mkuu unajua mengi kuliko tarakimu unazoandika, tarakimu zinatumika kudanganya jamii, nimezungumzia idadi ya watu jumla, lakini nani ni mhanga wakuu wa vita?, kina mama, watoto, wazee, wazembe, na wenye mtazamo hasi na vuguvugu.
Rwanda watu waliobaki ni kundi la watenda kazi wengi, tegemezi wachache; walipo ni zaidi ya Japani wakipanga uzazi kwa miaka 100 kwani wao wanafungu dogo la wazee ukilinganisha na Japani.
Tanzania ina raia wengi wa miaka 0-21, i.e. umri tegemezi ukiachilia wazee.
Hivyo ukiangalia idadi tegemezi kwa kmita mraba kwetu itakuwa juu na wafanyakazi kwa kmita mraba kwao itakuwa juu.
Kwa mtazamo huo kama tutahusika na kazi ya nguvu kama kilimo, ardhi yao itatoa mara nyingi zaidi ya TZ.
Hivyo taarifa ya idadi ya watu kwa eneo hauwezi kutoa hitimisho kama utoalo kwa idadi ya watu (jumla).
Kwa wingi wa watu wa Rwanda bajeti yao inaweza kuendeshwa na sehemu ndogo ya bajeti ya TZ.