Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 236
JK alionekana ni tumaini kubwa kwa vijana wan chi hii wakati anajitayarisha kuingia madarakani. Mapema mwezi May 2005 aliporudi Dar kutoka Dodoma baada ya CCM kumteuwa kugombea urais msafara wake wa kutoka Dar Airport kuja mjini ulikuwa na umati mkubwa wengi wao wakiwa vijana.
Wengine walilala barabarani kwa furaha na matumaini na wengine hata kudandia gari lake wakipiga kelele ‘Ajira!" Wazee hawakuonekana kabisa kufanya hivyo.
Na vivyo hivyo ilivyokuwa mikoani alipokwenda kujitambulisha, na pia wakati wa kampeni za 2005.
Leo hii JK anawakwepa vijana, anaona ni bora awakumbatie wazee. Na leo haikuwa mara ya kwanza kukutana na wazee, maana akiwa miongoni mwao anajisikia anafuraha kwani wazee hawana madai ya msingi kwake ukilinganisha na vijana.
Pia anajua akiwa miongoni mwa wazee ambao wengi wao ni wa CCM, watampigia makofi, vigelegele kwa lolote atakalolisema. Narudia, kwa lolote atakalolisema – na leo tumeona!
Vijana ambao ndiyo twaambiwa ni taifa la kesho na ndiyo wenye matatizo lukuki, JK anawaono si lolote si chochote. Hata hiyo katiba aliyozungumzia, itawahusu vijana zaidi.
Kwa nini JK sasa anawaogopa vijana na hali ndiyo walimpa kura nyingi kumwingiza madarakani.