Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,105
Nampongeza Mhe. Rais kwa kuona umuhimu wa kuunda sub committee za kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya haki jinai
Lakini nadhani kuna jambo ambalo Mhe. Rais alipaswa kuliona; kamati ina wazee wengi kuliko vijana: waliochakata na kuandaa taarifa naamini ni sekretarieti na ndiyo maana Mwenyekiti amewapongeza kwa kukaa zaidi ya siku tatu bila kulala.
Si afya kuwapa kazi hawa wazee akina Mhe. Jaji , Mzee Sefue, IGP na wengine kuumiza kichwa kuhusu utekelezaji wa ripoti hii. Napendekeza aboreshe kwa kufanya yafuatayo
1. Hawa wazee wabaki kupokea taarifa ya utekelezaji kila baada ya kipindi fulani
2. Ateue vijana wataalam kutoka kila sekta watakaohusika na kuichakata na kuja na actionable startegy pamoja na kuwekwa mpango wa utekelezaji.
Kufanya hivi kutawaondolewa pia hawa wazee lawama za kuonekana wameandika taarifa wasiyoweza kuitekeleza. Ukimwona Mhe. Jaji wakati anasoma unaona kazi uwezo wake wa akili upo sawa ila mwili umefika muda wa kukaa na kupumzika muda mrefu kuliko kufikiria tena changamoto ambazo hata yeye alipokuwa mkuu wa taasisi alishindwa kuzitatua.
Mzee Mwema na Mangu ukiwaambia leo wakasimamie mabadiliko ndani ya polisi lazima watakwama tu kwa sababu baadhi ya culture waliziweka wao. Leo wanaanzaje kumfundisha mwenzao namna ya kuongoza jeshi? Wataonekana kama wanamk9mand IGP aliyepo.
We need separate team ikiwa chini ya KM kiongozi ndiyo iunde sub committee Kwa lengo la kuleta ufanisi. Wazee wabaki kama washauri; kwanza wamejitahidi sana kwa umri wao kusimamia kazi hii