Kwanini kila kitu kizuri ni Rwanda tu?

Kwanini kila kitu kizuri ni Rwanda tu?

Makaura

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
892
Reaction score
295
Nimekuwa najiuliza, iweje chochote kizuri inakuwa Rwanda ndio ya kwanza, mfano Gender equality Rwanda ndio ipo juu hata zaidi ya US, nchi yenye ajali za barabarani chache duniani mojawapo ni Rwanda, mji wenye usafi Afrika Kigali, nchi yenye mvuto wa uwekezaji ni Rwanda, nchi ya mwisho kwa rushwa East and Central Afrika ni Rwanda. Kuna mtu ameniambia kuwa sababu ni Rwanda ni nchi ndogo, lakini sio kweli kwani Burundi ni kubwa? Kwani Zanzibar ni kubwa? Kwa ujumla sithani kama kuna uhusiano kati ya udogo wa nchi na kuwa na mambo mazuri kwa karibu kila jambo. wadau labda ni kwanini mambo mazuri imekuwa Rwanda tu?
 
rwanda ni nchi ndogo sana hivyo ni rahisi kui control hapo ndipo walipopatia hakuna muujiza hapo
 
Wamejipanga.
Na miundo mbinu walioweka, inafanya kazi.
Mkuu wao hacheki na kima.
 
RAIS MWENYE KUWAJIBIKA NA ASIYE NA MIZAHA udogo wa nchi sio kigezo cha eti ni rahisi kuikontrol vipo vinchi vidogo zaidi ya #rwanda na ni vya kipumbavu na hovyo kwelikweli/the way kagame leads the country matter.
 
Mana ake unataka kuniambia kuwa kuna uhusiano kati ya jambo zuri kama la kutokuwepo kwa rushwa na ukubwa wa nchi? Embu thibitsha usemi wako!
rwanda ni nchi ndogo sana hivyo ni rahisi kui control hapo ndipo walipopatia hakuna muujiza hapo
 
rwanda ni nchi ndogo sana hivyo ni rahisi kui control hapo ndipo walipopatia hakuna muujiza hapo

Mbona vijiji vyetu ni vidogo, vina Afisa mtendaji, Mwenyekiti wa kijiji, wenyeviti wa vitongoji lakini vina waganga wanaoelekeza albino auwawe?. Swala ni uongozi imara tu
 
afu kumbuka hawa jamaa walishachapana wenyewe kwe wenyewe so saiz heshima mbele mambo ya kipuuzi hawataki tena...kazi kwa kwenda mbele...unaweza fanya huwezi kula kona...sio huku kila mtu anajidai anaweza kuwa rais!!?
 
RAIS MWENYE KUWAJIBIKA NA ASIYE NA MIZAHA udogo wa nchi sio kigezo cha eti ni rahisi kuikontrol vipo vinchi vidogo zaidi ya #rwanda na ni vya kipumbavu na hovyo kwelikweli/the way kagame leads the country matter.

vipo vinchi vidogo halafu hujavitaja kama sio upofu ni nini ??
 
rwanda ni nchi ndogo sana hivyo ni rahisi kui control hapo ndipo walipopatia hakuna muujiza hapo

Point yako haijashiba! kwanini Taifa kubwa kama Marekani uchumi wao upo juu wakati lile ni taifa kubwa?
 
Mana ake unataka kuniambia kuwa kuna uhusiano kati ya jambo zuri kama la kutokuwepo kwa rushwa na ukubwa wa nchi? Embu thibitsha usemi wako!

rushwa ipo ila kwa kiwango kidogo
kama zanzibar
 
Mbona vijiji vyetu ni vidogo, vina Afisa mtendaji, Mwenyekiti wa kijiji, wenyeviti wa vitongoji lakini vina waganga wanaoelekeza albino auwawe?. Swala ni uongozi imara tu

hivi hivyo vijiji utaingia na visa ??
hapo mgeni unaingia unafanya mauaji unaondoka ndio kinachotokea
 
Hata mabinti wa Kinyarwanda ni wadhuri saaaana na mtoto wa Kagame.....

kgm.jpg
 
Point yako haijashiba! kwanini Taifa kubwa kama Marekani uchumi wao upo juu wakati lile ni taifa kubwa?

marekani wameanza kujitegemea lini kama taifa ??

Hivi unajua nchi karibu zote za ulaya ni kama mkoa tu hapa Tanzania ndio maana wameweza kuendelea haraka nchi kama ubeligiji ina watu milioni nane kama ingekua Tanzania watu milioni ningeweza kuwakumbuka hata robo tatu ya wakazi wa nchi nzima

asilimia kubwa ya nchi zenye eneo kubwa ni masikini hutaki unakuja na fact sio ubishani
 
hivi hivyo vijiji utaingia na visa ??
hapo mgeni unaingia unafanya mauaji unaondoka ndio kinachotokea

Ukiingia kwenye kijiji chenye uongozi imara ni lazima uripoti kwa mwenyeki na uwaeleze umekuja kufanya nini, hata zamani serikali za mitaa ilikuwa hivyo
 
Mimi nadhani ni pazuri kwa kuwa wanakwaya wao walikwisha imba ''Kwetu Pazuri''
 
marekani wameanza kujitegemea lini kama taifa ??

Hivi unajua nchi karibu zote za ulaya ni kama mkoa tu hapa Tanzania ndio maana wameweza kuendelea haraka nchi kama ubeligiji ina watu milioni nane kama ingekua Tanzania watu milioni ningeweza kuwakumbuka hata robo tatu ya wakazi wa nchi nzima

asilimia kubwa ya nchi zenye eneo kubwa ni masikini hutaki unakuja na fact sio ubishani

Mantic ya kusema nchi ndogo inakuwa na maendeleo ni wrong Idea, nchi kubwa unaweza kuifanya ndogo kwa kuweka tawala kuanzia kitongoji, kijiji, kata hadi mkoa. China ni nchi kubwa lakini imeendelea, Brazil nchi kubwa imeendelea, Russia nchi kubwa imeendelea. Kuwa na nchi kubwa ni fursa ya maendeleo

Zanzibar nchi ndogo, iko hoi.
Comoro nchi ndogo, iko hoi.
Mali nchi ndogo, iko hoi
Burundi ni chi ndogo, iko hoi
 
Back
Top Bottom