Uchaguzi 2020 Kwanini Lazaro Nyalandu atakuwa mgombea mzuri kuliko Membe, Mbowe au Lissu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Kwanza kabisa sifikiri kama Tanzania kwa mwaka huu kwenye nafasi ya urais upinzani utashidwa. Pamoja na ukweli kwamba Magufuli kafanya zaidi ya Kikwete kwenye kipindi chake cha kwanza lakini Magufuli amekandamiza sana demokrasia kwa kipindi cha miaka karibu mitano sasa.

Lakini upinzani unaweza kutumia ugombeaji kuonyesha utofauti kwenye sera, kuonyesha sehemu gani zinahitaji mabadiliko lakini kikubwa ni muda wa wapinzani kuonyesha na kutoa mawazo mapya. Katika wagombea wakuu Mbowe, Membe , Lissu na Nyalandu kwa mawazo yangu Nyalandu kwa kipindi hiki anafaa.

Lissu binafsi sijui kama atarudi maana huwezi kufanya kampeni kwa makesi na watu wa dola wanakuwinda kwa mtutu

Membe hawazi kwasababu mpaka sasa anafikiriwa zaidi kusamehewa kuliko kutoa mawazo yake . Vilevile hana jipya zaidi ya kutetea demokrasia kitu ambacho kila mgombea atafanya

Mbowe ni mpiganaji mzuri lakini sijasikia mawazo yake mapya na alishawahi kugombea huko nyuma. Nafikiri angebaki kama kiongozi wa chama

Nyalandu akichaguliwa atakuwa mgombea mzuri kwasababu zifuatazo

1. Kwanza umri ana miaka 49-50 ni mdogo kuliko wengine

2. Ana mawazo tofauti mfano mmoja tu tunavyosema mawazo tofauti. Nyalandu amesema kitu kimoja atakachofanya ni kuweka mitandao ya data mashuleni ili wanafunzi hata wa vijijini waweze kutumia library popote duniani. Haya ndiyo mfano wa mawazo mapya tunayo ongelea

3. Amesoma Iowa, USA ambako kuna wakulima wakubwa Duniani. Hili ni jimbo la wakulima na atasaidia sana kuleta mapinduzi kwenye kilimo

4. Uzoefu kwenye utalii utasaidia yeye kutoa mawazo tofauti jinsi ya kukuza utalii nchini. Utalii una uwezo mkubwa sana wa kutuletea pesa za kigeni.

5. Vilevile hajaondoka CCM kwa kufukuzwa lakini kwa roho yake mwenyewe na baada ya kutofautiana kisera na CCM. Sikumbuki ni lini mbunge wa CCM aliacha ubunge kama huyu kwa kujiamini.

Vyama vya upinzani vinatakiwa viwe na mawazo tofauti/ fikra tofauti za kutatua matatizo na Nyalandu ataweza kueleza na kuwakilisha mbinu mpya kuliko wenzake.

He pursued his undergraduate studies at Wartburg College in the United States, where he graduated with a Bachelor of Arts in Business Administration in 1997. Before that, he obtained an associate degree in Business Administration from Waldorf College in the United States.

Non-Political Leadership and Governance Experience[edit]
In April 2015, Nyalandu was appointed as Vice Chair of the New International Executive Board of Directors of Africa Travel Association (ATA)- a New York-based trade association promoting travel and tourism to Africa and strengthening intra-Africa partnerships.[2]

Nyalandu has previously served in a number of Organizations’ Boards including chairing the Finance Committee of the Board of Trustees of Tanzania National Parks Authority (TANAPA) from 2007 to 2010.

Nyalandu was also a student leader, known for his role as the National President of Tanzania Christian Students Fellowship (TCSF), commonly known as UKWATA in Tanzania, from 1991 to 1993.
 
Sisi wengine hatuamini kwa wagombea toka ccm, bila kujali ubora wao. Pia Nyalandu sio msafi wa hivyo.
 
Back
Top Bottom