Kwanini kuna mtu mweupe na mweusi?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Binadamu anafanana DNA yake na sokwe kwa zaidi ya 90%. kwahiyo babu wetu wa kale na sokwe walifanana sana na inasemwa walitoka chanzo kimoja. Babu yetu huyu aliishi msituni kama sokwe na alikuwa na rangi kama sokwe. Ukimuangalia sokwe unaweza dhani ni mweusi lakini chini ya manyoya ni mweupe.
1579069278587.png


Kwahiyo huyu grendi alikuwa mweupe na mwenye manyoya mengi. Baadaye maisha msituni yakawa magumu na huyu babu akaona mbona nyika za Africa Mashariki zina wanyama kibao!, ngoja nikaishi huko. Kwahiyo akatoka msituni na kwenda nyikani. Nyikani hakuna miti mingi ya kumkinga jua kama msituni.. Ukiongezea kuwa anamanyoya mengi basi jua na joto vilimtesa sana.

Ili kukabiliana na joto ikabidi ajiongeze, akatoka manyoya akatokeza tezi za jasho na kuanza kutoa jasho kwa wingi ili kujipooza. Lakini kupoteza manyoya kukamletea matatizo. Kabla ya kuona hiyo shida tuone kitu kinaitwa folate/folic acid.

Folic acid/folate ni aina vitamin B na ni muhimu sana kwa viumbe. Ukosefu wa folic ndiyo husababisha mgongo wazi kwa watoto, husababisha mbegu za kiume na mayai kutotengenezwa vizuri. DNA haitatengenezwa. Pia huababisha mishipa ya fahamu kutokuwa vizuri, Ndiyo maana wanaolalamika miguu kuwaka moto hupewa dawa zikiwa na folate ndani. wamama wajawazito hupewa FeFo, ile Fo ni folic. Baadhi ya dawa huua vimelea wa magonjwa kwa kuzuia utengenezaji wa folate. Hata baadhi ya dawa za kansa hutibu kwa kutageti hii fololate. Hii ni muhimu sana kwa uhai.
Kupigwa na jua kali huharibu folate mwilini kwa kiasi kikubwa. Watu weupe huunguzwa zaidi na jua. Kwahiyo huyu babu yetu mweupe akajikuta ana matatizo makubwa zaidi baada ya kukosa folate maana husababisha na anemia pia. Hapa ndipo binadamu akaja na suluhu la kutokeza ngozi nyeusi. Kwahiyo miaka hiyo homo sapiens au binadamu wote wakawa weusi.

Miaka 60,000-50,000 iliyopita binadamu akaanza kuhama kutoka Africa kujaza dunia yote. Baada ya kufika maeneo ya baridi yasiyo na jua akajikuta na shida tena. Binadamu anahitaji vitamini D. Vitamin hii hutengenezwa kwa sehemu kubwa kwenye ngozi kupitia mionzi ya jua. Ngozi nyeupe hutengeneza kwa ufanisi kuliko nyeusi. Mtu mweusi akiishi maeneo yasiyo na jua la kutosha hupatwa na upungufu wa vitamin D. Hii hupelekea magonjwa kama matege na kansa. Kwahiyo binadamu alivyokuwa anasambaa kwenda maeneo ya baridi akaanza tena kutengeneza ngozi nyeupe na kujazza manyoya hatua kwa hatua..

Kwahiyo zamani, watu weusi walikaa maeneo karibu na ikweta tu na weupe walikaa mbali na ikweta. Hata leo hilo linaonekana. Mweupe akija ikweta anakufa kwa folate deficiency na mweusi akienda kwenye baridi anakufa kwa vitamin D deficiency.

!watu walioishi kwenye barafu walitengeeneza weusi kidogo,kama waeskimo, sababu barafu huakisi miale na iliwafanya wapate mionzi ya kutosha. Wabushmen ni weupe sababu kusini ya Afrika jua siyo kali.

Inakadiriwa kuwa inaweza chukua miaka 2500 watu kubadilika rangi kutokana na mazingira, hivyo kwa creationists kama mimi, muda toka uumbaji kubadilika kwa rangi kunawezekana.

1579076263158.png
1579076380265.png
1579076741582.png
1579076754692.png


1579076701057.png
1579076844745.png
 

Attachments

  • 1579076476782.png
    1579076476782.png
    456.9 KB · Views: 3
  • 1579076684263.png
    1579076684263.png
    574.7 KB · Views: 4
  • 1579076680742.png
    1579076680742.png
    574.7 KB · Views: 3
  • 1579076718121.png
    1579076718121.png
    456.9 KB · Views: 3
  • 1579076749012.png
    1579076749012.png
    456.9 KB · Views: 4
  • 1579076749672.png
    1579076749672.png
    574.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom