Kwanini Julius Mtatiro alienda CUF?

Katika suala la kujenga hoja hapa natofautiana na wanajamvi,
Mtatiro anmaweza kujenga hoja panapohitaji hoja na anaweza kutumia nguvu ya watu pale inapohitajika na nirahisi wanaomfuata kuamini kuwa atakachoamua hata kama kinatumia nguvu ya umma kitaweza kuleta manufaa.
Kwangu mimi namheshimu sana mtatiro na namheshimu sana mnyika,
Tofauti nayoiona kati yao ni kuwa mnyika anaweza kujenga hoja tu, kuthubutu mambo ya kipiganaji ya level ya juu hawezi.
Mtatiro anajenga hoja na kuthubutu hata mambo ya hatari.

Binafsi kama nilivyowahi kusema awali katika moja ya mada nafikiria mtatiro hakufanya makosa makubwa kupambana na mnyika, nafahamu alijua namna mnyika alivyojijenga lakini katika kwa sababu alijua hakukuwa na dili ya vyama kuachiana majimbo aliingia ubungo na kutetea kura za chama chake hata kama chadema ilishinda lakini yy alionesha uwezo mkubwa wakujenga hoja na wapiga kura walimuelewa.
Lakini pia kupitia siasa za ubungo zilizompatia umaarufu zaidi nadhani alizidi kujijenga na kufahamika kwa wananchi wa kawaida ambao kabla walimfahamu kama kiongozi wa harakati za wanafunzi wa vyuo vikuu.

Kwa vyovyote vile mtatiro anabakia kuwa mwanasiasa kijana mahiri mwenye msimamo thabiti na asiyeyumbishwa na ndio maana alifanikiwa sana kwenye siasa za vyuo vikuu kama ambavyo anafanikiwa akiwa CUF.

Kwa mtizamo wangu hata kama angekuwa CHADEMA leo angebakia kuwa kiongozi wa kutumainiwa mno hata kama asingekuwa NAIBU KATIBU MKUU.

Give a credit to a person who deserves.
 
kwani anatoka kaskazini?

Ni kweli, Chadema intafuta watu wa kaskazini maana kaskazini chadema hatukubaliki sana- hasa Moshi ambako imeambulia wabunge 3 tu. Tunakubalika zaidi kanda ya ziwa mfano shinyanga na Mwanza tumepata wabunge 7 na jiji lote la Mwanza - si haba.
 
Tumtendee haki Mtatiro, ni mpiganaji na mtetezi wa wanyonge. Yupo tayari kupata matatizo ili wengine wapate kile anachoamini yeye Mtatiro kuwa wanastahili kupata.
Kwa mtazamo wangu, kwa jinsi CUF wanavyoendesha siasa zao Mtatiro hawezi kucomply, anaendelea kuwepo CUF kwakuwa hawezi kwenda CCM, na hawezi kwenda CDM kwakuwa lazima atakalia benchi tena sana na kwa jinsi Chadema ilivyojijenga kama taasisi sio rahisi aaminiwe na kupewa madaraka ili apate mkate wake wa kila siku. Vyama vingine vya upinzani vilivyobakia havina tofauti na kundi la Ze Komedi hawezi kwenda huko.
 
[QUOTE=ritz
Kwani imeandikwa wapi kuwa kila mtu lazima uwe CDM?
Uwezo wako wa kufikiri ni kama wa Ridhiwani JK, Kila wakati ni kuigopa CDM. Ungetamani ajiunge na Magamba?
 
Back
Top Bottom