Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Kuna hivi hapa vingne navyo vimeondololewa kwenye biblia.

-1 Esdras
-2 Esdras
-Tobit
-Judith
-The rest of Esther
-The wisdom of solmon
-Ecclesiasticus
-Baruch with the epistle Jeremiah
-The song of the 3 Holy children
-The history of Susan
-Bel and the Dragon
-The prayer for manesses
-1 Maccabees
-2 Maccabees

Ila dah hiki kitabu cha The wisdom of solmon kwa kweli kina confuse aisee
Mimi binafsi... Biblia yangu ina vitabu vya deuterokanoni 7.... Tobiti, ester, wamakabayo, judith, Joshua bin sira, baruk.... Ni biblia ya muunganiko wa makanisa ya kiprotenstant na wakatoliki... Nkifika home ntaipiga picha kwa ushahidi zaidi
 
Mkuu kama ndivyo ulivyoelewa hivi, basi hukukielewa kitabu cha Enoch! Na pengine ni kwa sababu ya lugha!
Enoch alipozaliwa alikuwa ni mtu mwenye muonekano wa tofauti manaa hata ngozi yake ilikuwa inang'aa sana.
Sasa wakati wa enzi hizo, wana wa Mungu (malaika) waliwatamani wanawake wa kibinadamu. Moja wa malaika wao kiongozi alikuwa anaitwa Azazel na wakashuka wakawachumbia wana wa binadamu, wakaingia kwao wakazaa watoto. Hao watoto walikuwa wanaitwa Wanefil.
Hao kina Azazel wakawafundisha wana wa binadamu juu ya mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kujipamba, kujipodoa na hata kutengeneza vioo vya kujiangalia. Walifanya machukizo mengi sana mbele za Mungu.
Basi hao wanefil wana wa hawa malaika walikuwa ni madubwana na walikuwa wamekuwa mzigo mkubwa mbele za jamii maaana walikula vyakula vyote vikaisha, wanyama, ng'ombe n.k.
Basi binadamu wakamlilia Mungu juu ya hao wanefil maana walikuwa wameilemea nchi.
Sasa kwa matokeo hayo Mungu akaagiza kuwa kina Azazel na malika wengine wafungwe kwenye gereza huko kuzimu mpaka siku za mwisho, pia akawatupa hao wanefil huko kuzimu ndio wakawa majini au pepo wabaya unaowasikia sasa hivi.
Enoch ndiye aliyeitwa na Mungu mpaka mbinguni na wakati anaelekea huko mbinguni kuongea na Mungu nadhani alikuwa amefika kwenye mbingu ya tatu ndipo alipokutana na kina Azazel wakawa wanamsihi awaombee msahmaha kwa Mungu kutokana na matendo yao ili waachiliwe...
Basi kufika huko mbinguni, Enoch alipanda mpaka mbingu ya saba kuongea na Mungu juu ya mambo mbali mbali na ndipo Mungu akampa Enoch kazi ya kwenda kuwahukumu hao malaika wakosefu kina Azazel...
Kwa hiyo sio kweli kuwa Wanefil ndio walikuja kuwa watu weusi... Bali ndio walikuja kuwa majini!
Na hao wanefil ni madubwana makubwa kweli kweli. Yani Mnefil mmoja wanaigina kina Le Mutuz Watano hivi!
kama wanefili ndo walikuja kua mapepo na majini vipi wale malaika walioasi pamoja na shetani je wao ni kina nani mkuu.?
 
kama wanefili ndo walikuja kua mapepo na majini vipi wale malaika walioasi pamoja na shetani je wao ni kina nani mkuu.?
Sina elimu ya kutosha juu ya pepo wachafu na majini. Ila kwenye biblia imesema hawa Wanefil walikuwa evil spirits... Sasa sijajua tofauti kati ya evil sprits, demon etc ni nini? Ila wote ni kabila moja tu mkuu...
 
Ni hv kwa kifupi tu huko nyuma kuna tukio kubwa sana lilitokea na hadi leo athari zake zinatawala maisha yetu.tukio hilo ni interaction kati ya binadamu na viumbe fulani wengine wa Mwenyezi Mungu(huwa tunawaita tu malaika hii inatupa upofu sana)walikuwa 200 wakiongozwa na mkuu wao Azazel waliposhuka ktk kilele cha mlima Hermon na kuigiza maumbile ya kibinadamu.kilichowaleta ni kutamani binadamu.walitaka kukaa nao,wawatawale,wazae nao,waanzishe empire yao tofauti na utaratibu waliopangiwa na Mungu.wakafanya hivyo.ikazaliwa offspring ya ajabu,majitu makubwa yenye nguvu za kutisha na akili za ajabu na roho za ajabu maana nusu binadamu nusu malaika.waliitwa nephilims,leo tunawaita titans(usifikiri hadithi ya kigiriki hii)!kutokana na hiyo offspring kuwa imbalance,ilileta vurugu kubwa duniani,na kama Mungu asingeingilia kati mbegu ya binadamu pure ingetoweka.hao malaika pamoja na hayo matoto yao ndio walifundisha binadamu mambo meengi ambayo leo yana sehemu kubwa ktk sayansi,elimu na tamaduni zetu hasa mashariki ya mbali,India na america.base yao kuu ilikuwa bara la Atlantis lililokuwepo katikati ya america na ulaya.kitendo hiki kilimchukiza Mungu mno akaamua kutuma gharika ya maji na kuteketeza dunia nzima pamoja na bara la Atlantis isipokuwa binadamu mmoja anaitwa Nuhu na watoto wake na baadhi ya wanyama ambao hawakuchafuliwa(nephilims walizaana hata na mijusi,kilichotoka hapo ni balaa).LAKINI kuna laana alitamka Mungu,kwamba roho za viumbe hao hataziangamiza,ataziacha na zitakuwa chanzo cha kila uovu duniani kwa umri wote wa dunia hadi mwisho ili viumbe wake wote wapate darasa how serious was this mistake!roho hizo ndizo zilimuongoza Nimrod kuijenga Babylon na kuanzisha idol worshiping na tamaduni za Atlantis zikaanza kurudi taratibu huku spidi yake ikivurugwa na elimu ya dini ya mitume na manabii wa Mungu.ilibidi utaratibu wa kuinteract na binadamu ili kutimiza lengo lao waufanye kwa siri,taratibu,miaka na miaka,wakiibadili dunia taratibu hadi mazingira yakiruhusu,roho hizi zikiwa ndani ya miili ya kibinadamu,zitaigeuza dunia nzima kuwa kama Atlantis!ndipo hapa vyama vya siri na dini zisizoeleweka vinaposhamiri underground.
Source mkuu
 
Acha uongo wewe. Yaani Enock na hao akina Luka na Matayo alitangulia nani? Yaani usimuamini Enock ukamuamini Luka ambaye kimsingi habari za Yesu kasimuliwa tu.
Kwanza sikubaliani na stori za huyo uliyemnukuu. Ila unaongea kana kwamba kitabu hicho aliandika Enoch mwenyewe. Uhakika huo unautoa wapi?
 
Kwatarifa yako Martin Luther ndiye aliyepunguza vitabu 7 vya Agano la kale......Upo dunia gani wewe...Au wewe ni Msabato nini....?
Mh..! Niko interested kujua hivyo vitabu alivyopunguza, alipunguza lini na reference za hicho unachokisema. Nijuavyo mimi, wakati wa Luther tayari Biblia ilikuwa imeshakamilika kama kitabu!
 
Kuna hivi hapa vingne navyo vimeondololewa kwenye biblia....
Huwa nashangaa watu wakikuta vitabu havipo katika Biblia hukimbilia kusema viliachwa/viliondolewa. Ni namna ya ajabu kabisa ya kuwaza. Ila cha ajabu zaidi hawasemi nani aliviondoa, lini na hivyo vilivyopo ni nani aliviweka na ni lini.

Tuna vitabu vingi vya Mwalimu Nyerere, et al lakini hatusemi vilinyofolewa toka katika Katiba ya JMT. Tuna maswali mengi mazuri na hatusemi yamenyofolewa toka katika mitihani ya taifa. Ila ikija kwenye Biblia.... dah!
 
Kwa kuangalia tu mtu mweupe akili zake na za mtu mweusi, nani hapo ni uzao uliochafuliwa na hao aliens,
mkuu unatoka kwenye mstari.. hakuna aliens kwenye kitabu cha enoch na biblia kijumla
fallen angels sio aliens.. ni angels walileta tamaa zao za ngono kwa binadamu na mambo mengine yakaendele
 
Back
Top Bottom