Kwanini inaitwa mikoa ya pembezoni?

mlimbwa1977

Member
Feb 7, 2011
24
0
Mara kwa mara nimekuwa nikisikia kauli za viongozi mabalimbali hasa bungeni(mawaziri) kwamba wafanyakazi wanaopangiwa kazi katika mikoa ya pembezoni wanaacha kazi.Napenda kufahamu tofauti iliyopo kati ya mikoa ya pembezoni,mikoa masikini na mikoa iliyo mipakani.

Pia nimekuwa nikisia matamshi yanayotolewa na waandishi wa habari/watangazaji,kwa mfano,tukio la mabomu lililotokea gongolamboto nje kidogo ya jiji la Dar es salaam,police wamempeleka mtuhumiwa kituo cha kati.

Kama unao uelewa mzuri wa lugha yetu ya kiswahili,je matamshi yaliyoanishwa hapo juu yanatumika inavyostahili?

0713-046466
mlimbwa1977@yahoo.com
 
kwa mtu mwenye akili timamu hawezi shindwa kujua maana ya maneno hayo uliyoyaBOLD unless hauko okey kichwani
 
Watanzania tusipende kutoa majibu mapesi kwa mambo ya msingi,wapo watu wanaotatizwa na matamko ya maneno niliyobold hapo juu,badala ya kuonyesha weledi wako unakebehi.Ama kweli watanzania tumelaaniwa,watu hawana muda wa kutafakari,wanalipuka tu kujibu hoja kimzahamzaha tu.

Please,Watu werevu wasaidieni wanaotatizwa kwa kutolea ufafanuzi maneno hayo.
 
.wanaposema pembezoni mwa nchi maana yake ni mikoa iliyo mipakani na nchi jirani.
mikoa ya kati ni mikoa iliyo katikati mwa nchi kama dom na sgd.
kituo cha kati maana yake ni central police yaani kituo kikuu.
 
Kama maana ya mikoa ya pembezoni ni iliyo mipakani mwa nchi, kwanini inatajwa kukimbiwa na wafanyakazi kwa kisingizio cha kukosa hiduma muhimu? Mara zote wanaposema mikoa ya pembezoni wanataja,Mtwara,Ruvuma,Kigoma,Kagera,Rukwa.Lakini hawataji mikoa kama Tanga,Mwanza,Arusha,Mbeya ambayo pia ipo mipakani? Wanasema kabisa kwamba wafanyakazi wanaopangiwa huko wanapaswa kupewa motisha.Endelea kujadili.
 
kweli viraza nchi hii hawatapungua!
 
Pengine pembezoni hapa inawakilisha mikoa yenye sifa zote mbili zifuatazo: a) mipakani b) miundombinu ya shida hasa ya usafiri
 
Sijui kuhusu kwenu unapotokea, ila kwetu hii hali ya 'upembezoni' ipo sana. Kwa kawaida kuna shamba (mahali pale mnapoishi, hapa sizungumzii mj¡ni) na katika eneo hili kutakuwa na sehemu moja ambapo nyumba mnayoishi ndio imejengwa. Ni kawaida kwa eneo hili karibu na nyumba kupata attention zaidi kulinganisha na maeneo yaliyo mbali na nyumba ile, si ndio?

Vivyo hivyo kwa Kigoma, Rukwa, n.k., inawezekana K'njaro na Arusha ipo pembezoni lakini ipo karibu na pale nyumba ilipojengwa!
 
Back
Top Bottom