James Kasonda
Member
- Apr 2, 2012
- 84
- 49
Wakuu Habari!
Huwa Na Jiuliza Kuna Uhusiano Gani Kati Ya Umaskini Na Ulokole, Kwani Nina Ndugu Yangu Kabla Ya Kuokoka Alikuwa Na Kibato Kizuri Tu, Na Gari Na Nyumba Nne. Lakini Baada Ya Kuokoka Amefilisika Kabisa Ameuza Gari Na Nyumba Mbili. Sasa Anashindwa Hata Kuwasomesha Watoto Wake Yaani Amechoka.
Swali La Kujiuliza Kwanini Idadi Kubwa Ya Watu Wanaojiita WALOKOLE Ukiingalia Maisha Yao Ni Duni Lakini Sio Wote. Sasa Kuna Uhusiano Gani Kati Ya Ulokole Na Umaskini?
Walokole walio na maisha duni ni waumini(kondoo) lakini si viongozi wao (wachungaji). Kwa nini? Kwa sababu kama Yesu alivyosema ni kwamba wanachunwa ngozi wakiwa hai. Hawana ujuzi sahihi wa neno la Mungu kwa hiyo wanatumiwa kama vitega uchumi bila wao kujijua. Viongozi wao wanaishi maisha ya juu na ya kifahari wakati wao hawajui kesho watakula nini.
Kwa moyo mweupe kabisa wanafikiri sadaka wanazotoa zinaenda kuendeleza kazi ya Mungu kumbe zinaenda kutajirisha watu. Mungu anaona na anawaonea huruma kwa jinsi wanavyochunwa ngozi wakiwa hai. Yesu anatoa shauri hili lenye upendo kwa hao kondoo wanaoteseka:
"Tokeni kwake watu wangu ikiwa hamtaki kushiriki pamoja naye dhambi zake na ikiwa hamtaki kupokea sehemu ya mapigo yake"