Kwanini kiporo kinasababisha kiungulia?

Mwanaoshimba

Member
Mar 8, 2017
61
82
Wakuu naomba wenye majibu ya kisayansi wanisaidie kwenye hii mada. Watu wengi wakila chakula cha jana au juzi-kiporo, iwe wali, ugali, ndizi au kingine chochote kile hutokea mara nyingi kupatwa na kiungulia. Hata ukichemsha kweye microwave, hali hiyo itatokea tu.

Sasa najiuliza, kuna uhusiano gani kati ya chakula kikiwa kiporo na kusababisha kiungulia?

Kuna mabadiliko gani ya kikemikali yanayosababisha hali hiyo?

Je kuna maarifa, kwa maana ya treatment ambayo kiporo kinaweza kufanyiwa ili kuondoa hilo badiliko la kikemikali?

Kusema ukweli napenda sana kiporo, ila kinachoniboa ni kiungulia baada ya kula.

Najua kuna maarifa lukuki kwenye hili jukwaa, naomba msaada wenu wakuu.
 
Kiungulia maana yake ni kwamba tumboni kuna acidi nyingi sana na sometimes hupelekea kurudi juu (reflux) ya koromelo(oesophagus) na kusababisha kiungulia.

Hivyo Mara nyingi sana vyakula vilivyolala vinakuwa na acidi nyingi kuliko chakula chenyewe halisi hivyo husababisha acidi kuongezeka tumboni na hatimaye kiungulia hutokea.

Ukitaka usipate kiungulia baada ya kula kiporo fanya hivi,koroga majivu kwenye kikombe halafu kunywa au kula dawa maarufu kama magnesium.(Magnesium trisilicate)

Majivu na hizo dawa vina BASE (tindikali) ndani yake hivyo chemical reaction itatokea kati ya acid ya kwenye chakula na base iliyoko kwenye majivu.
 
Kiungulia maana yake ni kwamba tumboni kuna acidi nyingi sana na sometimes hupelekea kurudi juu (reflux) ya koromelo(oesophagus) na kusababisha kiungulia.
Hivyo Mara nyingi sana vyakula vilivyolala vinakuwa na acidi nyingi kuliko chakula chenyewe halisi hivyo husababisha acidi kuongezeka tumboni na hatimaye kiungulia hutokea.
Kuna namna ya treatment ya kupunguza hiyo acid kwenye kiporo kabla ya kukila?
 
Kiungulia maana yake ni kwamba tumboni kuna acidi nyingi sana na sometimes hupelekea kurudi juu (reflux) ya koromelo(oesophagus) na kusababisha kiungulia...
Mkuu unapozungumzia acid unamaanisha vitu kama Hydrocloric acid, nitric acid, sulphuric acid, phosphoric acid, acetic acid, latic acid, ascorbic acid nk nk. Sasa hapa ulivyosema vyakula vilivyolala vinakuwa na acid, je hiyo acid inatoka wapi ambapo awali haikuwepo?? Kuna any reaction mechanism inayoleta acid chakula kikilala?

Pia sidhani kama ni sahihi kusema magnesium ambayo basically ni metal kua ni base. Apparently hata kama ulimaanisha kua ukiitumia then ikaingia tumboni na kuchanganyika na maji kutengeneza MgO ama Mg(OH)2 hiyo reaction isongeweza kuwa complete kutokana na joto kuwa dogo mno. Labda hapo ulimaanisha MgO. Just thinking as a chemist sio biologist.
 
Mkuu unapozungumzia acid unamaanisha vitu kama Hydrocloric acid, nitric acid, sulphuric acid, phosphoric acid, acetic acid, latic acid, ascorbic acid nk nk. Sasa hapa ulivyosema vyakula vilivyolala vinakuwa na acid, je hiyo acid inatoka wapi ambapo awali haikuwepo?? Kuna any reaction mechanism inayoleta acid chakula kikilala?
Kweli! Hapo bado panahitaji ufafanuzi zaidi.
 
