Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

Nakubaliana na wewe saggy, lowasa anafaa kuwa rais, sema amechafuliwa sana na magamba wenzake. ukiangalia utendaji wa jk na lowasa, angalau lowasa amejaribu kuonyesha utendaji kuliko jk, sijawahi kumwona akilalama kama kiongozi, pale penye tatizo anachukua hatua, mfano usamabzaji wa maji kanda ya ziwa, na ujenzi wa shule za kata. amethubutu, tatizo ni chama, ila kama ulivyoonyesha akisimama kama independent candidate, inawezekana ila nguvu kubwa itahitajika. Binafsi I'm proud of Dr. slaa.
 
Aseme ukweli alionao,Hakuna asiyejua UBORA wake,EL ni koingozi Shupavu na asiyeogopa mtu ,mkali na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Chama na serikali,na wote tunaona kwamba toka alipotoka kwenye wadhfa wake wa Uwaziri mkuu kwakweli Serikali na Chama vimepoteza Uimara wake na Serikali imepwaya sana kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka ya 2006 na 2007!!!Anayebisha atoe Hoja yake hapa!
 
For 50 years tumeongozwa na chama kimoja na kimeprove failure..2015 lazima tubadilishe ladha.
 
Njia kuu ya kujisafisha kwa lowasa ni kwenda mahakamani na awafungulie kesi walio "msingizia " yeye na wnziwe kuwa ni mafisadi. Akishasafishwa na mahakama basi ahame chama chake na aanzishe chama kingine kama yeye kweli ana mvuto wa watu. Kwa nini anganganie ccm? Kwa nini asianzishe chama kingine? Chadema ndo hata hatakiwi huko, labda aende cuf
 
Jenga hoja sio kukimbilia kusema anasafishwa,jenga hoja hapa,hii sio Forum ya Udaku!
Huu ni mkakati wa kupata maoni hasi ili muweze kuyafanyia kazi mapema kwa lengo la kumuwezesha fisadi wenu kuchukua nchi. Na sio utawala wa nchi
 
Aseme ukweli alionao,Hakuna asiyejua UBORA wake,EL ni koingozi Shupavu na asiyeogopa mtu ,mkali na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Chama na serikali,na wote tunaona kwamba toka alipotoka kwenye wadhfa wake wa Uwaziri mkuu kwakweli Serikali na Chama vimepoteza Uimara wake na Serikali imepwaya sana kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka ya 2006 na 2007!!!Anayebisha atoe Hoja yake hapa!
Tatizo kuu ni ufisadi wake! Anyway, ile ndege ya uchumi wa Tanzania bado iko uwanjani au imeanza kuondoka?
 
Ni Kweli anajiandaa kutoa ukweli wote ili Watanzania waujue,but huyu jamaa amekomaa sana kisiasa na kifikra na kama Chama Chake hawawezi kumshukuru kwa namna alivyowaokoa basi hakuna tena.Maaskari wa miamvuli wa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu walikuwa

EL
Prof.Maaaak Mwaaaaandosya
John Tusker Baridi Maguuvufuli

Nilisahau

1.Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria kwa Miji ya Kahama na Shinyanga!

Hata sasa ni kama mambo yamepwaya sana,mwansiasa huyu shupavu alikuwa msaada mkubwa sana kwa Raisi wetu JK na yeye mwenye JK awewahi kukikri ukweli huu.

Bado nina imani kwamba Sisiem Hawatafanya kosa kutomsimamisha ili arejeshe heshima ya Chama na mvuto wa Serikali yake kwa wanaanchi.Kutengwa kwakwe ni moja ya sababu inayoyumbisha sana Serikali ya kwa sasa na sababu ya Chama tawala kupoteza ushindi katika majimbo makubwa na ushawishi kwa wananchi tofauti na miaka ya 2006 mpaka 2007.


Ahsante Bibi Hilary Clinton kwa kuwathibitishia wanachi wa Tanzania kwamba Kampuni hiyo ya kufua umeme haikuwa ya ubabaishaji,Waziri wa mambo ya Nje wa Taifa kubwa kama USA hawezi kuja kutuongopea hapa.Tuchunguze na tupate ukweli wa maswali haya Mawili.

1.Je ni kweli kwamba EL hakuwa anatekeleza maamuzi ya Baraza la Mawaziri?

2.Je ni kweli kwamba Bunge halikutekeleza wajibu wake wa kuhoji utendaji kazi wa Serikali na badala yake kukumbilia kugeuka mahakama ya kutuhumu makosa?Je tunaweza kuwa na Bunge la kuunda Kamati za kutafuta Mkosaji na si la kuishauri Serikali na kuihoji kwa niaba ya Wananchi?

3.Ni Mitambo ya nani ya umeme wa dharura iliyowashwa sasa hivi kama si ilele tuayoishutumu

4.Je Ufumbuzi wa tatizo la umeme umepatikana?Nchi bado iko Gizani na kuna Umeme wa Uhakika?

Hongera sana EL,Maana ukweli unazidi kugundulika siku kwa siku,Maelfu ya Watanzani bado wana imani na utendaji kazi wako mahiri,ushupavu,mvuto na uzoefu wako mkubwa bado unahitajika kwa Taifa letu.Songa mbele na usiogope mtu unaungwa mkono na watu wengi sana.
 
