Kwanini Julius Mtatiro alienda CUF?

Huyu dogo hapendi walipo watu waakili tulivu na aliona CUF yeye atakuwa pekee na kafanikiwa kuukwaa lakini sasa ndiyi hivyo ana pwaya kilakukicha na thamani yake inaisha.
 
Nafikiri aliupima vibaya upepo wa siasa,kwani wakati huu CUF ndiyo ilikuwa chama kikuu cha upinzani!!
 
Binafsi namuona jamaa hafit pale CDM kutokana na hulka yake ya kuropoka na kusema bila kufikiri, huwezi kufananisha na mnyika hata kidogo mnyika ni mtu wa kufakari jambn ndipo afanye comments
Mtatiro na Lema, nani bingwa wa kuropoka kama sio Lema
 
Uchaguzi mkuu 2010, bila mpango mkakati. He can make it 2015, let us wait & c!

Yeah -- he can make it in 2015. Aachane na chama cha maswahiba wa CCM na ajiunge na CDM akamtoe Idi azzan Kinondoni. In fact angefanya hivi last year saa hizi angekuwa Mjengoni anapambana na yule mama.
 
Mimi naitwa mohammed mtutuma, ni msaidizi maalumwa Naibu Katibu Mkuu CUF Tz bara, mhe Julius Mtatiro.
Kuna upotoshaji unaendelezwa hapa ndani na imenilazimu nitoe ufafanuzi.
1. Kuna watu wanajaribu kuwadanganya wadau humu kwamba mtatiro ndiye amejianzishia mada hii - napenda kuwahakikishia kuwa mtatiro hajaanzisha mada hii na hana ID za bandia katika mitandao kama ambavyo wengi humu tunafanya.

2. Mtatiro hana tabia ya kujifanya vile ambavyo hayuko, he is living in a real world na ndiyo maana lazima kuna watu watamuunga mkono na wengine hawatamuunga mkono,watampenda na kuna wengine watamchukia.

3. Mtatiro alijiunga CUF kwa utashi wake, pamoja na kufuatwa na viongozi kadhaa wakubwa wa vyama vya CCM na CDM bado aliamua kujiunga CUF kwa sababu mtatiro anaamini atawatumikia watanzania vizuri na kwa utashi zaidi akiwa CUF kuliko akiwa CDM au CCM.

4. Mtatiro hufuatilia mijadala yote humu jamvini na anaheshimu maoni ya kila mtu hata kama yana lengo la kupotosha wadau n.k.

Nilitaka kufafanua masuala haya muhimu kwani nimeona kuna haja ya kufanya hivyo.
 
Kama utakumbuka ule mgomo wa TAHLISO 2008 pindi Julius Mtatiro akiwa Waziri Mkuu wa DARUSU na Katibu Mkuu wa TAHLISO ni dhahili utagundua ni kwa nin mtatiro alikwenda CUF. Ktk ule mgomo ni CUF ndio walimpa mtatiro msaada wa kisheria, ikiwamo kulipia gharama zote za Wakili, so mtatiro aliwalipa fadhila CUF, But sina shaka atajiunga na CDM soon!
 
Kama utakumbuka ule mgomo wa TAHLISO 2008 pindi Julius Mtatiro akiwa Waziri Mkuu wa DARUSU na Katibu Mkuu wa TAHLISO ni dhahili utagundua ni kwa nin mtatiro alikwenda CUF. Ktk ule mgomo ni CUF ndio walimpa mtatiro msaada wa kisheria, ikiwamo kulipia gharama zote za Wakili, so mtatiro aliwalipa fadhila CUF, But sina shaka atajiunga na CDM soon!


