Kwanini Januari Makamba anawatesa

Kwanini Januari Makamba anawatesa

Utawala wa magufuli wanamchukia na ndio fitna mkubwa waliiofanya ukawa kushindwa 2015 Kwa kuiba kurwa ikishirikiana Nape,Mwigulu.Kinana,na wenzake wote wamefukuza bado yeye anatafutiwa kosa ila naye amechaligundua ndio yupo kimya
wakimfukuza watamuweka nani? Makonda?
 
Utawala wa magufuli wanamchukia na ndio fitna mkubwa waliiofanya ukawa kushindwa 2015 Kwa kuiba kurwa ikishirikiana Nape,Mwigulu.Kinana,na wenzake wote wamefukuza bado yeye anatafutiwa kosa ila naye amechaligundua ndio yupo kimya
Hivi unaamini magufuli anaweza akashindwa kumtoa? Magufuli na January ni marafiki wakubwa tofauti na wewe unavyowaza
 
Mmeshaanza pumba za kusifiana humu, muda ukifika wagombea watajitokeza na walio na weledi na kazi hiyo watapitishwa, hakuna sababu ya kuwashwa washwa
 
Ila nimemuona juzi ile siku ya maadhimisho ya muungano kwa kweli kapungua sana sijui anasumbuliwa na nini kakonda hadi uso
 
#Musiba
IMG_20190429_091639.jpeg
 
Sawa Praise Tema ya JM.

Ila kwenye suala la mifuko ya plastic naona kakurupuka japo ni jambo zuri sana.

Angetakiwa kwanz kuhakikisha ma supplier wanasambaza mifuko ya karatasi kwanza.
Angeanzia viwandani

Ila alichofanya ni kuwaumiza wafanyabiashara wadogo.

Huyu ana mpango wa kuwa rais.

Kwa nini jambo dogo kama hili alishindwa kuliona?
mzee umesahau ya viroba
 
January sio mtendaji hata kidogo, anajitahidi kuongea kwa busara, ila busara sio maendeleo, hatuhitaji mtu wa busara, tunahitaji mchapa kazi kama Mh Rais wetu JPM...!! Busara, au sijui maneno mazuri apeleke kwa mke wake na vimada wake.. Hapa Kazi Tu
 
Katika miaka mitatu hii kama kuna Waziri aliyeonyesha utulivu, weledi, ukomavu na kujiamini basi ni Januari Makamba. Amekaa kimya, anafanya kazi zake kimyakimya bila mihemko na kwa ufanisi na pale anapozungumza mara moja moja basi anatema busara tu. Hata hivyo, pamoja na ukimya wake bado amebaki gumzo. Na kila baada ya muda unaandikwa uzi au story inatungwa kumhusu na kusambazwa. Swali langu: nani anateswa na ukimya wa Januari Makamba? Shida ni nini?

Kama shida ni yeye kuchukua fomu kubwa mwaka 2020, yeye kishatangaza anarudi Bumbuli na kule hana mpinzani ndani ya CCM na nje. Na yeye kakulia kwenye Chama na anajua utaratibu wa CCM. Kama shida ni 2025, nimemfuatilia kauli zake na mienendo yake; hakuna mahali amesema anataka Urais na hakuna mahali ameonyesha hata dalili. Mara ya mwisho nimemsikia akihojiwa na Gerald Hando wa EFM kuhusu 2025 na akasema “sasa hivi ni mapema sana kuzungumzia au kuamua au kujipanga kuhusu 2025 na tuna Rais ambaye bado ana muda mrefu, aachwe afanye kazi na ikifika wakati huo kama mahitaji ya mimi kuwemo basi nitaamua wakati huo lakini sio sasa”. Sasa tishio linalofanya watu wahangaike kumchafua linatoka wapi?

Labda nijaribu kuchakata kitu kimoja kilichonijia kichwani: tishio kubwa ni heshima aliyonayo kwenye jamii na ushawishi alionao kwa makundi mbalimbali kuanzia Marais wastaafu (Mzee Mwinyi, aliandika dibaji ya kitabu chake; Mzee Mkapa, alimsomesha Marekani; Mzee Kikwete, alifanya naye kazi na kumlea kisiasa). Yuko karibu na Mzee Kinana na wazee wengine wa Chama; yuko karibu na viongozi wa dini zote. Zanzibar anakubalika sana, kuliko mwanasiasa yoyote wa Bara. Hadi wapinzani Bungeni wanamkubali. Kubwa zaidi yupo karibu na media na makundi ya vijana. Mitandaoni anaheshimika, ana wafuasi wengi na anasikilizwa.

Mimi naona hii ndio inatesa watu. Wachafu wanataka achafuke nao. Na dhambi kubwa ya CCM ni kuchafuana. Yaani CCM wenyewe hawataki kuwe na msafi miongoni mwao hata mmoja. Katika kampeni za CCM za 2020, Januari ni moja ya turufu ya mikakati na ushawishi hasa kwa vijana.

Nimeona uzi wa kipuuzi kabisa unatembea eti kama “salamu kwa Januari Makamba” kwamba kakosea kuelezea historia ya chanzo cha jina Tanzania, wakati Januari kasema uhalisia wa historia. Kama umedanganywa huko nyuma usilaumu aliyekupa maarifa, ndio ushukuru sasa umepata ufahamu. Yaani mtu yuko tayari kupingana na historia na rekodi iliyopo hadi Serikalini kisa tu ampige Januari Makamba. Upuuzi wa kuungaunga hauwezi kumwangusha mtu mwenye nyota ya kupendwa na anayeheshimika. Story za kutunga za Bumbuli, ambako Januari ni kama mfalme na hana mpinzani, haziwezi kushusha nyota yake.

Nawashauri wanaoteseka kwamba kwa Januari wanahangaika na mwanamikakati aliyepikwa na Jakaya, Kinana, Mzee Makamba na akachanganya na maarifa ya kisasa ya kijasusi na akaiva kisawasawa. Wanaoteseka naye mnacheza na kivuli, mwenzenu yuko dakika 30 mbele.

Mwalimu Julius Kato
Geita
28 April 2019.
Sauti ya mtu inasikaka inasikika nyikani yaandaeni mapito ya bwana..View attachment 1083741
Mbona povu linakutoka
 
Kuna ile ishu ya dada yake kudanga na mzungu na wakatengeneza deal wakapiga 1.nakitu milion dollars ili kampuni ya mzungu ipate tenda bagamoyo kule ila sio kesi wote tunafanya makosa lakini
 
Kifahamu CCM vizuri - kiko tofauti sana:-
Wakati Nyerere anang'atuka wengi walidhani Rais angekuwa PM wake lkn akaibuka na Mwinyi,
Wakati Mwinyi anang'atuka tukadhani Kikwete/Salim mmoja angekuwa Rais lkn akaibuka Mkapa,
Wakati Mkapa amemaliza watu wakadhani Salimu/Mwandosya lkn akapewa JK,
Wakati JK anang'atuka watu wakadhani Lowassa lkn akaibuka JPM

CCM hakipangiwi hata ung'ae kama dhahabu CCM inang'aa zaidi
Awe tayari kupokea matokeo - bahati nzuri kwake iwe JPM afanikiwe asipofanikiwa baraza lake lote halitapewa dhamana ya uongozi tena
 
Nyie mijitu mipumbavuh sijui mtaisha lini....january anaweza mwogopesha nani?umaskini wako unakufanya ujipendekeze tu kwa watu na kuja kuanzisha uzi wa kipumbavu.Kama unamuandaa aje kugombea Urais basi agombee urais wa familia yako. Kama anakubalika zanzibar aende kugombea Zanzibar au huko Bumbuli.
Haya ni matusi eti january naye anafaa kuwa rais? Kweli ccm imekufa
Labda kama hawamjui huyo kijana!
 
hatutaki mtu sijui mstaarabu,sijui mwadilifu,huo uadilifu apeleke kwenye family yake,baada ya jpm,tunaweka kitu kingine mfano mkuchika,au lugola
 
Sijawai kuwaelewa walimu ni watu wasiojielewa ikiwemo na huyu mleta mada.
 
Back
Top Bottom