SIO KWA CCM,LABDA AINGIE TLP AU CUF NA HII ATASHINDA BAADA YA CHADEMA KUTAWALA KAMA MIAKA HAMSINI HIVI KWANI hili dudud CCM LINAKUFA SIKU SIO NYINGI
 
Jamani ..........hukyu kila mtu aliyekaa karibu naye anajua na sizani kama wewe mwana JF uko safi sana .....kwa kweli tanzania hii sasa inahitaji mtu aliye na msimamo ,si mwoga ,mwenye maamuzi na jasiri huyu mzee anaweza .............kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kwa ni lazima awe Rais wa Tanzania? Anatafuta nn pale Magogoni? Kama kweli tunaipenda nchi yetu na tunaumia na jinsi kundi dogo linavyotafuta rasilimali zetu, kitu muhimu kwetu kukifanya ni kuiondoa CCM madarakani
 
Kila mtu ana haki ya "KUOTA NDOTO" Lowasa anazo haki zote za kuota ndoto za kuwa rais lakini sidhani kama ana haki ya "Kuitimiza" hata Malechela alikuwa na ndoto hata akajiita embe bivu, Sumaye, Dr Salim na wengineo lakini hawakuwa na haki ya kutimiza ndoto zao.Kwa Lowassa labda Mungu ashuke na ampigie kampeni live!
 
Serekalini na kwenye chama tawala almost everyone ni mwizi, but Lowassa kapitiliza "ni mlafi asiye na kiwango". Tatizo lake la pili ni dikteta hataki na havumilii kukosolewa na akitaka jambo lake atalazimisha bila kujali madhara wala athari kwa watu wengine, kwake kumwaga damu ya mtu si tatizo hata kidogo. Partly ni inferiority complex hajiamini ndo maana hataki challenge. Hili la kwamba ni mchapakazi give me a break! Sifa pekee aliyonayo ni kiongozi pekee anayetumia elimu yake vizuri. Lowassa ana degree ya maigizo na maisha yake yote amekuwa anaigiza.Ni muigizaji mzuri kiasi cha kwamba watu wanaamini anachoigiza, wanadhani ndio uhalisia. Kinachoonekana kama ni mchapa kazi ni maigizo tu, anatumia taaluma yake vizuri.

Hivi atakuwa raisi wa aina gani? Kiongozi ambaye upande moja alikuwa anaiba mabilioni upande wa pili wananchi maskini wananyang'anywa mbuzi wao na kuku kujenga shule? Wanaezuliwa mabati ya vibanda vyao watoe michango ya kujenga shule ili hali pesa alizoiba yeye, walizoiba maswahiba wake na zilizoibiwa chini ya usimamizi wake zingetosha kabisa kujenga shule bila kuwapora watanzania maskini kidogo walichobakiwa nacho. Huyu mtu ana mtandao mkubwa sana wa walafi nyuma yake, watu wasio na kiasi na ambao hawasiti hata kwa sekunde moja kuiuza nchi yao. Akiwa raisi nawahakikishia utakuwa mwisho wa Tanzania kama unavyoijua. Atajaza watu wake (whether they are competent or not) provided akiwaambia geuka kulia wanageuka. Kwa mtu yeyote atakeyepishana naye it will be almost impossible to scratch a living! Itachukua miaka mia moja, mark my words "100 years" kuja kuikomboa nchi hii tena kwa damu nyingi sana.

Huyu mtu hajali kabisa kuhusu nchi hii wala wananchi wake wala mustakabali wake, akipewa he will turn it into his personal property, ataweka mkono wake kila mahali.

Lowassa mnamjua lakini au mnapewa wijisenti tu kuja kumsafisha hapa? Acheni kabisa aisee
 
sabuni haina shombo na almas haichafuki kwa vimbi................LOWASSA ANAFAA,ILA AKISIMSMA NA MAGUFULI...............KURA YANGU ATAIKOSA.
 
jamiani kina lowassa nchi hii tunao wengi kwanini tunamkariri wa monduli,ambaye tumeshampa nafasi akaitumia visivyo,huu ni wakati wa kina lowassa wengine kupewa nafasi,naamini wapo wenye uwezo wa kufanya makubwa zaidi ya hayo,tatizo hatujawapa tu nafasi.
 
Akiwa raisi I 'll do one of the two things, kuingia msituni au kuhama nchi na kuukana uraia wangu!
 
Duuh alivyomchafu yabidi kumloweka kwny pipa lenye sulfuric acid au kwny nuclear reactor chamber ya Fukushima Daichii
 
Hakuna hata mmoja anayeweza kueleza jambo hapa akajenga hoja ikaeleweka jamani,ni kurusha maneno na tu na chuki,hatuwezi kujenga nchi ya Majungu jamani,mtu mmoja afanye analysis ya kina ni kwanini asifae kuwa Rais,wasilishe hoja hapa na atuambie kwa undani anavyojua,maneno ya mitaani na jamani ndo tuamini?kwanini tunajadiri mambo katika upande mmoja?Mimi nasema mwana Jamii yoyote atueleze a,b,c,d,e na awe na Facts ambazo zitatushawishi kuamini kwamba hafai.

Unless otherwise ni chuki binafsi na kusikiliza maneno ya uchochezi kutoka mitaani,tuache siasa za ushabiki jamani,haitoshi kusema tu mtu fulani hafaio ooh fulani anafaaa,tell us! kwa nini anafaa na kwanini asifae,FULL STOP!

Hakuna hata mtu mmoja aliyetoa ufafanuzi wa yele niliyoeleza kwamba si ya kweli,nijuacho mimi ni kwamba hakuna asiye na mapungufu,ila EL anafaaa kwa mtizamo wangu mimi na wala simsafishi hapa.

Jengeni hoja hapa tuisome na leteni Facts sio maneno ya chuki ya mitaani tu!
 
Back
Top Bottom