Ndio maana nikasema taarifa nyingi zinazotolewa hapa ni uongo na zina malengo ya kuficha ukweli na usahihi wa taarifa.
Mgomo wa 2008 uliopelekea mtatiro kukamatwa na kufikishwa mahakamani ulifanyika wakati mtatiro ameshastaafu masuala ya uwaziri mkuu UDSM na ukatibu mkuu wa vyuo vikuu TZ, Serikali ilikuwa na hofu kuwa vyuo vilivyokuwa vikifungwa mfululizo wakati huo palikuwa na mkono wake kwa kiasi kikubwa(jambo ambalo mimi na wewe hatujui ukweli wake).
Alipofikishwa mahakamani alimkataa wakili kutoka CDM na wakili kutoka CUF na katika kesi ile alitetewa na wakili kutoka TANGANYIKA LAW SOCIETY hadi kesai ilipofutwa, kwa hiyo mtatiro hakuwahi kutetewa na wakili wa chama chochote cha siasa alipokuwa hajajiunga na siasa rasmi.
Tusilazimishe sababu kuwa kwa nini alijiunga CUF na siyo CDM, Kila mtu akijiunga CDM vyama vingine vote vijifute? na visipokuwepo CDM itapata challenge kutoka wapi?
 
Kila mtu akijiunga CDM vyama vingine vote vijifute? na visipokuwepo CDM itapata challenge kutoka wapi?

Kuna watu hawajui kuwa wapo watu hawafuati upepo bali upepo huwafuata wao. Mtatiro japo sio mtu mwenye busara ila ni mtu mwenye msimamo sana hayumbishwi wala si mchumia tumbo kama kundi la watoto walioenda CDM ambao wengi wao pia walikuwa wanajipeleka biyani.
 
Hivi watu wa chadema wana ulemavu wa akili? Maana wao wanaona kila kitu kizuri ni lazima kiwe Chadema! Acheni hizo!
 
Nyie watu bana, yaani mkiendelea kidogo tu mtaniaminisha kwamba mleta siredi ni Mtatiro.

Kwani ni nani asiyejua kuwa wakati ule CUF ilikuwa kwenye chati ?
 
Julius Mtatiro ni jembe kwelikweli hili halina ubishi hata John Mnyika anafahamu ukweli huu, ila mpaka leo nashindwa kuelewa kwanini mpambanaji huyu hakujiunga na CHADEMA badala yake akatimkia CUF?
alitoa sharti kuwa apewe ubungo kwa tiketi ya chadema mnyika, na wadau wa cdm wakagoma akaona bora aende cu then agombee ubungo dhidi ya mnyika
 
Nashindwa kuelewa mpaka sasa maana kwa jinsi navyomfahamu Mtatiro, angepata raha sana kama siasa zake angefanyia CDM.
 
Udini+ukabila wapi na wapi ? hii iko wazi kwani umakini na upembuzi wa mambo kwa Julius ni mdogo,kwahiyo viatu vay CDM vinge mpyaya..
 
Kwangu mie ambae namkumbuka tangu akiwa UDSM, ni mtu wa watu lakini anakosa misimamo binafsi inayomuongoza. Labda nae anasubiri anunuliwe maana CUF ndio ccm B
 
Apewe muda haalfu tutajua kama Mtatiro ni mwanapinduzi au la? Ila Kama alikwenda CUF kwa masilahi basi huko alikokwenda alipiga bao maana kama ni madaraka aliyoponayo CUF asingeyapata akiwa CHADEMA kwani kule kumesheheni vichwa. Binafsi naona ni bora apewe muda ili dhamira zake zijidhihirishe, na kwa mwendo wa kukosoa hata mazuri ya wapinzani sijui anasimama wapi.
 
Mtatiro kwenda CUF nakumbuka ni msaada waliompa pindi anakabiliwa na kesi za kupakaziwa kipindi yupo chuo(UDSM) na CUF ndio walimsimamia hadi mwisho hivyo tangu hapo akawa directly linked na ukiangalia na position aliyopewa ndio basi,lakini ninavyo mjua Mtatiro si mtu wa hoja yeye ni migomo tu tangu Ifakara akiwa waziri wa chakula hadi chuo akiwa waziri wa mikopo so anatakiwa abadilike awe mtu wa hoja anaweza akatufaa watanzania
 
Back
Top Bottom