aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 834
- 1,213
Ndugu Watanzania kila mtu anayo haki ya kuishi maisha popote pale kwa kuzingatia misingi ya sheria ya ukaazi wa eneo husika.
Nasikitishwa na baadhi ya watu ambao kwa matakwa yao waliamua kuhama kutoka Tanzania bara na kuja visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutafuta riziki zao kutelekeza familia zao.
Utelekezaji upo wa aina mbili.
1.Baba kukimbia familia
2.Baba anaishi na familia lakini hatoi huduma zinazostahiki hata kama ana uwezo na pia kutojali Watoto kusoma.
Wakina Mama wengi wa bara na visiwani wanalalamikia utelekezwaji wa familia,lakini kuna kitu nikakibaini kwa ambao sio wazawa kwamba kipo tofauti na kutoka katika makabila Matatu yanayopatikana Tanzania bara ambao wanaishi hapa visiwani.
Kuna watu kutoka kabila la Musoma baadhi yao sio wote ,watu wa kabila la Kinyamwezi na ni baadhi ikiwemo watu kutoka Kondoa.
Baadhi yao na sio kidogo hawana habari ya watoto kusoma hata ile elimu ya lazima yaani Skuli ya Msingi.
Ukiwauliza Wazazi wote wawili utagundua kwamba Mama hana kauli,maana Mama atasema mimi sina uwezo na Baba yao anasema hata yeye hakusoma na kwao elimu sio ya lazima.
Unapomkabili Baba anaweza kuwa na majibu mawili kwamba sina uwezo au watoto wenyewe hawataki.
Lakini unapowahoji Watoto wakiwa peke yao wanakwambia shida ni sare za Skuli Baba hataki kununua tunavaa mpaka zinachanika kwamba hazifai tena.
Kwa hiyo baadhi yao wanaendeleza utamaduni ambao hata Tanzania Bara haukubaliki,kwamba mzazi aamue tu kwamba Skuli au Shule haina umuhimu kwa Watoto wake.
Haya wapo wengine ambao walikuja na waume zao kisha waume wakawatoroka na hawajui walipo wanasikia tu habari Mume yupo kijiji fulani alimuradi mateso kwa familia.
Nilijaribu kugusia suala la ukeketaji 😡 Kwa hizo kabila maana niliingiwa na wasiwasi kwamba huenda jambo hilo linafanyika kwa Siri visiwani.
Nikapata baadhi yao ambao wanasema huwa hawafanyi hapa bali wanasafiri maana Kumbe kuna msimu maalum.lakini wengine wakasema wapo ambao hufanya hapahapa kwamba kumbe kuna Mangariba! Lakini waliombwa kuhifadhiwa wasijulikane.
Niliwauliza wakina Mama ambao Watoto wao hawasomi kwamba je kama watoto wao hawasomi wanafanya nini? Wakasema wanasaidiana na Baba zao kazi za ukulima na kwa wenye kufuga basi wanasaidiana na wale wadogo kabisa husalia Nyumbani.
Swali la mwisho nikauliza je wanapenda Watoto wao wasome? Wengi walisema wanapenda Watoto wao wasome hata kwa kuwagharamikia wao ila hawana chanzo cha mtaji.
Kuna mwingine anasema alikuwa akifanyakazi ya kufua kwa watu na kulima ili aweze kusomesha wanawe,lakini mume alipoona hivyo akamwachia majukumu yote ya familia ikiwemo kulisha chakula na hata watoto wakiumwa na mambo mengiyo.hiyo ikawa ni shida akashindwa.
Kwangu mimi inakuwa ni habari haswa suala linapozidi watu zaidi ya 20.
Jambo jingine wakina mama wana hofu hata kusikika Radioni wanaona watakuwa wamejipalia makaa ni wachache wanaokubali lakini ninaendelea na jitihada za kuvunja ukimya na naona tunaelekea kuzuri nitaleta mrejesho muwasikie.maana nahitaji idhini yao kurusha mahojianoe.
Ahsante