Kwanini kila ndoa inayovunjika lawama anatupiwa mwanamke!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini kila ndoa inayovunjika lawama anatupiwa mwanamke!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Karina, Sep 22, 2011.

 1. Karina

  Karina Member

  #1
  Sep 22, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana MMU kuna ndoa zomevunjika nimezishuhudia zaidi ya 3 na zote ukizisikiliza kesi zao nimwanaume kutokuwa mwaminifu yaani kuwa na nyumba ndogo au kutoka na wanawake tofauti tofauti nje ya ndoa lakini cha kushangaza jamii inawahukumu hao wanawake walioachwa kuwa wameshindwa kuipalilia ndoa mara wawaambie mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe. sasa mimi huwa najiuliza WHY??? mwanamke tu jamani??
   
 2. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mwanamke huwa ndo nguzo ya nyumba na ndo huleta maelewano au kuharibu ... lawama zinakuwa kwa vile kashindwa kuitunza nyumba yake
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  sababu mwanamke ndiye anayeolewa kwa kutolewa mali,hivyo ana jukumu la kuilinda,..sema jingine
   
 4. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mfume dume Karina,malezi yetu yanamtaka mama azae na alee watoto,hivyo ikitokea kutokuelewana jamii inatarajia wazazi (hasa mama) kuweka maslahi ya watoto kwanza above everything including her personal happiness,health and welfare. Too sad Karina lakini hayo ndo mazingira tuliyokulia.
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kila watoto wanapolala nja lawama kwa mwanaume
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mfumo dume tuliourithi na unaendelea kututafuna
  Angalia hata maandiko yanasema wazi kabisa "mwanamke mwerevu huijenga nyumba kw amikono yake ila mwanamke mpumbavu huibomoa kwa mikono yake" hapo haimtaji mwanaume japo mwanaume hapo anaweza kuwa ndiye mkosaji
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  100% umefinalize mjadala
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sina cha kuongeza
   
 9. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  bad hapo majukumu ya kuitunza ndoa na nyumba yako kwa mwanamke maana wanaume kukiwa na tatizo hupenda kuzikimbia nyumba au kukimbia tatizo ... na furaha ya nyumba ni mwanamke
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kweli jamani, lawama zimezidi kwa wanawake.
  Ndoa hadi kuvunjika unakuta mwanamke kashavumilia mengi ila bado wanatulaumu.
  Waone vile!!
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  Mfumo dume
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Inatokea kwamba sisi wanaume ndio tunasababisha mengi ila ni wepesi sana kukimbia majukumu maana lolote litakaloharibika ndani ya nyumba lawama zinakuwa kwa wake zetu hata kama sisi ndi wasababishi
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hasira jamani usije ukapigana na key board bure
   
 14. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  lakini sisi wanaume tunaweza kuwa ni tatizo , au wanawake ni tatizo au wote ni matatizo ... ila zigo la lawama linamwendea mwanamke kwa vile ndo mlezi
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwa asilimia kubwa sisi wanaume tuna matatizo tena ndo waanzilishi wa mengi ndani ya familia ila ni wepesi sana kukwepa lawama
  na vile vile ni wagumu sana kukiri madhaifu yetu na kukubali kukaa chini na kuyajadili kwenye ngazi ya familia
  So wenzetu wanapovumilia wakichoka huwa wanaamua lolote na liwe au tunaporealize kuwa tuna makosa inakuwa too late wenzetu washachoka
   
 16. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  lakini kama ni mlezi hata mtoto akikosea huwezi kumchoka .. utatumia kila mbinu ila wengi wa wanawake hukumbilia kulaumu tu
   
 17. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakubali uvumilivu ni muhimu sana kwenye masuala ya ndoa
  Ila kuna mengine kwa kweli hayavumiliki
  kuna sehem nao hawa wenzetu wanafika wanasema enough is enough wacha litokee la kutokea aondoke maana inakuwa sasa mambo anayofanyiwa yamezidi kipimo
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  tatizo ni pale wanapoanza kutoa mambo nje ndo wanakutana na ushauri usiofaa .... hasa yey anapoanza kukuelezea ni lazima aonyeshe kwamba wewe ni tatizo
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu ushawahi kukutana na situation unapofikia pooint of no return yaani kama ni ushauri ushatoa mpaka basi na kama ni kuyaongea mmeshayaongea sana ikiwamo na vikao vya ndugu na wazazi na ijapofikia hapo mhusika anakuwa hana other option zaidi ya kuamua liwalo na liwe
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huo ndio mfumo DUME. kimsingi Ndoa ikivunjika wote (yaani Mume na Mke) mmechangia, lakini jamii ni mara nyingi inamhukumu mke kwa sababu kwa mujibu wa mafundisho ya mapokeo kutoka kizazi hadi kizazi, mke hutakiwa kumvumilia mume hata kama atakuwa na matatizo kiasi gani...................... Huo ndio ujinga wa ndoa.
   
Loading...