Kwanini kiwanda kikifungwa, mnashangilia?

Kwanini kiwanda kikifungwa, mnashangilia?

Mtoa maada umeingia chaka! hiyo thread nyingine inaongelea Dangote kufunga kiwanda Nigeria siyo hapa kama kawaida yako ya ku-rush ukaanzisha thread yako kupinga! JITAFAKALI!
 
Hivi tatizo ni huwa ni nini kwa maana sijawahi kuelewa yaani mtu akisikia tu fununu mahali Kiwanda kinafungwa basi hukimbilia JF kwa furaha na vifijo kushangilia, hivi ni kwa nini? Na siyo kiwanda tu akisia hata basi la Mwendokasi limepata pancha au kuharibika mbio kwa furaha JF kuhabarisha huku akifurahia au kama kuna habari Benki xyz inafungwa au kupata hasara furaha huwajaa, hivi ni kwa nini?

Je, ni ubinafsi tu kwamba watakaoathirika ni wengine na siyo wewe au ni nini? Yaani unafaidika nini na wenzako kupoteza kazi?
Na wewe kwanini ufipa wakipata matatizo
Unakuja kushangilia?
 
Vipi kuhusu Wafanyakazi waliopoteza kazi? Hiyo furaha yenu ya ,,I told you so” inawahusu nini?
'Who cares'? Haya ni baadhi ya majibu yako against madhila yanayowapata baadhi ya watanzania. Na sisi kama jamii pana katika hili tunasema who cares?
 
Na wewe kwanini ufipa wakipata matatizo
Unakuja kushangilia?

Kwa sababu hakuna watu wasio na hatia huko, lkn Kiwanda kina Watanzania wengi hata vyama hawana na wala hawahusiki na maamuzi yoyote!
 
Kwa hiyo ndo maana unashangilia kiwanda kikifungwa?

Kuna tofauti gani na kupunguza watu kazi kwa kisingizio cha vyeti fake kisha nafasi zao zisijazwe na wenye vyeti halali? Usijifanye una uchungu na ajira za wananchi kwa kiwanda kufunga huku mnaharibu uchumi kwa sera mbovu kiasi kupelekea viwanda kufungwa.

Lazima uwe na uelewa mpana, sasa hivi ndio debe la viwanda limeshika kasi lakini viwanda ndio vinafungwa, hujiulizi tu? Sera mbovu ndio zinachangia haya yote. Nyie kalieni siasa za kipuuzi za wizi wa kura 2020 huku uchumi unaharibika mnaishia kuhadaa umma kwa kuzindua miradi ya zamani.
 
Hiyo ndo sababu ya wewe kufurahia kiwanda kikifungwa?
 
Wewe jamaa ni mpuuzi Sana,
Kwa taarifa ni kwamba kwenye uandishi kuna kitu kinaitwa Satire.
Embu kajifunze nini maana ya satirical writings.
Kimsingi watu wanaandika kama wanatumia lugha ya furaha lakini hawamaanishi wana furaha.
Kimsingi watu wanaumia Sana rohoni na hiyo ni stahili tu ya kufikisha ujumbe.
Tundu lisu alishaonya sana kuhusu kuvunjwa Kwa mikataba ya serikali bila kufuata taratibu, watu wakamwita mpiga deal, jamaa wakakamata ndege yetu baadae mkamwita kibaraka wa wazungu.
Huyo huyo tundu lisu alionya sana kuhusu mikataba ya madini hakusikilizwa, mnakuja kukurupuka sijui kuzuia makinikia, sijui kuita uongozi wa acacia kujadili mara Kwa mbwembwe eti acacia wamekubali kutulipa sijui Tirion 100 na zaidi. Hadi leo hawajalipa hata cent watu waliandika satirical kwamba kila mtanzania atapata Noah yake.
Kimsingi hizo ni aina za uandishi wa kifasihi mara nyingi watu wanazitumia bila hata wao kujua wanatumia satire.
Sasa wewe zumbukuku unafikiria watu wanafurahi na kkushangilia.
Na 2020 labda muibe Kura tena Sisi hasira zetu tutazionyesha kwenye ballot boxes.
 
Hiyo ndo sababu ya wewe kufurahia kiwanda kikifungwa?

Usiwe mnafiki na huu uzi wako wa uchuro kujifanya una uchungu na ajira wakati redundancy ikipita kwa jina la vyeti fake ulikuwa kimya ukishangilia eti nchi inanyooshwa. Onyesha kiwanda chako ulichofunga watu wakashangilia.

Hivyo viwanda mnavyojifanya mnahamasisha hamna jitihada zozote ya kuhubiri majukwaani kusaka mtaji wa siasa nyepesi. Niliwahi kusema kama kweli serekali hii mnaamini katika viwanda nilitaraji mawaziri wajiunge wanne wanne wajenge hata kiwanda cha 1b Kundi kwani wanakopesheka. Au badi hata tungemuona first lady kawa mfano kwa kiwanda kimoja cha 500m. Mmebaki mnahamasisha wengine nyie hamuwezi. Hata msipohamasisha wajengaji wataendelea kujenga kwani hata vilivyopo walijenga bila uhamasishaji wenu. So usilete hoja ya kinafiki wakati huna kiwanda wala hujawahi kumiliki kiwanda kwa kujifanya una uchungu na ajira.
 
Hivi tatizo huwa ni nini kwa maana sijawahi kuelewa yaani mtu akisikia tu fununu mahali Kiwanda kinafungwa basi hukimbilia JF kwa furaha na vifijo kushangilia, hivi ni kwa nini? Na siyo kiwanda tu akisia hata basi la Mwendokasi limepata pancha au kuharibika mbio kwa furaha JF kuhabarisha huku akifurahia au kama kuna habari Benki xyz inafungwa au kupata hasara furaha huwajaa, hivi ni kwa nini?

Je, ni ubinafsi tu kwamba watakaoathirika ni wengine na siyo wewe au ni nini? Yaani unafaidika nini na wenzako kupoteza kazi?
Huwa tunashangilia kwa sababu Tope Kichwani husema hii ni Tanzania ya Viwanda, sasa ajabu ni kuwa viwanda vingi vinakufa na kufungwa badala ya kustawi
 
Huwa tunashangilia kwa sababu Tope Kichwani husema hii ni Tanzania ya Viwanda, sasa ajabu ni kuwa viwanda vingi vinakufa na kufungwa badala ya kustawi

Vipi Wafanyakazi wanaopoteza ajira? Kosa lao ni lipi hadi mshangilie?
 
Je hao wanaoshangilia walishauri juu ya tahadhari au la?
 
Vipi kuhusu Wafanyakazi waliopoteza kazi? Hiyo furaha yenu ya ,,I told you so” inawahusu nini?
Watu kupoteza kazi ni matokeo ya kiwanda/biashara kufungwa ambayo ni matokeo ya hizo sera zisizo rafiki kwa biashara. Hivyo sisi tukifurahi au kusikitika bado watu watapoteza kazi tu
 
Hivi tatizo huwa ni nini kwa maana sijawahi kuelewa yaani mtu akisikia tu fununu mahali Kiwanda kinafungwa basi hukimbilia JF kwa furaha na vifijo kushangilia, hivi ni kwa nini? Na siyo kiwanda tu akisia hata basi la Mwendokasi limepata pancha au kuharibika mbio kwa furaha JF kuhabarisha huku akifurahia au kama kuna habari Benki xyz inafungwa au kupata hasara furaha huwajaa, hivi ni kwa nini?

Je, ni ubinafsi tu kwamba watakaoathirika ni wengine na siyo wewe au ni nini? Yaani unafaidika nini na wenzako kupoteza kazi?
Rais mwenyewe huwa anafurahi akisikia watu wanaishi kama mashetani.
 
OK, vp kuhusu wanaopoteza kazi na kipato chao, wao kosa lao ni lipi hadi mfurahie?

Na nyie vipi kuhusu watu kupotea, kupigwa risasi hadharani, mbona watu wakipinga ukatilii huu na nyie mnawacheka? Mnazifikiria familia zao hata kidogo?
 
TATHMINI YANGU BINAFSI
1. Wivu,chuki na husda.Asilimia kubwa ya vijana tunaoneana sana wivu hasa ukiona mwenzio akiwa kakuzidi kipato,kazi nzuri,maendeleo na ndio maana ukisikia mwenzio kaachishwa kazi/kiwanda/kampuni imefungwa unadiriki kushangilia.
2.Unafiki na roho ya kichawi maana ukweli ni kwamba hakuna anayependa maendeleo yako zaidi ya babako na mamako
3.Imani ya kuona kwamba mtakuwa sawa kimaisha wakati kila mtu ana mipango yake
Mwisho wa siku huwa nina msemo wangu "UNAFIKI WA UJANANI,NDIO UCHAWI WA UZEENI"
 
Mkali kwanza uko sahihi hata kuna MTU alisema tutaishi kama mashetani.
Nadhani yameaza kutekelezeka sasa.
Lkn kwenye viwanda nadhani watu wanaona wanapuuzwa Mawazo yao na ushauri
 
Back
Top Bottom