MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Bunge letu lina wabunge wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo.
Ikumbukwe kuwa CCM ina wabunge 276, CHADEMA ina wabunge 72, CUF 42, NCCR-Mageuzi 1 na ACT-Wazalendo 1.
Wakati hotuba ya bajeti inasomwa bungeni, mbunge wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alikuwa nje ya nchi.
Kilichonishangaza zaidi, wabunge wa upinzani hawakupiga hata makofi(meza) wakati Maboresho ya Mfumo wa Kodi, Ada na Tozo Mbalimbali zilipokuwa zinasomwa.
Ikumbukwe kuwa maboresho hayo yametokana kwa kiasi kikubwa na hoja za hao hao wapinzani ambao walizitoa mwaka jana na pia mwaka huu katika hotuba na mijadala kwa Wizara ya fedha na mipango.
Kwa mfano, mwaka jana wapinzani walipiga kelele sana kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani katika huduma zinazotolewa kwenye usafirishaji wa bidhaa/mizigo nje ya nchi (ancillary transport services). Katiba bajeti hii, kodi hiyo imeondolewa.
Kodi nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana na wapinzani ni kodi ya Mwaka ya Leseni ya Magari (Annual Motor Vehicle Licence Fee) iliyokuwa inalipwa hata kwa magari ambayo hayatumiki. Kwa sasa kodi hiyo imefutwa na badala yake hiyo itatozwa kwa magari yanayotembea tu na italipwa mara moja tu pale gari linaposajiliwa. Mbunge Msigwa wakati akiungana na baadhi ya wabunge wa CCM kutoa mapendekezo haya ya kuitaka serikali ihamishie kwenye mafuta alishangiliwa sana na kambi ya upinzani.
Sehemu nyingine iliyokuwa inalalamikiwa sana ni serikali kutokufahamu vizuri kiasi gani cha madini kinasafiriswa nje ya nchi. Kwa sasa serikali imeamua kutoruhusu usafirishaji wa madini kutoka migodini na kupeleka moja kwa moja nje ya nchi. Aidha, Serikali itaanzisha maeneo maalum (clearing houses) katika viwanja vya kimataifa, migodini, na kadhalika ambapo madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali cha kusafirisha madini hayo ambacho kitatozwa ada ya asilimia moja (clearing fee) ya thamani ya madini hayo.
Kitu kingine kilichoanzishwa na serikali kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye bidhaa za mtaji (capital goods) ili kupunguza gharama za ununuzi/uagizaji wa mashine na mitambo ya kuzalishia.
Serikali imeamua pia kupunguza kiwango cha kodi ya Mapato ya Makampuni (Corporate Income Tax) kutoka asilimia 30 mpaka asilimia 10 kwa miaka mitano kuanzia mwaka mwekezaji atakapoanza uzalishaji, kwa waunganishaji (assemblers) wa magari, matrekta na boti za uvuvi.
Kutotozwa pia ushuru kwa mtu anayesafirisha mazao yake kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine yasiyozidi tani moja (1) na pia kupunguzwa kwa ushuru wa mazao (produce cess) kwa sasa yatatozwa asilimia 2
Haya yote wakati yanasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, wabunge wa kambi ya upinzani walikuwa wamenuna huku nyuso zao zikionekana kusononeka.
Mimi kama mwananchi wa kawaida nikajiuliza, hawa wabunge wa upinzani hawakuona hata jema moja katika hii bajeti hasa ikichukuliwa kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wanayapigia kelele yamefanyiwa kazi?
Kwa nini wanaonekana kusononeka wakati hata baadhi ya madai yao yamekubaliwa?
Kwa vielelezo msikilize kwenye video Mbunge Peter Msigwa alivyosema na kushangiliwa na wabunge wa upinzani kuhusu kodi ya mwaka ya leseni ya magari.
Kwa wenye bando dogo anzia kuangalia video dakika ya 8:30.
VIDEO: