Husninyo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 23,723
- 9,193
Hasira jamani usije ukapigana na key board bure
nitamvunja mtu nywele. Tena sijui nianze na wewe..
Hasira jamani usije ukapigana na key board bure
Inatokea kwamba sisi wanaume ndio tunasababisha mengi ila ni wepesi sana kukimbia majukumu maana lolote litakaloharibika ndani ya nyumba lawama zinakuwa kwa wake zetu hata kama sisi ndi wasababishi
Kweli jamani, lawama zimezidi kwa wanawake.
Ndoa hadi kuvunjika unakuta mwanamke kashavumilia mengi ila bado wanatulaumu.
Waone vile!!
tatizo ni pale wanapoanza kutoa mambo nje ndo wanakutana na ushauri usiofaa .... hasa yey anapoanza kukuelezea ni lazima aonyeshe kwamba wewe ni tatizo
napinga hiyo tetesi ya wanaume. Inastahili kuwa hivi "Mwanamume mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono na miguu yake miwili". Maana ya kuwa kichwa katika familia ni nini? Yangu haitavunjika ng'o hata kama mwanamke ni kama kinanda najua jinsi ya kumpunguza volume, hata awe moto ntazima kwa CO2 na sio maji. Wanaume tuwe na busara, mwanmke kiumbe kidogo sana, mpeleke taratibu atafika na sio kukanyagia accelerator hadi mwishoJamani wana MMU kuna ndoa zomevunjika nimezishuhudia zaidi ya 3 na zote ukizisikiliza kesi zao nimwanaume kutokuwa mwaminifu yaani kuwa na nyumba ndogo au kutoka na wanawake tofauti tofauti nje ya ndoa lakini cha kushangaza jamii inawahukumu hao wanawake walioachwa kuwa wameshindwa kuipalilia ndoa mara wawaambie mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe. sasa mimi huwa najiuliza WHY??? mwanamke tu jamani??
na ndio inastahilimi nadhani siku hizi imebadilika wanaume ndo wanalaumiwa instead
mwanamke huwa ndo nguzo ya nyumba na ndo huleta maelewano au kuharibu ... lawama zinakuwa kwa vile kashindwa kuitunza nyumba yake
hata sisi wanaume tunalifahamu hilo ila ujeuri tu. Mungu turehemu sisi wanaume, hawa wanawake wametuvumili vya kutosha.Kumbe na wewe umeshaligundua hilo mamaa.
andaeni migomo ( sex strike). hii mifumo dume itokomee mbaliso ni mkeo ambaye anaenda kukutongozea wanawake wengne nje?
achen justfcation zenu zisizovaa ndala....ukadig nje et lawama umpe mkeo?
ni km vile uamue kukojoa seblen afu useme ni uyu mwanamke kanifanya nikojoe apa cz kashindwa kunishtua kwenda chooon....try to admit MNAPOKosea ahh inakera...yaan kafanya yeye then lawama kwako
Ndoa isipoanza na misingi ya kumjua Mungu huleta shida na matokeo yake ni kuvunjika au kuwa na kesi zisizoisha katika ndoa hiyo.Wanandoa pekee wanaweza kuokoa ndoa yao au kuifanya isiwe na amani.Kukosa uaminifu kwa wanandoa nitatizo kubwa sana katka dunia ya sasa iliyojaa matamanio ya kila aina .Kujenga ndoa juu ya misingi ya dini huepusha matatizo mengi kwenye ndoa.Kwa wakristo lazima watambue mke na mme wanapooana wanaambatana na kuwa mwili mmoja.Kwahiyo lazima watambue wameanza maisha mapya ya kuacha wazazi wao,lazima waambatane pamoja(kuacha kutamani nje ya ndoa) na lazima wawe na umoja.Ndoa yenye umoja hustawai na haiwezi kuvunjwa na upepo wa dunia hii.ndoa iliyojengwa katika misingi ya Mungu wanandoa watatumia maneno ya upole ,watafanyakazi kwa kushirikiana na kila ,wanachopata wataweka wazi na kupaga namna ya kukitumia,wanakuwa na makusudi mema,watapendana kama nafsi zao,watasameheana .Haya yote ni matunda ya roho ya upendo kwa ndoa .Mungu aziponye ndoa zote zenye shida ya kutoelewanaJamani wana MMU kuna ndoa zomevunjika nimezishuhudia zaidi ya 3 na zote ukizisikiliza kesi zao nimwanaume kutokuwa mwaminifu yaani kuwa na nyumba ndogo au kutoka na wanawake tofauti tofauti nje ya ndoa lakini cha kushangaza jamii inawahukumu hao wanawake walioachwa kuwa wameshindwa kuipalilia ndoa mara wawaambie mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe. sasa mimi huwa najiuliza WHY??? mwanamke tu jamani??
kwani wewe ni suspect No. 4. Mtoa mada ameeleza vizuri sana kuwa the real issue ya hizo case 3 ni infidelity lakini badala ya jamii kuona hilo inawalaumu wanawake. jamii inakuwa impartial, partisan kumfavour mwanume.Mimi nashangazwa na mijadala ya namna hii kwani haiko ballanced! Mtu ametoa case tatu ambazo yeye anaamini kuwa wanawake wanalaumiwa kwa kuvunja ndoa, halafu anatoa mjumuisho kuwa kila ivunjikapo ndoa basi mwanamke hulaumiwa!!! Hii mie sijaiona. Ndoa inapovunjika, wale wanaojua kilichosababisha ndoa kuvunjika hukisema, na ikiwa mhusika ni mwanamke jamii husema!!
mtoa mada hajasweep into conclusion ila ameeleza alichosikia na judgement ya jamii sasa anauliza iweje basi mwanamke ndo anatupiwa lawama zote. mkuu kwani wewe unaishi dunia ipi huelewi mambo haya. hujawahi kusikia mtu amehukumiwa miaka 30 kwa kosa ambalo halijui bali kapewa?Hizi "sweeeping conclusion" za kuwa mwanamke anaonewa au mfumo dume ndo tatizo lenyewe. Hivi wanawake kwenye ndoa ni malaika na hawasababishi ndoa kuvunjika?? Wenye ndoa wanajua. Hata jamii inaposema aliyesababisha ndoa kuvunjika ni mke, tujiridhishe kwa kufanya utafiti si kwa kupinga tu na kulaumu mfumo dume!!
duh! hii mada yaonekana imekuchoma sana ila sijui kwa nini. kuwasupport wanawake haimaanishi ana feminist ideology. samahani kama amekukwazaHizo case 3 unazotolea mfano inaonekana hauna details za kutosha ila tu umeamua kuwa "FEMINIST" wa kutetea mwanamke kwa kila jamba bila kuangalia uhalisia!! Jamii huwa ina jinsi yake ya kuchambua mambo, hata tukitaka kulazimisha misimamo yetu tutaendelea kuonekana watu wa ajabu!
na mwanamume pia sio malaika. tukubali pia makosa na tuwe tayari kuomba msamaha. tatizo letu wanaume ni kujifanya Miungu midogo, iwapo tutabadilisha hii dhana sidhani kuna ndo inaweza vunjikaWanawake si malaika ndani ya ndoa, na ni kweli kuwa wapo wanaovunja ndoa zao kwa makosa yao! Jamii inapofanya conclusion, imeona kilichotokea! Pale ambapo wenye kosa ni wanaume, jamii husema vile vile!! Tusigeuze jukwaa hili feminism movement, tuongee vitu kwa haki na kuangalia uhalisia wa kila tukio kwa mapana yake!
mwanamke huwa ndo nguzo ya nyumba na ndo huleta maelewano au kuharibu ... lawama zinakuwa kwa vile kashindwa kuitunza nyumba yake