Kwanini kiungo hiki hupoteza thamani baada ya kujifungua?

Jumax

Senior Member
Mar 4, 2017
117
229
Habari wanaJF
Ningeomba kufahamishwa ni kwanini Matiti ya mwanamke hupoteza thamani yake (kama sehemu ya siri ) baada ya kujifungua mtoto. Maana kuona ziwa la mwanamke ambae hanyonyeshi ni sawa na umemchungulia sehemu yake ya siri sasa ni kwanini hali huwa tofauti wanapojifungua yaani unakuta mdada ananyonyesha hadharani pasi na kujifunika japo upande wa kanga hata ikiwa kwenye daladala.
 
Aliyekwambia hupoteza thamani nani?

Wakati anapojifungua thamani yake ndio huongezeka na ambalo ndio huwa kusudi la yeye kuwa na matiti.

Hakuumbwa na matiti ili amvutie mwanaume, ameumbwa ili amnyonyeshe mtoto.

Kunyonyesha hadharani inategemeana na mazingira yenyewe.

Acheni watoto wale hadharani, hizo kupoteza thamani ni tafsiri zenu tu.
 
Matiti ya mwanamke yanakazi moja tu kumnyonyesha mtoto anapojifungua.

Na hayapotezi thamani yake kabisa tena thamani yake huongezeka Mara baada ya kujifungua.

Kuonekana hadharani wakati wa kunyonyesha inatokana na tamaduni za kidini na kabisa husika wapo ambayo toka utoto matiti huwa yako wazi tu na wapo wengine toka kuzaliwa mpaka kufanya hutaona titi lake.

Thamani ya mwanamke ni jinsi tamaduni yake ilivyomjenga na mwanaume anavyomchukilia.

Waliowengi matiti yana thamani kabla na baada ya kujifungua na si rahisi kuayaona
 
Aliyekwambia hupoteza thamani nani?

Wakati anapojifungua thamani yake ndio huongezeka na ambalo ndio huwa kusudi la yeye kuwa na matiti.

Hakuumbwa na matiti ili amvutie mwanaume, ameumbwa ili amnyonyeshe mtoto.

Kunyonyesha hadharani inategemeana na mazingira yenyewe.

Acheni watoto wale hadharani, hizo kupoteza thamani ni tafsiri zenu tu.
Umejibu vizuri mkuu,anachotakiwa kwa sasa ni kusubiri aoe na mtoto wake atakapozaliwa ndio atagundua jinsi yanavyopanda thamani,anaweza kutamani liongezeke jingine yawe matatu...
 
Huwa hayapotezi thamani yeyote ukiyaona yapo nje nje usidhani kuwa ni yameshuka daraja.

Pale huwa analisha mtoto hawezi kukubali mtoto afe njaa kisa kuna watu wamemzunguka ni lazima atanyonyesha tu.

Hata wewe ulinyonyeshwa hadharani ulipokuwa mdogo.
 
Wastaarabu hawanyonyeshi hovyohovyo hadharani....

Hata kama ni hadharani hujitAnda kanga..
 
Wastaarabu hawanyonyeshi hovyohovyo hadharani....

Hata kama ni hadharani hujitAnda kanga..
mkuu nashukuru sana kwa kuniunga mkono hapo tunazungumzia zaidi suala la USTAARABU
 
Kwani kazi ya matiti ni nini?
Mi nahisi kazi yake kuu ni kunyonyesha hayo mengine ni extra
Af mi naona m/mke akijifungua ndo yanaongeza thamani make yanaanza kutimiza majukumu yake mama.
 
Kuna wanaume wengine wakiona manyonyo tu wanapata msisimko sasa huku uswahilini wakina mama wanajiachia tu wananyonyesha watoto maziwa yote nje wanakuwa wanawapa watu mfazahiko,ni vizuri wawe wanajifunika kama hivi
bfd493001b58f08cf8530dc4b741d5e4.jpg
 
Habari wanaJF
Ningeomba kufahamishwa ni kwanini Matiti ya mwanamke hupoteza thamani yake (kama sehemu ya siri ) baada ya kujifungua mtoto. Maana kuona ziwa la mwanamke ambae hanyonyeshi ni sawa na umemchungulia sehemu yake ya siri sasa ni kwanini hali huwa tofauti wanapojifungua yaani unakuta mdada ananyonyesha hadharani pasi na kujifunika japo upande wa kanga hata ikiwa kwenye daladala.
Si kweli hata kidogo. Ila Aina hii ya mtazamo ndo haina thamani katika jamii. Thamani kubwa ya titi ni kunyonyesha.
Wapo akina mama wachache ambao huwa na shida katika maziwa yao na hivyo hawanyonyeshi. Lkn sijawahi kuona hata mmoja Mwenye kujinasibu kuwa eti matiti yake sasa yanathani kwa kuwa hanyonyeshi.
 
Aliyekwambia hupoteza thamani nani?

Wakati anapojifungua thamani yake ndio huongezeka na ambalo ndio huwa kusudi la yeye kuwa na matiti.

Hakuumbwa na matiti ili amvutie mwanaume, ameumbwa ili amnyonyeshe mtoto.

Kunyonyesha hadharani inategemeana na mazingira yenyewe.

Acheni watoto wale hadharani, hizo kupoteza thamani ni tafsiri zenu tu.
Na commedian Kansiime alimaanisha nini kwa kusema hivi: "I'm sure if babies had to know how many adult mouths have sucked the same breast before them they'd prefer to take porridge....."
Mimi naona matiti yana kazi zaidi ya kunyonyesha vichanga. It is an appertizer
 
Back
Top Bottom