Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,189
- 128,277
DC Bashite ataamishiwa Kyaka akacheze Mamba.
HIV nawe jingalao mbona unatuletea mada za kijingajinga humu,,yan macho yamekutoka kweli eti unamtetea makonda,,kweli nmeamin ukiwa na akil ni Mali kubwa sana
HIV nawe jingalao mbona unatuletea mada za kijingajinga humu,,yan macho yamekutoka kweli eti unamtetea makonda,,kweli nmeamin ukiwa na akil ni Mali kubwa sana
acha kuchepuka we dada,kama makonda kakufikisha zaidi ya mumeo hamia kwakeIko tabia mbaya sana ya wabunge wengi kutengeneza kashfa ili kumng'oa mtumishi wa umma au kiongozi wa taasisi flani au kiongozi wa kisiasa kwa manufaa flani.
Iko tabia ya kutafuta au kutengeneza zengwe dhidi ya mtu flani ili tu watu flani waanze kufanya yao!!
Iko hii tabia ya wabunge kuleta kashfa bungeni baada ya kununuliwa.
Kwa upande wa Kinondoni namuona mbunge kubenea akijitahidi kwa hali na mali ili tu Makonda ang'olewe ukuu wa wilaya ya Kinondoni.
Sielewi jitihada hizi ni kwa manufaa ya nani nyuma ya pazia??
Utaendelea kushikiwa akili zako hadi lini?umefinyangwa kiasi kwamba huwezi hata kuitafuta kweli,umebaki kuwa mateka wa kudumu katika kokolo la wanasiasa uchwara wa CCM wenye hofu ya kupoteza maslahi yao.
Sawa,ngoja nikubaliane na wewe kwamba Richmond ni ya Lowassa,lakini ili kuweka kumbukumbu sawa nikukumbushe jambo moja:Wakati wa uwasilishaji wa Ripoti ya kamati teule iliyochunguza mkataba wa Richmond,mwenyekiti wa kamati hiyo aliliambia bunge letu tukufu kuwa katika uchunguzi wao kamati imegundua mambo mengi ambayo kama wakiyasema yote Serikali itaanguka.
Ili kuinusuru Serikali na anguko kuu,mwakyembe na wenzake waliamua kuuficha ukweli mchungu,ambao kwa maoni yao kama ungelisemwa bungeni Serikali nzima Isingeaminika Kabisa hivyo ingepelekea Serikali yote kuangushwa na Bunge lenyewe kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na Rais.
Je,kama Richmond ni ya Lowassa,kitisho cha kuanguka kwa serikali yote kilitoka wapi wakati Lowassa angeweza kuwajibishwa tu na Rais akateua Baraza jipya?
Kama kweli Richmond ni ya Lowassa,ilikuwaje mtu huyu muovu aendelee kuhofiwa na Rais kiasi cha kumfanyia kila aina ya mizengwe ili asifurukute kisiasa?
Hoja ya kuwa Lowassa akipewa nchi atalipiza kisasi ilitoka wapi kama kweli aliwajibika kihalali kutokana na makosa aliyoyafanya?
Taifa limewekwa chini ya konga la propaganda chafu kwa muda mrefu,ni wakati sasa wapenda haki tuungane kuudai ukweli uliofichwa na kamati teule ya Richmond.Hatuwezi kuendelea kuruhusu watu wachache waendelee kuwafanya wenzao kafara za kisiasa kwa maslahi yao binafsi.
Aliyeficha ukweli amekabidhiwa ofisi kuu ya sheria,tunamuomba sasa atoke hadhalani na lipoti nzima ya kamati teule ili tuweze kutoa hukumu kwa haki.Kama hilo ni gumu kwake,tunaomba aiongoze ofisi yake ilitendee haki Taifa kwa kumburuza mahakamani Mh.Lowassa ili akahukumiwe kutokana na makosa aliyoyafanya.
Kubenea ni taplo la kisiasa. wenye akili tulisha achana nae. naomba mwenye CV yake aipost humu