Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Nakubaliana na wewe.lakini why JWTZ?
Nchi hii haina njaa. Au hamjasikia jana kwenye vyombo vya habari kwamba mkoa wa Rukwa umewasilisha rasmi jana barua serikalini ukiomba uruhusiwe kuuza mazao yake nchi jirani?
waberoya - watu wengi hawaelewi - wanafikiri jeshi ni kuvaa magwanda na minyota mabegani
hawajui jeshi lazima liwe mfano kwenye nyanja za Uchumi, Ufundi, Mawasiliano, Elimu, Utabibu, Utafiti nk
Jeshi letu lipo lipo tu - eti wanangojea vita ije - isipokuja? hiyo bajeti ya bilioni zote hizo kwa mwaka inatoka kwa nani?
Majeshi yote duniani muda wa amani wanatumia kuweka nguvu katika masuala kama hayo na mengine ambayo waberoya kafafanua zaidi.
Mfano kama tunataka mapinduzi ya kilimo - kwa nini tusitumie jeshi letu liwe mfano? its true nchi za wenzetu majeshi yamekuwa yanatangulia then wananchi wanafuata nyuma - na ndiyo maana jeshi letu linaitwa JESHI LA WANANCHI.