Kwanini Idadi Kubwa Ya Walokole Ni Maskini?

Kwanini Idadi Kubwa Ya Walokole Ni Maskini?

Status
Not open for further replies.
Mbona hawa mitume na manabii wa kileo ni matajiri sana? Wao hawamfuati yesu?

Hili ni hekalu la CREFLO DOLLAR


tumblr_inline_mxayqa86fh1ss6hjj.jpg


Hekalu la JOYCE MEYER

meyercompound%20(1).jpeg


Hekalu la GETRUDE LWAKATARE

moja1.jpg


duh.. ndo maana siku hizi hamu ya kwenda kanisani imepungua sana!

sina hata bajaj ya kupaki pembeni, wakati huo huo lwa-k ana jumba la dhahabu!
 
Wakuu Habari!
Huwa Na Jiuliza Kuna Uhusiano Gani Kati Ya Umaskini Na Ulokole, Kwani Nina Ndugu Yangu Kabla Ya Kuokoka Alikuwa Na Kibato Kizuri Tu, Na Gari Na Nyumba Nne. Lakini Baada Ya Kuokoka Amefilisika Kabisa Ameuza Gari Na Nyumba Mbili. Sasa Anashindwa Hata Kuwasomesha Watoto Wake Yaani Amechoka.
Swali La Kujiuliza Kwanini Idadi Kubwa Ya Watu Wanaojiita WALOKOLE Ukiingalia Maisha Yao Ni Duni Lakini Sio Wote. Sasa Kuna Uhusiano Gani Kati Ya Ulokole Na Umaskini?
1.Suala la kufilisika lipo hata kwa watu wengine we angalia magari ya Scandinavia huwezi amini
2.Wapo atu wanapata utajiri kwa wizi na baadaye kuporomoka
3.Huwezi husisha imani ya mtu na umasikini labda kama wewe unakerwa na imani hiyo!
4.Waganga wa kienyeji huwa wanauza dawa za utajiri lakini wao wanishi kwenye umasikini wa kutupa mbona hili hujauliza??
 
Mtu akiokoka anahamishwa kutoka ufalme wa shetani na kuwekwa ufalme wa Mungu na Bwana Yesu. Hivyo tayari anakua adui mkubwa wa shetani na hivyo shetani uanza vita kali ya kuhakikisha kuwa hafanikiwe kifedha. Kinachotakiwa kufuata hapa ni kwa mlokole huyu kujifunza na kuamini kwa bidii Neno la Mungu kuhusu utajiri na ulinzi wa Mungu, pamoja na kujiepousha kabisa na dhambi za mazoea. Akifanya hivyo baraka na utajiri wa Kristo umfuata na hatakuwa maskini tena. Ninao ushahidi mwingi wa ili, nikiwemo mimi mwenyewe. Tatizo ni kuwa traditional walokole wameaminishwa na shetani kuwa wako duni na mafanikio ni dhambi. Lakini huu sio mpango wa Mungu kwani injili itahubiriwaje duniani kote bila pesa? Na pesa atatoa nani kama sio walokole hawa hawa wanaojua uthamani wa injili? Na Mungu amehahidi kuwa ukitoa kwa ajili ya injili utabarikiwa, ila tatizo ndio hilo la mindset na imani kuwa Mungu atawabariki.

Kwa upande mwingine, kama mlokole alikuwa mpiga ma-dili haramu (rushwa, kitu kidogo, wizi, n.k) sehemu yoyote ile, akishaokoka inabidi anaacha yote na hivyo uonekana kama vile amekuwa maskini.
Katika upande mwingine,
 
Jibu ni rahisi sana... Je inawezekana kwa mtoto wa mfalme kuwa masikini?. Alie-okoka anakuwa mwana wa Mungu. hivyo Kwenye ulimwengu wa Kiroho yeye ni "prince" na ulimwengu wa Kimwili yeye Ni "mfalme".

kwamaana imeandikwa "Kwake Yeye aliyetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu Yake, akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu Wake ambaye ni Baba yake. (ufunuo.1:5-6)" na pia imeandikwa "Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa Zake Yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu. (1peter.2:9)"

KWANINI WENGI WANAOKOKA WANAKUWA MASIKINI?

Yesu mwenyewe alisema "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka" (mathayo:11:12). Kwahiyo mtu akitaka kuokoka lazima aamue kwelikweli... kwamaana wokovu hupatika kwa nguvu. Na baada ya mtu kuamua kuokoka hapo ndio shetani nae huanza kazi yake kuhakikisha anarudi kwake (kwahiyo kila ambae hajaokoka bado ni washetani)

Kwanza mtu anaeokoka huyo ndie wa Kristo kwani Kuokoka ni Kubatizwa kwa Roho Mtakatifu (sio kama huko kubatizwa kwa maji). Pia mtu ambae hataki kuokoka yeye Bado ni washetani kwamaana imeandikwa "Yeyote asiye na Roho wa Kristo yeye sio wa Kristo (warumi.8:9)"

MAPIGO MATAKU KWA KUTOKA KWA SHETANI DHIDI YA ANAEOKOKA

Mtu akiokoka na kama ni mvivu wa kusoma neno mara nyingi hupigwa mapigo haya matatu na shetani ili awe mfano mbaya kwa wenzake na hivyo wenzake wengi wakatae wokovu/kuokoka.

PIGO LA 1. Shetani atamdanganya alieokoka na kumfanya mtu huyo adhani utajiri ni dhambi... (hivyo wengine huishia kuuza mali zao na kukubali kuwa masikini)

Mlokokole huyo anaweza kudanganywa kwasabu Halijui NENO vizuri na hajui kuwa imeandikwa "Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini Wake ninyi mpate kuwa matajiri.(2korintho.8:9)"

Kwa mwana wa Mungu pesa zote anazomiliki ni za Mungu na kwaajiri ya kutimiza mapenzi ya Mungu. Lakini kwa mtu wa shetani utajiri wote ni wake na kwa ajili ya mapenzi yake wala sio ya mungu. kwahiyo mtu wa shetani ameweka tumaini lake kwenye hela hivyo mtu kama huyo ni mwabudu pesa na watu kama hawa ndio Yesu alisema "ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu"

PIGO LA 2. Shetani anamdanganya na kumfanya mtu aanze kuimba na kusema masuala ya siku za mwisho mda wote

Yote hii ni kwasabu mtu huyo hajui kuwa siku za mwisho zilisha anza tangu siku ya Pentekoste pale ambapo Roho Mtakatifu alimwaga duniani. kwani imeandikwa "Katika siku za mwisho, asema Bwana, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili"(matendo.2:17).

KWAHIYO MPAKA TUNA MIAKA 2014 YA SIKU ZA MWISHO. Lakini asielijua hili hadanganywa na shetani kiasi kwamba anakuwa mvivu na kutofanya kazi akizani sasa ndio siku za Mwisho. ndio maana Pualo alisema "asiefanya kazi na asile"

PIGO LA 3. Ni mtu baada ya kuokoka tu ghafla huanza kuhubiri injili pasipo mpangilio wowote na kila mahali...

mtu huyo mlokole mpya hufanya hivyo kwasababu bado hajasoma kuwa imeandikwa "Kuna wakati kwa ajili ya kila jambo, nayo majira kwa kila tendo chini ya mbingu: (mhubiri.3🙂" na tena mbele kidogo imeandikwa "kuna wakati muafaka na utaratibu wa kila jambo (mhubiri.8:6)"

Hivyo mtu huyo huonekana kanakwamba amechanganikiwa baada ya kuokoka... na kwanjia hiyo watu huishia kudharau wokovu hadi wengi wao wanakufa pasipo wokovu. THIS IS BIG LOSS kwamaana imeandikwa "mwandamu amewekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu ( angalia waebrania.9:27)". kwahiyo atakaekufa bila ya wokovu atahukumiwa.


MTU KUWA MASIKINI NI KWASABABU HALIJUI NENO VIZURI. na hapo ndioo shetani anaamuwa kupatumia vizuri kwani anaeokoka katika nyakati za mwanzo huwa halijui neno vizuri.

Kuna silaha za Mungu 6 (waefeso.6:10-18)

1. Kweli
2. Haki
3. injili ya amani
4. imani
5. wokovu/kuokoka (waefeso.6:17)
6. upanga wa Roho ambao ndio neno.
Yote haya YAKO chini ya msingi wa moambi

ALIEOKOKA ANAZO SILAHA ZOTE 5 yaani kuanzia ya 1-5 lakini hiyo silaha ya sita hupatikana kwa kusoma Neno la Mungu (biblia). Kwahiyo UKIONA MTU NI AMEOKOKA HALAFU ANAKUWA MASIKINI UJUE HILO NI PIGO LA SHETANI KWASABABU HUYO ALIEOKOKA HALIJUI NENO VIZURI. Yaani mtu huyo bado hana hiyo silaha ya Sita.
 
Wanauza mali zao wamfuate kristo kwani Yesu hakuwa na mali wala mahali pa kuweka kichwa chake.

Na huu mtari unaosema "Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini Wake ninyi mpate kuwa matajiri (2korinth.8:9)"
KAMA HICHO ULICHOSEMA NI SAHII NA HUU MTARI UNAMAANA GANI?
 
