Kwanini kiwanda kikifungwa, mnashangilia?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,583
Reaction score
27,838
Hivi tatizo huwa ni nini kwa maana sijawahi kuelewa yaani mtu akisikia tu fununu mahali kiwanda kinafungwa basi hukimbilia JF kwa furaha na vifijo kushangilia, hivi ni kwanini?

Na siyo kiwanda tu akisia hata basi la mwendokasi limepata pancha au kuharibika mbio kwa furaha JF kuhabarisha huku akifurahia au kama kuna habari benki XYZ inafungwa au kupata hasara furaha huwajaa, hivi ni kwanini?

Je, ni ubinafsi tu kwamba watakaoathirika ni wengine na siyo wewe au ni nini? Yaani unafaidika nini na wenzako kupoteza kazi?
 
Hivi tatizo ni huwa ni nini kwa maana sijawahi kuelewa yaani mtu akisikia tu fununu mahali Kiwanda kinafungwa basi hukimbilia JF kwa furaha na vifijo kushangilia, hivi ni kwa nini?
Je, ni ubinafsi tu kwamba watakaoathirika ni wengine na siyo wewe au ni nini? Yaani unafaidika nini na wenzako kupoteza kazi?

Tunafurahia wote tuishi kama mashetani kumbuka usemi wa Mwenyekiti wenu
 
kushangilia ni kuboresha ujinga wa wachangiaji.
ila kujadili sababu kwa kwa nini kimefungwa na nini kifanyike vingine visifungwe kwa kutoa creative opinions ni bora zaidi.

Ila kujadili pancha ya mwendokasi ni matokeo ya kwashakoo ya ubongo kitengo cha siasa.
 
Hivi tatizo ni huwa ni nini kwa maana sijawahi kuelewa yaani mtu akisikia tu fununu mahali Kiwanda kinafungwa basi hukimbilia JF kwa furaha na vifijo kushangilia, hivi ni kwa nini? Na siyo kiwanda tu akisia hata basi la Mwendokasi limepata pancha au kuharibika mbio kwa furaha JF kuhabarisha huku akifurahia au kama kuna habari Benki xyz inafungwa au kupata hasara furaha huwajaa, hivi ni kwa nini?

Je, ni ubinafsi tu kwamba watakaoathirika ni wengine na siyo wewe au ni nini? Yaani unafaidika nini na wenzako kupoteza kazi?
Kama unajinasibu kuwa ni wakati wa viwanda halafu vinakufa vilyopo lazima uchekwe
 
Hivi tatizo ni huwa ni nini kwa maana sijawahi kuelewa yaani mtu akisikia tu fununu mahali Kiwanda kinafungwa basi hukimbilia JF kwa furaha na vifijo kushangilia, hivi ni kwa nini? Na siyo kiwanda tu akisia hata basi la Mwendokasi limepata pancha au kuharibika mbio kwa furaha JF kuhabarisha huku akifurahia au kama kuna habari Benki xyz inafungwa au kupata hasara furaha huwajaa, hivi ni kwa nini?

Je, ni ubinafsi tu kwamba watakaoathirika ni wengine na siyo wewe au ni nini? Yaani unafaidika nini na wenzako kupoteza kazi?
Hebu muulize yule jamaa wa white house na genge lake,
Ni kwa nini alisema tuishi kama mashetani? je ni roho mbaya au ni roho ya kimaskini?
 
Kwa hiyo ndo maana unashangilia kiwanda kikifungwa?
 
Watu hawashangilii ila wanafurahi kuona kile wanachokisema ni ukweli na kinapata support kwa vitu hivyo kufanya vibaya.
Mfano wewe ukiambiwa mmeo ni Malaya ukakataa siku zikivuja picha akionekana yupo uchi wa mnyama na mwanamke mwingine ambaye sio wewe wakivunja amri ya sita, lazima watu wafurahi maana kwa kitendo hicho mtaanza kuongea lugha moja na kukubaliana kwamba ni kweli mmeo ni mtu wa vistobe.
Hivyo furaha yao ni wewe kuona uhalisia, sasa kwa suala la kuchukua hatua ni juu yako.
Same applied to all matters affecting the society be it economically, socially au politically.
 
matendo na sera za serikali zinasababisha viwanda kufungwa na kupelekea maisha kuwa tofauti na ahadi zilizotolewa.
 
Watu hawashangilii ila wanafurahi kuona kile wanachokisema ni ukweli na kinapata support kwa vitu hivyo kufanya vibaya.
Mfano wewe ukiambiwa mmeo ni Malaya ukakataa siku zikivuja picha akionekana yupo uchi wa mnyama na mwanamke mwingine ambaye sio wewe wakivunja amri ya sita, lazima watu wafurahi maana kwa kitendo hicho mtaanza kuongea lugha moja na kukubaliana kwamba ni kweli mmeo ni mtu wa vistobe.
Hivyo furaha yao ni wewe kuona uhalisia, sasa kwa suala la kuchukua hatua ni juu yako.
Same applied to all matters affecting the society be it economically, socially au politically.

OK, vp kuhusu wanaopoteza kazi na kipato chao, wao kosa lao ni lipi hadi mfurahie?
 
LUMUMBA street
Mmeanza kupagawa nanyie ndio Safi
 
The joy of "I TOLD YOU SO!!". wanatoa ushauri lakini wanaonekana sio wazalendo, hivyo pale mambo yanapokwenda mrama kwasababu serikali haiambiliki ni jambo la kawaida kuwa na "kafuraha" kidogo na matumaini kuwa serikali itajifunza na kuanza kufuata ushauri mbadala kutoka kwa wadau
 
Sera na mawazo ya MTU mmoja ni tatizo, tufikiri,tuwaze na tutende kama Taifa.

Hapo tutafurahi,tutasononeka pamoja.
 
The joy of "I TOLD YOU SO!!". wanatoa ushauri lakini wanaonekana sio wazalendo, hivyo pale mambo yanapokwenda mrama kwasababu serikali haiambiliki ni jambo la kawaida kuwa na "kafuraha" kidogo na matumaini kuwa serikali itajifunza na kuanza kufuata ushauri mbadala kutoka kwa wadau

Vipi kuhusu Wafanyakazi waliopoteza kazi? Hiyo furaha yenu ya ,,I told you so” inawahusu nini?
 
Lkn kwa nini mnafurahia Kiwanda kikifungwa?
Umefanya vibaya kutumia neno " kwanini mnashangilia"

Kila kitu kinamaandalizi kabla ya kufanyika, waandae wananchi kupokea mabadiliko kuliko kuandaa mabadiliko ili wananchi wayapokee.

Kipindi cha mpito mengi yatajitokeza yasikushangaze.
 
Kwa hiyo ndo maana unashangilia kiwanda kikifungwa?
Yaah! Huenda watu wanafurahia kuona ule unabii wa kuishi kama mashetani ukitumia kwa kila njia ikiwemo kufa kwa viwanda. Mwisho wa siku atakayefurahi ni yule anayeona sasa watu wanaishi kama mashetani.
 
Back
Top Bottom