Senior Member

  #12
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wapo wengi wanaoweza zaidi yake mimi nakubali kabisa,ndio maana nimesema pia hakosi mapungufu,Wataje hao ni akina nani na wana sifa zipi jamani,Hawa watu wote tuwajadiri wazi wazi jamani.
   
 13. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  johnie johnie..yes papaaaa
   
 14. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mie namkubali sana huyu hasa baada ya kujua kuwa mengi amezushiwa na ****** ili ****** apate nafasi ya kuweka vimeo vyake
  go go go el

  mix with yours
   
 15. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Teh teh.....................

  Hoja ipi unataka,ukweli mbona uko dhahiri kwamba hata umuingize kwenye washing machine ama umsugue kwa steel wire kama sio dodoki huyo mtu hasafishiki........Ni mchafu sugu.......Period.

  Hata aende Nigeria sijui kwa nabii Joshua et al.......Kamwambie hafai kuishi Magogoni...

  Sababu za uchafu wake zinajulikana,sina haja ya kuziweka hapa,nitajaza bandwith bureeee.....

  Bala.....
   
 16. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hatumtaki..........
   
 17. s

  saggy Senior Member

  #17
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unasema Ukweli Mkuu,mimi jamani nimesema haya kwa mujibu wa ufahamu wangu mdogo ninaofahamumengine siyafahamu,kama kuna anayemfichia siri aseme sasa na Watanzania watamwelewa,nani asiyejua kwamba Waziri Mkuu anatengeneza maagizo ya Baraza la Mawaziri,kwanini Mzigo huo akatatwikwa EL peke yake?Je Bunge ambacho ni Chombo cha Wananchi katika kuihoji serikali ilikuwa wapi na Je Bunge ni chombo cha kungoja kungoja Kufanya Uchunguzi wa Matatizo ambayo tayari yameishatokea?Kwanini halisadii kuishauri Serikali kuepuka matatizo hayo?
   
 18. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ngd Hicho Kiasi cha Pesa Tujuze wenzako na Umejuaje au alikuambia wakati anakwiba!
  Manake wizi huwa Siri Unless ni Mshirika wa wizi huo!Jisafishe!
  Lakini,Watanzania ndio wenye Uamuzi wa Mwisho wa Nani awe Rais wao, Kikubwa tume Huru,Katiba Safi na Fair game!
  Kutaka si Kikupata, mbona Hata mie Mkweche nataka Ubunge!
   
 19. M

  Marytina JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Katika CCM wote wanaotajwa kuufukuzia urais 2015 mimi NAMKUBALI LOWASSA ZAIDI
   
 20. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,382
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Hivi EL ataendelea kuteseka na kinyongo moyoni mpaka lini? Kwani asije front akawambia watanzania A-Z ya maroroso yoooote ya JK na walivyokuwa wakifanya madudu yao. Hiyo pekee ndiyo itatuthibitishia kuwa EL ni msafi na kupata tena kura yangu
   
Loading...