Kwanini kambi ya upinzani ilikuwa imenuna wakati bajeti inasomwa bungeni?

Yaani hii nchi ina majuha kweli.Unashangilia bajeti isiyoendana na unacho kusanya.Deni la taifa linazidi kukua ila bajeti haionyeshi ni mkakati upi waliona kupunguza madeni.Hiyo misamaha unayoshingili mingi hamgusi mwananchi wakaida moja kwa moja ila mafuta yanayogusa watu moja kwa moja wamekaba wewe kwako sio tatizo.
Hakuna niliposema wapinzani washangalie bajeti yote bali nimesema wange appreciate angalau hata yale waliyopendekeza na kukubaliwa na serikali kama walivyokuwa wanapiga makofi wakati Mbunge Peter Msigwa alipokuwa anatoa ushauri kwa serikali kuhusu masuala hayo.
 
Yaan sijui walikuwa wakishangilia nn mfano kufutwa linsen na kupandisha mafuta kama petrol na disel hapo nan ataumia kiufupi bangi ziliwafanya washangilie
 
Kuna uhusiano gani baina ya upigaji makofi na kutekelezeka kwa bajeti? Miaka yote ya bajeti hata bajeti iliyopita 2016/2017 waliipigia makofi kwa mbwembwe na kuisifu sana mwisho ilitekelezeka kwa 34%!! Makofi ni kelele tu hayasaidii bajeti kutekelezeka.....
 
Wapinzani watakuwa wameyaaona makosa kwenye budget na hawataki kuwa wanafiki wa kushangilia kitu ambacho watakuja kukilalamikia baadaye.
 
Kwa hiyo wanafanya nini bungeni, maana wamekaa kama sanamu tu
 
Kama bajeti iliyopita upinzani ndo waliotoa hoja za msingi ambazo CCM leo wanashangilia. Huoni kuwa wakinuna wanajua zaidi tutakavyo potea maana kutokana na mifano yako Upinzani ndo unamawazo best, badala ya kutaka washangilie waombeni wawaambie mnapokosea
 
Bongo upinzani utabaki upinzani tu. Wabunge wa kambi ya upinzani hawataki kabisa kuonesha wanafurahishwa na utendaji wa serikali hata chembe kidogo. Kwa tanzania kambi ya upinzani na kambi ya chama tawala ni kama paka na panya. ikitokea kambi ya chama tawala au serikali kwa ujumla inafanya vizuri na wananchi wanakubali kinachofanyika wapinzani wao kama sio kutafuta vijisababu chokonozi ii kutibua mchakato thabiti basi wataamua kukaa kimya tu, kama sio kutoka nje ya ukumbi wa bunge. Kwao wanaamini upinzani ni kupinga kila kitu kinachofanywa na chama tawala.
Kwa kifupi wabunge wa kambi ya upinzani siku zote wanaiombea mabaya serikali. Wanadhani serikali ikiboronga ni ahueni kwao. La hasha. Kuboronga kwa serikali ni kadhia kubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Nchi ikishaenda mlama ni aibu kwa wanasiasa wote, wa chama tawala na upinzani. Mantiki yangu hapa ni kwamba kufeli kwa serikali ni kufeli kwa kambi ya upinzani, kwani kazi kubwa ya chama cha upinzani ni kukosoa serikali pale inapokosea, kutoa maoni ya kipi kilicho bora kifanyike na kupongeza pale panapostahili.
Kwa huu mtindo wa kambi ya upinzani kususia susia ni kudidimiza maendeleo ya nchi, kidemokrasia na kiuchumi. Mpinzani anaposusa na kuishia kulalamika kwa kila lifanyikalo pasipo kujenga hoja endelevu ni sawa na kuwa na upinzani usio na meno, kiasi cha kukifanya chama tawala kufanya kitakacho, eidha kwa kukomoa upinzani au kwa kuamini upinzani hauna hoja endelevu.
kambi ya upinzani ibadilike sasa -ikue kidemokrasia. Demokrasia ni kujenga hoja na kama malumbano yanatokea basi yawe marumbano ya hoja, sio malumbano ya hulka na kejeli.
Wafurahishwe na nini wakati bajeti iliyopita imetekelezwa 30% tu??

Hatupendi unafiki.
 
Bunge letu lina wabunge wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo.

Ikumbukwe kuwa CCM ina wabunge 276, CHADEMA ina wabunge 72, CUF 42, NCCR-Mageuzi 1 na ACT-Wazalendo 1.

Wakati hotuba ya bajeti inasomwa bungeni, mbunge wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alikuwa nje ya nchi.

Kilichonishangaza zaidi, wabunge wa upinzani hawakupiga hata makofi(meza) wakati Maboresho ya Mfumo wa Kodi, Ada na Tozo Mbalimbali zilipokuwa zinasomwa.

Ikumbukwe kuwa maboresho hayo yametokana kwa kiasi kikubwa na hoja za hao hao wapinzani ambao walizitoa mwaka jana na pia mwaka huu katika hotuba na mijadala kwa Wizara ya fedha na mipango.

Kwa mfano, mwaka jana wapinzani walipiga kelele sana kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo nje ya nchi (ancillary transport services). Katiba bajeti hii, kodi hiyo imeondolewa.

Kodi nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana na wapinzani ni kodi ya Mwaka ya Leseni ya Magari (Annual Motor Vehicle Licence Fee) iliyokuwa inalipwa hata kwa magari ambayo hayatumiki. Kwa sasa kodi hiyo imefutwa na badala yake hiyo itatozwa kwa magari yanayotembea tu na italipwa mara moja tu pale gari linaposajiliwa. Mbunge Msigwa wakati akitoa mapendekezo haya ya kuitaka serikali ihamishie kwenye mafuta alishangiliwa sana na kambi ya upinzani.

Sehemu nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana ni serikali kutokufahamu vizuri kiasi gani cha madini kinasafiriswa nje ya nchi. Kwa sasa serikali imeamua kutoruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi. Aidha, Serikali itaanzisha maeneo maalum (clearing houses) katika viwanja vya kimataifa, migodini, na kadhalika ambapo madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali cha kusafirisha madini hayo ambacho kitatozwa ada ya asilimia moja (clearing fee) ya thamani ya madini hayo.

Kitu kingine kilichoanzishwa na serikali kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mtaji (capital goods) ili kupunguza gharama za ununuzi/uagizaji wa mashine na mitambo ya kuzalishia.

Serikali imeamua pia kupunguza kiwango cha kodi ya Mapato ya Makampuni (Corporate Income Tax) kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 10 kwa miaka mitano kuanzia mwaka mwekezaji atakapoanza uzalishaji, kwa waunganishaji (assemblers) wa magari, matrekta na boti za uvuvi.

Kutotozwa pia ushuru kwa mtu anayesafirisha mazao yake kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine yasiyozidi tani moja (1) na pia kupunguzwa kwa ushuru wa mazao (produce cess) kwa sasa yatatozwa asilimia 2

Haya yote wakati yanasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, wabunge wa kambi ya upinzani walikuwa wamenuna huku nyuso zao zikionekana kusononeka.

Mimi kama mwananchi wa kawaida nikajiuliza, hawa wabunge wa upinzani hawakuona hata jema moja katika hii bajeti hasa ikichukuliwa kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wanayapigia kelele yamefanyiwa kazi?

Kwa nini wanaonekana kusononeka wakati hata baadhi ya madai yao yamekubaliwa?

Kwa vielelezo msikilize kwenye video Mbunge Peter Msigwa alivyosema na kushangiliwa na wabunge wa upinzani kuhusu kodi ya mwaka ya leseni ya magari.

Kwa wenye bando dogo anzia kuangalia video dakika ya 8:30.

VIDEO:

Sidhani Kama walikuwa wamenuna. Walikua wanasikiliza kwa umakini Zaidi. Hata darasani mtoto anayesikiliza kwa umakini uelewa wake utakua tofaut na yule anayepiga madawati wakati mwl anafundisha.
 
Bajeti ya kuuma na kupuliza hiyo kwa mtanzania

Imehamisha maumivu kutoka point A kuyapeleka point B.

Kwa kuweka kodi kwenye mafuta itaongeza gharama za usafirishaji na hatimaye gharama za bidhaa zitapandaa tu.
 
Bunge letu lina wabunge wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo.

Ikumbukwe kuwa CCM ina wabunge 276, CHADEMA ina wabunge 72, CUF 42, NCCR-Mageuzi 1 na ACT-Wazalendo 1.

Wakati hotuba ya bajeti inasomwa bungeni, mbunge wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alikuwa nje ya nchi.

Kilichonishangaza zaidi, wabunge wa upinzani hawakupiga hata makofi(meza) wakati Maboresho ya Mfumo wa Kodi, Ada na Tozo Mbalimbali zilipokuwa zinasomwa.

Ikumbukwe kuwa maboresho hayo yametokana kwa kiasi kikubwa na hoja za hao hao wapinzani ambao walizitoa mwaka jana na pia mwaka huu katika hotuba na mijadala kwa Wizara ya fedha na mipango.

Kwa mfano, mwaka jana wapinzani walipiga kelele sana kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo nje ya nchi (ancillary transport services). Katiba bajeti hii, kodi hiyo imeondolewa.

Kodi nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana na wapinzani ni kodi ya Mwaka ya Leseni ya Magari (Annual Motor Vehicle Licence Fee) iliyokuwa inalipwa hata kwa magari ambayo hayatumiki. Kwa sasa kodi hiyo imefutwa na badala yake hiyo itatozwa kwa magari yanayotembea tu na italipwa mara moja tu pale gari linaposajiliwa. Mbunge Msigwa wakati akitoa mapendekezo haya ya kuitaka serikali ihamishie kwenye mafuta alishangiliwa sana na kambi ya upinzani.

Sehemu nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana ni serikali kutokufahamu vizuri kiasi gani cha madini kinasafiriswa nje ya nchi. Kwa sasa serikali imeamua kutoruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi. Aidha, Serikali itaanzisha maeneo maalum (clearing houses) katika viwanja vya kimataifa, migodini, na kadhalika ambapo madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali cha kusafirisha madini hayo ambacho kitatozwa ada ya asilimia moja (clearing fee) ya thamani ya madini hayo.

Kitu kingine kilichoanzishwa na serikali kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mtaji (capital goods) ili kupunguza gharama za ununuzi/uagizaji wa mashine na mitambo ya kuzalishia.

Serikali imeamua pia kupunguza kiwango cha kodi ya Mapato ya Makampuni (Corporate Income Tax) kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 10 kwa miaka mitano kuanzia mwaka mwekezaji atakapoanza uzalishaji, kwa waunganishaji (assemblers) wa magari, matrekta na boti za uvuvi.

Kutotozwa pia ushuru kwa mtu anayesafirisha mazao yake kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine yasiyozidi tani moja (1) na pia kupunguzwa kwa ushuru wa mazao (produce cess) kwa sasa yatatozwa asilimia 2

Haya yote wakati yanasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, wabunge wa kambi ya upinzani walikuwa wamenuna huku nyuso zao zikionekana kusononeka.

Mimi kama mwananchi wa kawaida nikajiuliza, hawa wabunge wa upinzani hawakuona hata jema moja katika hii bajeti hasa ikichukuliwa kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wanayapigia kelele yamefanyiwa kazi?

Kwa nini wanaonekana kusononeka wakati hata baadhi ya madai yao yamekubaliwa?

Kwa vielelezo msikilize kwenye video Mbunge Peter Msigwa alivyosema na kushangiliwa na wabunge wa upinzani kuhusu kodi ya mwaka ya leseni ya magari.

Kwa wenye bando dogo anzia kuangalia video dakika ya 8:30.

VIDEO:

Kuna mambo yanafikirisha sana! Hivi tunahitaji kuona wabunge wakishangilia bajeti inaposomwa au wanakuwa makini kuijadili bajeti yenyewe? Yaani wabunge wamshangilie waziri anayeleta mapendekezo kwao badala ya kutafakari kwa makini kile kinachowasilishwa kama mapendekezo na kujiweka tayari kuyajadili? Kwenye Bajeti jema haliko kwenye kusomwa, jema liko kwenye mjadala!
 
Bunge letu lina wabunge wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo.

Ikumbukwe kuwa CCM ina wabunge 276, CHADEMA ina wabunge 72, CUF 42, NCCR-Mageuzi 1 na ACT-Wazalendo 1.

Wakati hotuba ya bajeti inasomwa bungeni, mbunge wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alikuwa nje ya nchi.

Kilichonishangaza zaidi, wabunge wa upinzani hawakupiga hata makofi(meza) wakati Maboresho ya Mfumo wa Kodi, Ada na Tozo Mbalimbali zilipokuwa zinasomwa.

Ikumbukwe kuwa maboresho hayo yametokana kwa kiasi kikubwa na hoja za hao hao wapinzani ambao walizitoa mwaka jana na pia mwaka huu katika hotuba na mijadala kwa Wizara ya fedha na mipango.

Kwa mfano, mwaka jana wapinzani walipiga kelele sana kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo nje ya nchi (ancillary transport services). Katiba bajeti hii, kodi hiyo imeondolewa.

Kodi nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana na wapinzani ni kodi ya Mwaka ya Leseni ya Magari (Annual Motor Vehicle Licence Fee) iliyokuwa inalipwa hata kwa magari ambayo hayatumiki. Kwa sasa kodi hiyo imefutwa na badala yake hiyo itatozwa kwa magari yanayotembea tu na italipwa mara moja tu pale gari linaposajiliwa. Mbunge Msigwa wakati akitoa mapendekezo haya ya kuitaka serikali ihamishie kwenye mafuta alishangiliwa sana na kambi ya upinzani.

Sehemu nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana ni serikali kutokufahamu vizuri kiasi gani cha madini kinasafiriswa nje ya nchi. Kwa sasa serikali imeamua kutoruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi. Aidha, Serikali itaanzisha maeneo maalum (clearing houses) katika viwanja vya kimataifa, migodini, na kadhalika ambapo madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali cha kusafirisha madini hayo ambacho kitatozwa ada ya asilimia moja (clearing fee) ya thamani ya madini hayo.

Kitu kingine kilichoanzishwa na serikali kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mtaji (capital goods) ili kupunguza gharama za ununuzi/uagizaji wa mashine na mitambo ya kuzalishia.

Serikali imeamua pia kupunguza kiwango cha kodi ya Mapato ya Makampuni (Corporate Income Tax) kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 10 kwa miaka mitano kuanzia mwaka mwekezaji atakapoanza uzalishaji, kwa waunganishaji (assemblers) wa magari, matrekta na boti za uvuvi.

Kutotozwa pia ushuru kwa mtu anayesafirisha mazao yake kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine yasiyozidi tani moja (1) na pia kupunguzwa kwa ushuru wa mazao (produce cess) kwa sasa yatatozwa asilimia 2

Haya yote wakati yanasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, wabunge wa kambi ya upinzani walikuwa wamenuna huku nyuso zao zikionekana kusononeka.

Mimi kama mwananchi wa kawaida nikajiuliza, hawa wabunge wa upinzani hawakuona hata jema moja katika hii bajeti hasa ikichukuliwa kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wanayapigia kelele yamefanyiwa kazi?

Kwa nini wanaonekana kusononeka wakati hata baadhi ya madai yao yamekubaliwa?

Kwa vielelezo msikilize kwenye video Mbunge Peter Msigwa alivyosema na kushangiliwa na wabunge wa upinzani kuhusu kodi ya mwaka ya leseni ya magari.

Kwa wenye bando dogo anzia kuangalia video dakika ya 8:30.

VIDEO:

Nadhani walikuwa wasikiliza kwa makini ili waje na yao itakayokuwa bora zaidi. Huwezi kuboresha kama hujaielewa ya wenzio. Hao watu wako makini mkuu. Ngoja tusubiri ya waziri wao kivuli.
 
Ndugu yangu Msemaji Ukweli....maelezo yako ni mazuri saana na yanaendana kabisa na ule msemo wetu wa "Heri tisa kibindoni,kuliko kumi nenda urudi"
Karne ya leo ni sahihi huo msemo...?
Kambi ya upinzani kwa bahati mbaya saana wote ni active players hawana sub wala washangiliaji na wala hawafikii nusu ya wenzao.
Na ni kwa nini washangilie na bado hawajakamilisha malengo yao...???
Wangeshangilia zile hoja zao kupita nadhani wangepigwa na maneno ya kwenye kanga au nyimbo za taarabu.BORA KIMYA IWE SALAMA
 
Kama unafikiri utashi unapimwa kwa kupiga makofi na kushangilia kila kitu mimi nakupa pole sana., budget nzuri bila mipango mikakati mizuri ya utekelezaji ni kazi bure
 
Back
Top Bottom