Kwanini kada ya ualimu inapewa mshahara kidogo?

Kwanini kada ya ualimu inapewa mshahara kidogo?

Waalimu ndio kada inayopendelewa kuliko wengine ila hamjui tu. Mishahara yenu wala sio midogo ni sawa na watumishi wengine tu hakuna tofauti. Nyinyi mna ziada ya yafuatayo
1. Kazi zenu zinaisha saa nane na nusu na wengine wanakula kona kabla hata ya muda huo,
2. Mna likizo kama nne hivi kwa mwaka pale shule zinapofungwa mnakuwa na muda wa kutosha kufanya mambo yenu
3. Sawa hamna posho nyingi lakini kuna kusimamia mitihani, kusahihisha mitihani, kusimamia uchaguzi za serikali, mambo ya sensa na hizi zote mnalipwa

Tatizo lenu waalimu mnakopa sana, unakuta mtu yuko vikoba 3 vyote kakopa, kakopa bank, au hizi microfinance yaani ni shida. ukiwa unakopa lazima utaona mshahara mdogo sababu ya makato
Ukweli mchungu sana huu
 
Naomba niende Moja Kwa Moja kwenye maada hivi ni Kwa nini kada ya ualimu inapewa salary kiduchu kulinganisha na kada nyingine au kazi yao Haina direct impact kwenye jamiii? Naomba kuwasilisha
Wakiwa na maisha mazuri hasira za kuchapa watoto ovyo watazitoa wapi?
 
Kada zilizo chini ya tamisemi nying mshahara ni sawa Kwa ngazi zote kuanzia certificate had diploma had degree Kuna wengine ni za chini Zaid labda afya ndio kidogo Wana unafuu
Shangazi naomba hela, najua mshahara umeshatoka.
Seriously.
 
Hao wote wakiwa chini ya Serikali za mitaa wanaanzia TGSS E. Daraja moja mbele ya Walimu, mazingira, Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Jamii, Ushirika n.k
Nilishajibu mwanzo hapo mwalimu shahada ni tgts D na kama kada zingine ukiondoa nilizotaja n.k ...naona umerudi na Jibu lilelile Sasa sijui ilikuwa haujaelewa au umejazia hoja nyama.
 
Naomba niende Moja Kwa Moja kwenye maada hivi ni Kwa nini kada ya ualimu inapewa salary kiduchu kulinganisha na kada nyingine au kazi yao Haina direct impact kwenye jamiii? Naomba kuwasilisha
Mwalimu hazalishi chochote aliwai kunukuliwa kada mmoja mashuhuri wa CCM Taifa.
 
Huyo teller ana fursa ya kukopa benki na akarudisha bila riba ..mwalimu vipi akope chaki!?? Unajua fursa wanazozipata hao watu wa benki!??
nyingi sana, tena asiwaringanishe na waalimu, wana mshahara wa kawaida hata mwalimu anawazidi, but wana fursa zinazowabeba sana, kama kuachiwa vitip tip kibao na customers, mdogo angu ni teller, anakwambia per day sometimes anaweza kuondoka hata na 500k tips tu, sasa jiulize anakusanya sh napi mwezi mzima? sababu pia ye ni teller wa kudeal na watu wazito
 
Back
Top Bottom