Kwanini Jazz sio maarufu kwetu TZ?

Kwanini Jazz sio maarufu kwetu TZ?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Hivi ni kwanini muziki wa Jazz wenye asili yake huko nchini Marekani sio maarufu hapa nchini Tanzania? Miziki ya aina nyingi kutoka nchini Marekani ni maarufu sana hapa kwetu kama vile Reggae, Hip Hop, House, Rock & Roll, Pop n.k. lakini sio Jazz, sasa ni kwanini?

Je, hii ni sababu ya IQ yetu kuwa ndogo au ni nini? Kwa maana aina hii ya muziki wa Jazz mara nyingi hupendwa sana na watu very intelligent kama nobel laureates, wanasayansi n.k.
Je, moja ya sababu yaweza kuwa kwamba hatuwezi kuuelewa na kuweza kuenjoy aina hii ya muziki mzuri duniani?
 
Bongo mziki maarufu ni bongoflava na hip hop

hizo nyingine mbwembwe tu
 
Bongoflava, raggae na Hiphop ni miziki famous sana Tanzania.

Pop, rock and roll, country, jazz hata blues sio miziki inayovuta attention ya watu hasa nchi nyingi za Afrika.
 
Acha kuchapia bana, wapi USA na wapi Jazz?

Hizi Band kama Sikinde, Mlimani, Tabora Jazz nk zilikuwa ni JAZZ Band kikwelikweli na wala siyo utani.

Baadhi ya wanamuziki wa Jazz ni kama Hugh Masekela, Angelique Kidjo, Miriam Makeba, Richard Bona.......

[video=youtube;_Vskq0LueWs]https://www.youtube.com/watch?v=_Vskq0LueWs[/video]

Hapa chini kuna wimbo wa Bona, naupenda sana na ndani kuna Kimzigo kinaimba vizuri tu, sijui mtakiona? Killing smile yake kwa kweli inafurahisha. Angalia na wewe ugundue. Bona anatoka Cameroon na ni Mbantu, hivyo akiimba unakuwa kama unaelewa kidogo ila kumbe mhhh...... Ni mmoja ya wapiga Bass gitaa maarufu duniani, Top 10 ni lazima utamkuta huyu mchawi.......

 
Last edited by a moderator:
Wazee wa jazz tupo mkubwa, tunawajua kina George Benson, Earl Klugh ,Grover Washngton Jr, Carlos Santana , George Howard wako wengi me ninazo jazz nyingi tu.
 
Sikonge

duh, huo mziki wameunasinisha kama jazz lakini sio Jazz hiyo, hiyo ni socca rhumba, sifa kubwa ya jazz ni ala za upepo
 
Last edited by a moderator:
Kuna kushabikia na kusikiliza Music- wengi ni mashabiki wa Music -kuipenda Jazz lazima mawimbi na sauti ya vifaa vya music uzifahamu,kimsing ni music ulovunjwa vujwa keys.
 
BB King alikuwa mpiga Blues. Blues iko maarufu sana West Africa na huko ndiko asili yake.

Wanamuziki kama Ali Farka Toure ni Muafrica maarufu wa huo mziki, Erick Clapton, John Lee Hooker, Ray Charles, Muddy Water na wengineo weengi. Blues haipishani sana na Gospel hadi leo....



https://www.youtube.com/watch?v=LSWuzp_0hn4

Jazz. Namkumbuka BB King...

mkuu,that man was a true king..nilimjua thru my late dad.
Alikuwa anaekathose classics and jazz musics kitambo hicho
afu anantafsiria..si unajua saint kabwela..kizungu aleji(mzio)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kituko, hiyo ni Jazz. Sikiliza aina ya upigaji wa ala za mziki utajua ni jazz. Kuna aina nyingi sana za Jazz.

Ninao wimbo Original na ninaipenda sana hiyo CD, ila haupo kwenye Jazz,upo zaidi kwenye Salsa.

Kwa kubadilisha kidogo upigani, wanaita Cuban Jazz. Hii ni Jazz iliyo karibu na mziki wa Cuba.

Dahh,Soca Dance? Tafadhali bana, walau ungelisema Marengue Music vs Soca.

Wimbo wa Dolly Parton I Will Always Love You ulikuwa Country song ila Babyface na wenzake wakaubadilisha kabisa na akauimba Whitney Houston kama R&B.

John Lennon hakuwa mpiga Jazz hata kidogo, ila angalia Herbie Hancock alivyoufanya wimbo wake wa Imagine.



<b><a href="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=8870" target="_blank">Sikonge</a></b>

duh, huo mziki wameunasinisha kama jazz lakini sio Jazz hiyo, hiyo ni socca rhumba, sifa kubwa ya jazz ni ala za upepo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom