Kwanini Januari Makamba anawatesa

Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
901
907
Katika miaka mitatu hii kama kuna Waziri aliyeonyesha utulivu, weledi, ukomavu na kujiamini basi ni Januari Makamba. Amekaa kimya, anafanya kazi zake kimyakimya bila mihemko na kwa ufanisi na pale anapozungumza mara moja moja basi anatema busara tu. Hata hivyo, pamoja na ukimya wake bado amebaki gumzo. Na kila baada ya muda unaandikwa uzi au story inatungwa kumhusu na kusambazwa. Swali langu: nani anateswa na ukimya wa Januari Makamba? Shida ni nini?

Kama shida ni yeye kuchukua fomu kubwa mwaka 2020, yeye kishatangaza anarudi Bumbuli na kule hana mpinzani ndani ya CCM na nje. Na yeye kakulia kwenye Chama na anajua utaratibu wa CCM. Kama shida ni 2025, nimemfuatilia kauli zake na mienendo yake; hakuna mahali amesema anataka Urais na hakuna mahali ameonyesha hata dalili. Mara ya mwisho nimemsikia akihojiwa na Gerald Hando wa EFM kuhusu 2025 na akasema “sasa hivi ni mapema sana kuzungumzia au kuamua au kujipanga kuhusu 2025 na tuna Rais ambaye bado ana muda mrefu, aachwe afanye kazi na ikifika wakati huo kama mahitaji ya mimi kuwemo basi nitaamua wakati huo lakini sio sasa”. Sasa tishio linalofanya watu wahangaike kumchafua linatoka wapi?

Labda nijaribu kuchakata kitu kimoja kilichonijia kichwani: tishio kubwa ni heshima aliyonayo kwenye jamii na ushawishi alionao kwa makundi mbalimbali kuanzia Marais wastaafu (Mzee Mwinyi, aliandika dibaji ya kitabu chake; Mzee Mkapa, alimsomesha Marekani; Mzee Kikwete, alifanya naye kazi na kumlea kisiasa). Yuko karibu na Mzee Kinana na wazee wengine wa Chama; yuko karibu na viongozi wa dini zote. Zanzibar anakubalika sana, kuliko mwanasiasa yoyote wa Bara. Hadi wapinzani Bungeni wanamkubali. Kubwa zaidi yupo karibu na media na makundi ya vijana. Mitandaoni anaheshimika, ana wafuasi wengi na anasikilizwa.

Mimi naona hii ndio inatesa watu. Wachafu wanataka achafuke nao. Na dhambi kubwa ya CCM ni kuchafuana. Yaani CCM wenyewe hawataki kuwe na msafi miongoni mwao hata mmoja. Katika kampeni za CCM za 2020, Januari ni moja ya turufu ya mikakati na ushawishi hasa kwa vijana.

Nimeona uzi wa kipuuzi kabisa unatembea eti kama “salamu kwa Januari Makamba” kwamba kakosea kuelezea historia ya chanzo cha jina Tanzania, wakati Januari kasema uhalisia wa historia. Kama umedanganywa huko nyuma usilaumu aliyekupa maarifa, ndio ushukuru sasa umepata ufahamu. Yaani mtu yuko tayari kupingana na historia na rekodi iliyopo hadi Serikalini kisa tu ampige Januari Makamba. Upuuzi wa kuungaunga hauwezi kumwangusha mtu mwenye nyota ya kupendwa na anayeheshimika. Story za kutunga za Bumbuli, ambako Januari ni kama mfalme na hana mpinzani, haziwezi kushusha nyota yake.

Nawashauri wanaoteseka kwamba kwa Januari wanahangaika na mwanamikakati aliyepikwa na Jakaya, Kinana, Mzee Makamba na akachanganya na maarifa ya kisasa ya kijasusi na akaiva kisawasawa. Wanaoteseka naye mnacheza na kivuli, mwenzenu yuko dakika 30 mbele.

Mwalimu Julius Kato
Geita
28 April 2019.
Sauti ya mtu inasikaka inasikika nyikani yaandaeni mapito ya bwana..
images.jpeg
 
Sawa Praise Team ya JM.

Ila kwenye suala la mifuko ya plastic naona kakurupuka japo ni jambo zuri sana.

Angetakiwa kwanz kuhakikisha ma supplier wanasambaza mifuko ya karatasi kwanza.
Angeanzia viwandani

Ila alichofanya ni kuwaumiza wafanyabiashara wadogo.

Huyu ana mpango wa kuwa rais.

Kwa nini jambo dogo kama hili alishindwa kuliona?
 
Sawa Praise Tema ya JM.

Ila kwenye suala la mifuko ya plastic naona kakurupuka japo ni jambo zuri sana.

Angetakiwa kwanz kuhakikisha ma supplier wanasambaza mifuko ya karatasi kwanza.
Angeanzia viwandani

Ila alichofanya ni kuwaumiza wafanyabiashara wadogo.

Huyu ana mpango wa kuwa rais.

Kwa nini jambo dogo kama hili alishindwa kuliona?
Uko sahihi kabisa mzee, angehakikisha kwanza kuna supplies ya kutosha mtaani ya mifuko mbadala wa plastic, lkn kusema mwisho tarhr flan alafu hpo hpo eti ndio wanaita watu waende wakajadili mbadala wa hii mifuko huko ni kukurupuka mnoooo.
 
Uko sahihi kabisa mzee, angehakikisha kwanza kuna supplies ya kutosha mtaani ya mifuko mbadala wa plastic, lkn kusema mwisho tarhr flan alafu hpo hpo eti ndio wanaita watu waende wakajadili mbadala wa hii mifuko huko ni kukurupuka mnoooo.
Porojo
 
Hana sifa za kuwa raisi ukatibu mkuu wa chama na fadhila za mkwele ndio ngekewa anayo safiria. Kama kuna anae jua aniambie kafanya nini?
 
Nyie mijitu mipumbavuh sijui mtaisha lini....january anaweza mwogopesha nani?umaskini wako unakufanya ujipendekeze tu kwa watu na kuja kuanzisha uzi wa kipumbavu.Kama unamuandaa aje kugombea Urais basi agombee urais wa familia yako. Kama anakubalika zanzibar aende kugombea Zanzibar au huko Bumbuli.
 
January mtu mbaya sana huyo kijana huwa anajifanya mtu mwema mbele za watu lkn nyuma ya pazia ni zaidi ya mnyama bora hata magufuli
Huyu atauza nchi kwa wahindi na waarabu maana anawasujudu sio kitoto
 
Utawala wa magufuli wanamchukia na ndio fitna mkubwa waliiofanya ukawa kushindwa 2015 Kwa kuiba kurwa ikishirikiana Nape,Mwigulu.Kinana,na wenzake wote wamefukuza bado yeye anatafutiwa kosa ila naye amechaligundua ndio yupo kimya
 
Back
Top Bottom