Kwanini Juma Jabu aitwe House girl?

Kwanini Juma Jabu aitwe House girl?

Pengo

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2009
Posts
579
Reaction score
10
Wana jamii nimekutana na kisa cha kusikitisha mno wakati nilipokuwa namtembelea jamaa yangu anayeishi maeneo ya Tabata Kimanga.Jamaa yangu ana mtumishi wake wa ndani(House girl) ambaye ndiye mhimili wa kurekebisha mambo ya usafi na maakuli.Wakati natia mguu pale home jamaa akamwita yule housegirl wake "JJ hebu kamchukulie mgeni kinywaji katika kabati la mbeho".Nikamuuliza unamaanisha huyu binti anaitwa JJ?Jamaa akajibu kwa dhihaka kuwa JJ maana yake ni Juma Jabu beki mahiri wa Taifa Star,ikanishangaza sana lakini nikamuuliza tena unamaanisha huyu binti ana uhusiano wowote na huyo Juma Jabu?Jamaa yangu hakusita na kuniambia kuwa hapa bongo mtumishi wa ndani hususani wa kike anafananishwa na beki anayecheza nafasi ya kushoto yaani fullback left na ndio maana yeye amemfananisha na mlinzi mahiri wa Taifa Star Juma Jabu kutokana na utendaji wake wa kazi pale nyumbani.Nilibaki kinywa wazi nikitafakari kuwa hivi sasa itabidi mabeki wakimbie nafasi ya kushoto kwa kuhofia kufananishwa na watumishi wa ndani.Akina Amir Maftar,Njoroge,Samri Ayoub,Douglas Mhani,Yustas Bajwala,Alphonse Modest,Ahmed Amasha,Rashid Idd Chama,John Douglas na wengine wengi ambao hata humu jamvini huwa mnakamata beki tatu mpo hapo.
 
Haina maana kabisa....nawashauri waachane kuwadhalilisha hao wadada...na hata wachezaji wetu.....watafute majina mengine yenye kuleta maana....fedheha hatutaki kwenye jamii yetu....kama unataka kumpa jina kijanja...achana na mpango huo haufai....
 
hahaha huyo ni full back left au right, kuna wanaomwita beki 2 wengine beki 3 basi ni majina tuu, eti wengine wanasema sababu anafanya kazi zaidi ya mama mwenye nyumba na sometimes huziba pengo lake mama akiwa hayupo hahahahahahaha
 
Baba mwenye nyumba, ukishaanza kutoka na house girl kwisha habari yako!
 
huko ni kuwadhalilisha tu hao mabinti na naona haifai hata kidogo
 
Most correct heading: Kwanini House girl aitwe Juma Jabu (beki 3)?
 
Wana jamii nimekutana na kisa cha kusikitisha mno wakati nilipokuwa namtembelea jamaa yangu anayeishi maeneo ya Tabata Kimanga.Jamaa yangu ana mtumishi wake wa ndani(House girl) ambaye ndiye mhimili wa kurekebisha mambo ya usafi na maakuli.Wakati natia mguu pale home jamaa akamwita yule housegirl wake "JJ hebu kamchukulie mgeni kinywaji katika kabati la mbeho".Nikamuuliza unamaanisha huyu binti anaitwa JJ?Jamaa akajibu kwa dhihaka kuwa JJ maana yake ni Juma Jabu beki mahiri wa Taifa Star,ikanishangaza sana lakini nikamuuliza tena unamaanisha huyu binti ana uhusiano wowote na huyo Juma Jabu?Jamaa yangu hakusita na kuniambia kuwa hapa bongo mtumishi wa ndani hususani wa kike anafananishwa na beki anayecheza nafasi ya kushoto yaani fullback left na ndio maana yeye amemfananisha na mlinzi mahiri wa Taifa Star Juma Jabu kutokana na utendaji wake wa kazi pale nyumbani.Nilibaki kinywa wazi nikitafakari kuwa hivi sasa itabidi mabeki wakimbie nafasi ya kushoto kwa kuhofia kufananishwa na watumishi wa ndani.Akina Amir Maftar,Njoroge,Samri Ayoub,Douglas Mhani,Yustas Bajwala,Alphonse Modest,Ahmed Amasha,Rashid Idd Chama,John Douglas na wengine wengi ambao hata humu jamvini huwa mnakamata beki tatu mpo hapo.

Future ni ya ajabu sana hajui watoto wake watajaishia mikono ya nani amwombe Mungu msamaha kwa kukufuru. Pia nafikiri elimu yake ina mushkeri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom