Kwanini India katika kila vita hushindwa vibaya sana

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
2,650
2,000
India inatajwa kuwa ni moja ya mataifa yenye idadi kubwa ya wanajeshi na moja ya nchi zenye kumiliki silaha za nyuklia.Hata hivyo kila inapotokea kupigana na kushambuliana na majirani zake basi hushindwa vibaya mpaka ikabidi kuonewa huruma na adui yake.

Mfano katika mashambulizi mwishoni mwa mwaka jana na jirani na hasimu yake mkubwa,Pakistan kwanza ndege zao zilikosea shabaha na wakatoa takwimu bandia ambazo baadae zilikanushwa kwa ushahidi na Pakistani.

Katika mashambulizi yale rubani wake mmoja alitunguliwa na Pakistan na kushikwa mateka mpaka pale Pakistan walipoona huruma na kumrudisha kwao akiwa amenyongeka kwa aibu.

Juzi tena katika kushambuliana eneo la Ladakh mpakani na China walipigwa kwa magumi na mafimbo mpaka askari wake India wapatao 20 wakafa na idadi nyengine kushikwa mateka na China na hatimae kuachiwa huru hapo jana.

Katika mapigano hayo India bila aibu imekubali kuwa askari wake 20 kweli waliuliwa na China na wala haikusema iwapo waliweza angalau kumjeruhi angalau mmoja wa upande wa pili.Sijui ingekuwaje kama China wangeamua kutumia silaha za moto.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,861
2,000
... sio kweli kwamba kila vita na jirani zake India inashindwa vibaya na umetoa mfano wa Pakistan. Kasome historia ya migogoro baina ya nchi hizi mbili halafu urudi kutoa majibu hapa. Nenda kasome role ya India kwenye mgogoro kati ya Pakistan na Bangladesh ndipo utajua jinsi Bangladesh anavyomheshimu India jinsi alivyomaliza sakata lile Pakistan akiaibika ile mbaya.
 
Science Priest

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
1,811

Kaleta mada kishabiki, na anatakiwa afahamu china hawajasema ni wanajeshi wake wangapi hawajafa
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
21,056
2,000
Mambo yahusuyo majeshi,usije danganywa na taarifa za upande mmoja ukaamini ni kweli inawezekana.

Yaani ugomvi wa mitama,wanajeshu wa india wadundwe tu wanaangalia,au kwa vile wachina wanajua tai chi??
 
Mkogoti

JF-Expert Member
May 3, 2020
1,747
2,000
Kuna nyingine taarifa sijui nilisoma sehemu nimepasahau! Inahusu India walirusha na wenyewe Ile kitu inayoendaga mwezini, sasa bwana sijui walicheck kwenye computer science zao.

Wakasema mwezini kuna maji mengi sana! Lakini Pakistan wakaja kukanusha na kuutangazia ulimwengu kwamba mbona kitu chao hicho cha India kimeanguka kipo baharini. Sasa wenyewe India walijua mwezini kuna maji kumbe kitu kipo baharini kimeanguka🤣🤣
 
Paula Paul

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
4,015
2,000
Acha uongo wewe, India imepigana vita kamili nne na Pakistan na mara zote walitembeza mkong'oto, India iliisaidia Bangaladesh kupata uhuru kutoka Pakistan, au kwa lugha rahisi ilifanikiwa kuimega Pakistan na kuipunguza nguvu.
Bila kusahau vita ya 1971 Pakistan alisaidiwa na UK, US , Iran nk ..lakini bado India akabeba ushindi.
 
General Galadudu

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,840
2,000
Kuna nyingine taarifa sijui nilisoma sehemu nimepasahau! Inahusu India walirusha na wenyewe Ile kitu inayoendaga mwezini, sasa bwana sijui walicheck kwenye computer science zao.

Wakasema mwezini kuna maji mengi sana! Lakini Pakistan wakaja kukanusha na kuutangazia ulimwengu kwamba mbona kitu chao hicho cha India kimeanguka kipo baharini. Sasa wenyewe India walijua mwezini kuna maji kumbe kitu kipo baharini kimeanguka
........ We jamaa fala sana duh.
 
njumu za kosovo

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
418
1,000
Hahahahaa pia kilisema mwezini kuna vibua
Kuna nyingine taarifa sijui nilisoma sehemu nimepasahau! Inahusu India walirusha na wenyewe Ile kitu inayoendaga mwezini, sasa bwana sijui walicheck kwenye computer science zao.

Wakasema mwezini kuna maji mengi sana! Lakini Pakistan wakaja kukanusha na kuutangazia ulimwengu kwamba mbona kitu chao hicho cha India kimeanguka kipo baharini. Sasa wenyewe India walijua mwezini kuna maji kumbe kitu kipo baharini kimeanguka🤣🤣
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom