MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,992
- 10,497
Mbona wananchi wa sugu huwaulizi mwakilishi wao yuko wapiKuna maswala kama wananchi walionyeshewa na mvua au kupigwa jua au kuamka alfajiri kupiga kura na kumchagua muwakilishi bungeni ni lazima wajiulize.
Naamini na wengi tunaamini kuwa lengo kubwa na muhimu la mbunge kama muwakilishi wa wananchi ni kufikisha hoja za wananchi wake kwa serikali na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.
Jambo hili hufanyika bungeni kwa asilimia kubwa lakini pia hufanyika pindi inapojitokeza fursa kama vile ziara za viongozi wa serikali kitaifa.
Leo hii Arusha imepata bahati nyingine au fursa nyingine ya kutoa nyongo au kuelezea changamoto za wananchi wake.
Mrisho Gambo aliwakilisha Serikali ya mkoa kuelezea mafanikio na changamoto za kuwaletea maendeleo wanaArusha.
Pia mbunge mteule wa Arusha Bi Magige alitumia fursa kueleza baadhi ya dukuduku za wanaaArusha.
Nimeshangaa kutokuwepo kwa mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo la Arusha mjini katika ziara hii nyeti ili naye atumie fursa kufikisha ujumbe mbadala wa matatizo ya Arusha ...ujumbe ambao hakuwahi kuutoa bungeni au aliutoa bungeni lakini haujafanyiwa kazi.
Kwangu mimi hii ni fursa iliyopotezwa kwa makusudi na muwakilishi wa wananchi.
HOJA YANGU NI NINI HASWA?
1- Kwanini Lema ameamua kutokuwepo kwenye ziara hii na kuwawakilisha wananchi?
2- Je, jambo hili sio kuwapotezea haki ya uwakilishi watu wa Arusha?
3- Je, umuhimu wa Lema katika jimbo hili hauna maana?
4- Je, Lema alinyimwa kuwepo kwenye ziara hii au alitumiwa mualiko na akagoma kufika?
5- Je, mbunge Lema anawakilisha chama chake tu au anapaswa kuwawakilisha wananchi wote wa Arusha mjini?
6- Je, Lema ana hasira sana na polisi wa Arusha na hajali polisi waliounguliwa nyumba?
7- Je, Lema hafurahishwi na amani iliyopo Arusha kwa sasa?
8- Je, Lema amekatazwa na Chama chake kuwepo kwenye ziara hii?
9- Ama Lema anaamini katika kuwasilisha matatizo ya WanaArusha kwa wazungu mfano EU?
10- Au Lema kaona wananchi wamemkataa?
Maswali ni mengi ila jibu official linahitajika kwa wapiga kura wa Arusha juu ya hii tabia ya kususa iliyooneshwa na mbunge wao.
Pongezi kwa mbunge ole millya kwa kujitokeza jana pale Mererani na pia pongezi kwa meya wa jiji kwa kuwepo kwenye hafla hii ya polisi.
Hiki kiwonder chenu ikifika 2020 mtazalishwa sana