Kwanini kunguru akifa hatoki funza?

Kwanini kunguru akifa hatoki funza?

Boloyoung

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
697
Reaction score
655
Kiumbe yoyote akifa anaoza then funza wanamshambulia lakini kwa kunguru ni tofauti nimeshuhudia kunguru mfu wengi lakini sijaona funza, huyu kunguru ana nini?!
 
Damu yake ina sumu kali sana kiasi akifa hakuna bacteria ambaye anamsogelea na hivyo kutooza zaidi,

Kunguru hukauka tu na huwezi kuona INZI akimsogelea kunguru hata siku moja, kwani ana sumu kali sana akiwa mzoga.
Ivi sumu aliyonayo ndo inasababisha asinaswe na umeme? Maana namuonaga kwenye nyaya za umeme akiwa anatabasamu!
 
Kila mymana anashambuliwa na parasite mbalimbali ktotokana na bio composition ya mwili wake. Parasite wengi huweza kubadilika wakati ukiwa hai wanaishi na wewe bila madara ( symbiotic relation) lakini ukifa tuu wanabadilika kuwa decomposes wengi ni wale waitwao ( facultative parasites). Hoja kwamba kunguru hashambuliwi na decomposers si ya kweli kwani ingekuwa hivyo wakifa miili yao ingekuwa inadumu kama plastic au mifuko ya rambo ambayo ni non biodegradable, kwa kuwa niili yao huisha baada ya kufa, basi kuna parasite wanaowashambulia ambao sii lazima waonekane kwa macho. KILA MKUU ANA MKUU WAKE NA KILA MBABE KUNA MBABE ZAIDI YAKE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom