Chagua UKAWA, mwezi wa kumi ndipo utaelewa kwamba maendeleo yanaletwa na nini!
Nimekuwa najiuliza, iweje chochote kizuri inakuwa Rwanda ndio ya kwanza, mfano Gender equality Rwanda ndio ipo juu hata zaidi ya US, nchi yenye ajali za barabarani chache duniani mojawapo ni Rwanda, mji wenye usafi Afrika Kigali, nchi yenye mvuto wa uwekezaji ni Rwanda, nchi ya mwisho kwa rushwa East and Central Afrika ni Rwanda. Kuna mtu ameniambia kuwa sababu ni Rwanda ni nchi ndogo, lakini sio kweli kwani Burundi ni kubwa? Kwani Zanzibar ni kubwa? Kwa ujumla sithani kama kuna uhusiano kati ya udogo wa nchi na kuwa na mambo mazuri kwa karibu kila jambo. wadau labda ni kwanini mambo mazuri imekuwa Rwanda tu?