Kwanini Joseph Kasheku (Msukuma) anadharau wasomi?

Kwanini Joseph Kasheku (Msukuma) anadharau wasomi?

Sasa kama masomi yenyewe ndio haya kina majalalani na kina kitila mkumbo unategemea waheshimiwe? majitu yako kama maroboti tu hayana mbele wala nyuma yanaitikia nyimbo zote, lazima wazarauliwe tu
 
Msukuma anaponda elimu ya kibongo ila hapondi unachokiandika maana vyote hivo havijatengenezwa na elimu hii ya kukariri matundu ya panzi.

ni ukweli ulio uchi elimu ya kibongo ni ya hovyo sana, hawa tunaowaita wasomi ndo wametufikisha hapa kama taifa kwa zaidi ya miaka 50. Msomi wa kibongo hana uelewa wowte na hawezi kubuni chochote zaidi zaidi kukariri tu yale madude ya kwenye karatasi.. hii elimu yetu imelisadia nn taifa hili?

Namuunga mkono msukuma kwasababu yeye hajasoma lkn ni tajiri,je ww msomi una nini cha maana zaidi ya kende?
Siku ukipata tezi dume ndio utajua maana ya wasomi. Nchi hii ipo kwa sababu kuna wasomi unaowadharau. Usomi sio tu kugundua mabom ya nuclear hata kusimamia mambo ni usomi.
Ugunduzi mda mwingine hauna uhusiano na usomi, hata asie msomi anaweza kugundua kitu.
Watu wengi wasio wasomi wamegundua vitu ila wasomi wamevitengenezea utaratibu.
Hata ulaya wagunduzi ni kama 1% ya watu wote wa ulaya.
Hata huuu mfumo wa JF unaongozwa na wasomi waliosoma TZ.
Unapokea simu kwa sababu kuna msomi anadhibiti mitambo.
 
Tatizo la nchi sio wasomi,tatizo letu kama nchi ni kuruhusu siasa kwenye vitu vya kitaaluma,..wasomi bado wanafanya vizuri sana kwenye hii nchi,na mtu anayemponda msomi yawezekana yeye ameshindwa fikia hiyo level...Yes,yako madhaifu kadhaa kwenye Elimu yetu,lkn sio kweli kwamba Elimu yetu ni mbaya kupita kiasi,wako Watanzania Wasomi wanaofanya makubwa...Mfano kwenye field ya Afya kwa sasa Tanzania ni bora kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki,nchi kama Kenya na Uganda zinakuja jifunza hapa,kwa hiyo bado wasomi wetu wanafanya vizuri.
Changamoto tulionayo na hawa wasomi kuwezeshwa,unaweza ukawa na Elimu lkn kama hujatengenezewa mazingira mazuri,hiyo Elimu hutaweza itumia,lkn pia lazima tuache kuingiza siasa kwenye taaluma,...unakuta mwanasiasa ana nguvu na anataka kumuongoza mtaalamu,inabidi huyu mtaalamu awe mpole,maana mwenye nguvu mpishe...kwa kumalizia Elimu yetu bado ni bora,na wasomi wapewe nafasi.
 
Niko na huyo mueshimiwa msukuma wa somi wengi wamesomea kuneemesha matumbo yao na familia zao msukuma aendelee tu kuawasukuma hao wasomi
 
Anadharau wasomi sababu hawana pesa kama yeye na hao wasomi wameshindwa kuonyesha usomi wao na wamefanya siasa kama ajira, wakati Musukuma siasa ni kijiwe chake cha kupiga dili za kitapeli, kutokana na jeuri yake hata mawaziri wanamuogopa, jeuri yake ya pesa inamfanya apate vibali mbalimbali kama vya kuagiza au kuuza michele nje, kupata viwanja vya kujenga apartments sehemu azitakazo kutoka kwa watawala ambao wanamuogopa kwa kuhusu kuwa anaweza kuwa blackmail. Musukuma ana ukwasi mkubwa wa pesa lakini sidhani kama analipa kodi. Musukuma ni mhuni tu ila ni mjanja wa kujigeuza, huyu mwanzoni wakati wa kinyang'ang'anyiro cha kumpata raisi alikuwa kundi la Lowasa akiwa na akiwa na akina Kingunge ,Tibaijuka,Awesu na nakumbuka wakati wa mkutano wa Lowasa uwanja wa Sheikh Amri Abeidalikuwa wa mwisho kufika na akashuka na helicopter uwanjani, lakini baada ya kuona upepo umebadirika akjigeuza na kuwa mfuasi kindakindaki wa Jiwe na baada ya Jiwe kutwaliwa kageuka chawa wa mama! Huyo ndio Musukuma yeye yupo kuchumia tumbo lake.
Sijaona lolote la maana hapo yeye kama darasa la 7 hapo, kukwepa Kodi ndo ujanja au, kuwa kigeugeu ndo ujanja au?
 
Elimu ya Tanzania sio ya hovyo hata kidogo, Iko poa kabisa, ukimaliza High school Tanzania unaweza kusoma Harvard bila shida yoyote, hii inaonesha elimu yetu Haina tatizo,
Kinachokosekana Tanzania ni technology tu.
 
Ni kilaza tu huyo,..hupaswi kutumia nguvu kushindana na kilaza
 
Bungeni anaongea. Anadharau wasomi. Wasomi waliopo Bungeni wanashindwa kumjibu, tena anawatisha.

Anasahau kuwa akiugua anatibiwa na wasomi, magari yake yote yametengenezwa na wasomi, SGR inajengwa na wasomi ndio maana mabehewa yatembea kwenye reli bila kuanguka, umeme unasambazwa na wasomi, bararaba zinajengwa na wasomi.

Na kadhalika na kadhalika. Kila kitu cha kusomi kina taratibu zake. Anataka zisifuatwe.

Wasomi walioko Bungeni wanashindwa kumwambia haya.

Anataka nchi iendeshwe kwa matamko na mitulinga. Hata hiyo mitulinga inahitaji wasomi kuitekeleza.

Bwawa la Nyerere, pamoja na kutolewa maoni kuwa litaathiri mazingira. Waliotoa maoni yale hawakusema lisijengwe.

Yalikuwa maoni ya kisomi. Linajengwa na wasomi. MSUKUMA anataka nini?

Anasema yeye darasa la 7 lakini katamani usomi mpaka amenunua PHD.
Kwa sababu wasomi ni wajinga
 
Tatizo wasomi wanataka kutambulika kwa usomi wao wa kukariri maandishi na theory kuwa ndio taaluma, elimu ya Tanzania haina inachomsaidia mtanzania kabisa...kiufupi ni kupoteza muda huko kunakoitwa shuleni to vyuoni...watu hawajifunzi vitu vinavyohitajika katika mazingira yao ya kileo...ila kumezeshwa majitu mengi ya hovyo yasiyokuwa na uhalisia wa maisha ya leo...hawawezi kutatua changamoto za leo halafu wanataka kuheshimiwa....kwa lipi hasa....inachukiza...namuunga mkono mdau.
Hakika [emoji3578][emoji3578] ila kwa upande mwingine wa shilingi ni kwamba msukuma ni inferiority complex pia inamchagiza kuwapondea hao wasomi.
 
Siku ukipata tezi dume ndio utajua maana ya wasomi. Nchi hii ipo kwa sababu kuna wasomi unaowadharau. Usomi sio tu kugundua mabom ya nuclear hata kusimamia mambo ni usomi.
Ugunduzi mda mwingine hauna uhusiano na usomi, hata asie msomi anaweza kugundua kitu.
Watu wengi wasio wasomi wamegundua vitu ila wasomi wamevitengenezea utaratibu.
Hata ulaya wagunduzi ni kama 1% ya watu wote wa ulaya.
Hata huuu mfumo wa JF unaongozwa na wasomi waliosoma TZ.
Unapokea simu kwa sababu kuna msomi anadhibiti mitambo.

Lakini siku zote Msukuma huwa anaongelea wasomi alio nao bungeni ambao huaminika kwa usomi wao lakini hakuna lolote zuri kutoka kwao.
 
Wasomi wengi wanaringia elimu zao ingawa hizo elimu zao hazina tija kwa taifa, kifupi ni kwamba wasomi wengi wana elimu lakini hawana akili za kutumia akili zao, yaani wanaupungufu wa akili.
 
Mbona yeye alinunua PhD ili aitwe Doctor..
Ile waTz wajinga ndio maana comments nyingi zinasema wasomi gani mbona amezidi pesa?
Swali la kipumbavu sana hilo...
Wasomi wengine Tu kama Newton, Eisten wamekufa bila hela lakin kanuni zao zina matokeo halisi kwenye maendeleo ya binadamu
 
Ukimjudge msukuma kwa kutumia feeling lazima uchemke, lakini jamaa anachokizungumza kina ukweli ndani yake.
 
Back
Top Bottom