Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,163
- 10,891
India inatajwa kuwa ni moja ya mataifa yenye idadi kubwa ya wanajeshi na moja ya nchi zenye kumiliki silaha za nyuklia.Hata hivyo kila inapotokea kupigana na kushambuliana na majirani zake basi hushindwa vibaya mpaka ikabidi kuonewa huruma na adui yake.
Mfano katika mashambulizi mwishoni mwa mwaka jana na jirani na hasimu yake mkubwa,Pakistan kwanza ndege zao zilikosea shabaha na wakatoa takwimu bandia ambazo baadae zilikanushwa kwa ushahidi na Pakistani.
Katika mashambulizi yale rubani wake mmoja alitunguliwa na Pakistan na kushikwa mateka mpaka pale Pakistan walipoona huruma na kumrudisha kwao akiwa amenyongeka kwa aibu.
Juzi tena katika kushambuliana eneo la Ladakh mpakani na China walipigwa kwa magumi na mafimbo mpaka askari wake India wapatao 20 wakafa na idadi nyengine kushikwa mateka na China na hatimae kuachiwa huru hapo jana.
Katika mapigano hayo India bila aibu imekubali kuwa askari wake 20 kweli waliuliwa na China na wala haikusema iwapo waliweza angalau kumjeruhi angalau mmoja wa upande wa pili.Sijui ingekuwaje kama China wangeamua kutumia silaha za moto.