Kiungulia (kwa Kiingereza heartburn)

Ni hali ya kusikia maumivu makali katika koo la chakula. Maumivu hayo yana tokana na kupanda
kwa asidi iliyomo tumboni (asidi haidrokloriki = HCl) inayofanya kazi ya
kuua vijidudu vina vyoingia tumboni kwa njia ya chakula na maji. Mara nyingi kiungulia kikatokea baada ya tumbo kujaa gesi. Kiungulia kinaweza kuwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na

*Kula kwa pupa au kupita kiasi,

*Matumizi ya dawa za kulevya,

*Ujauzito,

*Tumbo kujaa gesi,

*Vidonda vya tumbo n.k.

Namna ya kuzuia kiungulia Kiungulia kinaweza kuzuiwa kwa namna mbali mbali.

Zifuatazo ni baadhi
ya njia za kuzuia kiungulia:

-Epuka kulala mara tu badaa ya kula chakula.

-Epuka kula kupita kiasi.

-Epuka kula vitu kama maharagwe, mboga za sukuma n.k.

-Epuka vinywaji vyenye asidi kwa wingi, mfano: soda n.k.

-Epuka matumizi ya dawa za kulevya. Tumia mto pindi ulalapo
 
Kiungulia (kwa Kiingereza heartburn)

Ni hali ya kusikia maumivu makali katika koo la chakula. Maumivu hayo yana tokana na kupanda
kwa asidi iliyomo tumboni (asidi haidrokloriki = HCl) inayofanya kazi ya
kuua vijidudu vina vyoingia tumboni kwa njia ya chakula na maji. Mara nyingi kiungulia kikatokea baada ya tumbo kujaa gesi. Kiungulia kinaweza kuwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na.....
Hoja ni kwa nini kiporo kinasababisha kiungulia? Zingatia mada.
 
Youngblood mjibu Ontario tunenepeshe bongo zetu. Hii ndiyo mijadala yenye shine na sio siasa muda wote. Anxious to hear from both of you Young blood and Ontario.
 
Mkuu unapozungumzia acid unamaanisha vitu kama Hydrocloric acid, nitric acid, sulphuric acid, phosphoric acid, acetic acid, latic acid, ascorbic acid nk nk. Sasa hapa ulivyosema vyakula vilivyolala vinakuwa na acid, je hiyo acid inatoka wapi ambapo awali haikuwepo?? Kuna any reaction mechanism inayoleta acid chakula kikilala?
Mkuu umenikumbusha mbali kuhusu magnesium kwenye kemia tuliambiwa nI metal sasa siku gas zilijaa matumboni kwenda hospital tukapewa vidonge vinaitwa magnesium tukaduwaa ila tulivipenda Ukawa kama mchezo kujifanya tunaumwa matumbo...
 
Youngblood mjibu Ontario tunenepeshe bongo zetu. Hii ndiyo mijadala yenye shine na sio siasa muda wote. Anxious to hear from both of you Young blood and Ontario.
Chakula kilicholala kinaweza kuingiliwa na acid forming bacteria hivyo kusababisha acidi iongezeke kwenye chakula.

Na swali lake la pili kuhusu magnesium,hiyo dawa nimesema imezoeleka kwa jina magnesium lakini kitaalamu inaitwa "Magnesium trisilicate" chemical formula yake ni ni kama ifuatavyo.
(Mg2O8Si3)

2.Kati ya tumbo na koromelo kuna valve(sphincter) hiyo inaweza kulegea na kuruhusu acid ipande juu kwenye koo na kusababisha kiungulia hutokea lakini mtu akipata magnesium trisilicate husaidia hiyo valve ikaze vizuri ili acid isipite hapo.
 
Jamani sisi tunataka suluhisho la kutuondelea kiungulia katiak kiporo, ninyi mnaonesha utaalam wa kubalance equations. Kama hamjui suluhisho si mnyamaze tu. Mimi ni mdau pia wa uporo tupeni suluhisho sio mnatuletea mambo yenu hayo base
 
Kiungulia maana yake ni kwamba tumboni kuna acidi nyingi sana na sometimes hupelekea kurudi juu (reflux) ya koromelo(oesophagus) na kusababisha kiungulia...
Sasa nimekuelewa-Nina acid reflux inayonitesa kwa muda sasa,huwa nilikuwa najiuliza ni kwa nn kila nikila chakula huwa inapanda kwenye koo haraka sikupata jibu.Thanks
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom