Kwanini Kikwete anawakwepa vijana na kukumbatia wazee?

Akikutana na vijana au wazee wa ukweli atawaeleza nini?mwacheni aendelee kujifariji na wazee njaa.
 
Thread hii imeakisi kwa kiasi kikubwa mtindio wako wa ubongo. Kwa akili yako wewe unadhani la msingi hapo ni forum aliyotumia kuhutubia au ujumbe alioutoa? Kwa taarifa yako cha msingi hapo ni ujumbe wake hata kama aliutoa akiwa jela na siyo kiti alichokalia wakati akitoa hotuba, au wale waliokuwa mbele yake wakati huo. Kwa wewe uliyezaliwa juzi huwezi kujua kwamba utamaduni huu ulianza toka enzi za baba wa taifa na hata vita ya Kagera aliitangaza akiwa na wazee wa Dar es Salaam akiwa Diamond Jubilee. Jinoe kidogo kabla hujakurupuka!
 
[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
Nimefuatilia Hotuba ya Ndg Mr. president Kikwete nimegundua kuwa yeye na washauri wake ikiwa pia na chama chake wemeshindwa kumshauri ni wapi aongelee mambo ta Kitaifa na ni kundi gani linaguswa na jambo husika.

Katiba hii tutakayopambana kufa au kupona ili iwe inayokidhi matakwa ya Watanzania ( VIJANA) na sio wazee wa CCM na tena wale wa Dar tu kama tulivyowaona wanasinzia wakati wa hutuba ya Mr.President.Yawezaka pia kuwa wazee hao wanafikili kuwa bado Tanzania ni CCM tu kwani walikuwa wanasikika wakiimba CCM kila Mr. President waliposema neno na kusahau kuwa CCM ITAKUFA kabisa baada ya uchaguzi 2015. Nionavyo mimi wale wazee wa Dar anaowatumia Mr. President kutokana na Umri wao miaka minne iliyobaki ya kikwete na hata kabla ya kupatikana kwa katiba mpya Umri wao kwa mjibu wa maandiko matakatifu hautawaruhusu kuwa na nguvu ya hata kutembea bila mikongoja ( sitaki niwatabilie uwepo wao duniani). kwa Ufupi katiba ijayo ni ya VIJANA na kamwe si wazee tena kama CCM wanavyojidanganya.

Hata hivyo Mr. President na serkali yake wanajua walivyolisahau kundi kubwa hili la vijana na kuendelea na kundi la wazee ambao wanajua muda wao ni mchache sana.

Vijana KUWENI macho na hili na msikubali kabisa na kwa wenye hakili za utambuzi wa mambo ya political Kipropaganda utagundua tu kuwa hizi ni mbinu zilizopitwa na wakati za kungangania wazee na kuwaacha VIJANA wakitaabika...

Hii inaitwa political Miscalculation na matokeo yake yataonekana ni swala la Muda tu Ndg Mr. President.
[/FONT]
Reyro,

Namna nzuri ya kuwa macho na vijana wenzako (kama unao wenzako) ni kujikusanya na kutafakari huo ujumbe wa Rais na kuanza kuufanyia kazi. Kinyume cha hayo utajipotezea muda wako kwa mambo ambayo huyawezi, na mwisho wake utakuwa si mwema.

Kama ni kijana na una Azma njema na nchi yako basi wakati ni huu na usikubali kuwachwa nyuma.
 
JK alichotakiwa kufanya ni kuongea na Watanzania wote na si "Wazee wa CCM wa Dar es Salaam!" Kisha baada ya kuongea na Watz wote aache nafasi ya maswali ili masuala mazito yanayotatiza ayajibu kama angeweza!
 
mwaka 2005 alivo kua anatafuta ridhaa ya watanzania
kuwa raisi,..alikua na falsafa ya "ujana",....kwamba yeye ni kijana na
anajali sana vijana.

Lakini ni mara mbili sasa amekua akikutana na wazee tu,...tena
wanaoitwa "wazee wa dar",...
Ndo kusema vijana hawana maana tena au mda
wa kuwajali vijana ni wakati wa kampeni peke yake?
 
nchi hii inajengwa na nani kwa asilimia nyingi, vijana tumesahauliwa kwa kiasi hiki, yeye ni wazee yani najiuliza ana maana gani kufanyua hivi?
1.hana uwezo wa kukabiliana na changamoto zao?
2.ni mwoga?
3.hana cha kusema make ameshindwa kuwatimizia ahadi zao alizowaahidi
4.anatuona hatuwezi na hatuna mchango wowote katika nchi>

ila ajue, ipo siku atatufikiria lakini muda utakuwa umekwisha!
 
Anajua sana vijana wana run Dunia,ila anaogopa challenge zetu maana anajua sisi sio vipofu a.k.a steve wonder,tumefunguka macho na tunaona ipasavyo
 
Kichekesho, Polisi wanadhani ndo wanashikilia amani, Pia polisi wanajifanya kilanja wa maamuzi wa wananchi, Tukijimwaga barabarani wanataona
 
dah..kweli kabisa mkuu....mara kwa mara utamsikia anazungumza na wazee, wazee ,wazee...vijana NO unasahau vijana ndio taifa la kesho hivyo ni vema azungumze nao pia. ili kuonyesha pia vijana mchango wao kimawazo unahitaji pia kuleta maendeleo
 
Ulitaka ushirikishwe kwenye lipi zaidi ya kutumiwa na cdm?
OTIS
 
Ulitaka ushirikishwe kwenye lipi zaidi ya kutumiwa na cdm?
OTIS

we dada mbona uko hivyo? Changia mada kwanini Amiri JESHI mkubwa anawagwaya vijana. Usilete hoja mmavi mmavi hapa!
 
Imekuwa ni kawaida yako pindi nchi inapoyumba kukimbilia kuwahutubia wazee hususani wa dar es salaam, na unaamini ama kuona kuwa ni sahihi
Wakati huo huo unapohutubia wazee huzungumzia mambo ambayo kuna uwezekano mkubwa hao wazee hawayaelewi ama ni mageni kwao, na hapa hupendelea kutumia mawasiliano ya njia moja kumaanisha wewe ndo huwa mzungumzaji tuu, huwa hutoi nafasi ya maswali wala ushauri
Kumbuka Chief, hii nchi si ya wazee peke yao na wala hao wazee si kanakwamba ndo wazalishaji mali.
Iga viongozi wakubwa wa dunia ambao huwahutubia vijana katika maeneo mbalimbali kama vyuoni, kwenye ma hall nk.
Acha kututenga vijana, pia acha woga njoo tukabili na ukubali maswali toka kwetu.

NB
pole kwa yanayotokea, nilikuasa lakini, hiyo kesho hotuba yako itakupa majibu ya aina mbili, kuona madokta wakirudi makazini kama utakubali kuwawajibisha wateule wako nkya na mponda, ama kushuhudia maiti na harufu kali, toka hapo Muhimbili na Ocean rd
Mungu alivyowaajabu atakupa pigo hata wewe kwenye familia yako na hapo ndipo utakapojua uchungu tulio nao, Sikulaani bali nakutabiria
 
Anazungumza na wazee kufikisha ujumbe kwa wengine wote waliobakia. Huu ni utamaduni uliokuwepo toka enzi za kabla ya Nyerere, Nyerere akauendeleza, Mwinyi akauendeleza, Mkapa akauendeleza na sasa Kikwete anauendeleza.
 
Back
Top Bottom