Acheni kuleta mistari ya biblia Jibuni sealing la mtoa mada
Sio tu walokole. Waangalie wote wanaojifanya wanaijua dini sana
Ni maskini wakubwa
 
Wakuu Habari!
Huwa Na Jiuliza Kuna Uhusiano Gani Kati Ya Umaskini Na Ulokole, Kwani Nina Ndugu Yangu Kabla Ya Kuokoka Alikuwa Na Kibato Kizuri Tu, Na Gari Na Nyumba Nne. Lakini Baada Ya Kuokoka Amefilisika Kabisa Ameuza Gari Na Nyumba Mbili. Sasa Anashindwa Hata Kuwasomesha Watoto Wake Yaani Amechoka.
Swali La Kujiuliza Kwanini Idadi Kubwa Ya Watu Wanaojiita WALOKOLE Ukiingalia Maisha Yao Ni Duni Lakini Sio Wote. Sasa Kuna Uhusiano Gani Kati Ya Ulokole Na Umaskini?

Mtu aliyeokoka hana ufisadi kwa hiyo usitarajie mapato ya ghafla ila anatakiwa awe mcha Mungu na kufuata kanuni za mafanikio kibiblia.Mafanikio ya mtu kimwili ni dhihirisho tu la halo yake kiroho "mpenzi ufanikiwe kama roho yako ifanikiwavyo".Hata hivyo ijulikane kuwa kipaumbele cha mtu aliyeokoka sio utajiri wa kupindukia " mali kidogo pamoja na kuridhika ni faida kubwa". Furaha anAyopata mtu aliyeokoka hailinganishwi katu na furAha ya kuwa na mali nyingi. Mbarikiwe
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Kwa sababu ukiupata utajiri wa dunia yote utakusaidia nini? Mambo tunayoyaangaikia ambayo wewe unaita "utajiri" ni ubatili mtupu maana baada ya siku zako hapa duniani hutandoka hata na kitasa cha mlango au wiper ya gari au hata tuu ATM card

Ndugu Yangu Simaanishi Utajiri Ulio Kufulu Nazungumzia Kipato Mtu Anashindwa Hata Kumlipia Mtoto Ada Kisa Yupo Busy Na Kanisani. Kutwa Nzima Ye Na Kazi Za Baba Mchungaji.
 
Waislam wengi washika dini ndo wanaovaa ndala, kanzu zina viraka, baraghashia ina matobo, na wengi wanategemea misosi ya kwenye shughuli. Hakika uislam na umaskini ni kama mkate na blue band
 
Wanadhani Yesu atawaletea pesa

Badala ya kwenda kufanya kazi
 
Mbona hawa mitume na manabii wa kileo ni matajiri sana? Wao hawamfuati yesu?

Hili ni hekalu la CREFLO DOLLAR


tumblr_inline_mxayqa86fh1ss6hjj.jpg


Hekalu la JOYCE MEYER

meyercompound%20(1).jpeg


Hekalu la GETRUDE LWAKATARE

moja1.jpg


Mkuu Safari Safari Hapa Nazungumzia WAUMINI WAO NA SIO WACHUNGAJI Mbona Hiyo Inaeleweka
 
1.Suala la kufilisika lipo hata kwa watu wengine we angalia magari ya Scandinavia huwezi amini
2.Wapo atu wanapata utajiri kwa wizi na baadaye kuporomoka
3.Huwezi husisha imani ya mtu na umasikini labda kama wewe unakerwa na imani hiyo!
4.Waganga wa kienyeji huwa wanauza dawa za utajiri lakini wao wanishi kwenye umasikini wa kutupa mbona hili hujauliza??

Ndugu Yangu Sijakashfu Imani Ya Mtu Huu Ni Mtizamo Wangu.
 
Shule za Kilokole pia ndio zinaongoza kutoa ZERO katika mitiani ya Kimataifa...

There must be something wrong..
 
Acheni kuleta mistari ya biblia Jibuni sealing la mtoa mada
Sio tu walokole. Waangalie wote wanaojifanya wanaijua dini sana
Ni maskini wakubwa

Namshangaa Huyo Jamaa Hata Mimi Biblia Naifahamu. Nachohoji Hapa Ni Kwa Kipato Chao Hakiwatoshelezi?
 
Mkuu...
Hata mashuleni huwa hawafanyi vizuri, wanaishia kuwa viongozi tu. Au ndio wanaconcetrate na mambo ya dini na kusahau shule? Wengi wa wanafunzi walokole wanafanya vibaya kwenye mitihani yao.

Mkuu hii ni kweli kabisa...

Hili hata mm nimelishuhudia wazi wazi....Utendaji wao pia makazini ni poor....

Tazama shule zinazomilikiwa na Walokole utajua...
 
Utakuta Inafika Mahala Hata NDOA ZAO ZINAVURUGIKA Kwa Sababu Ya Ulokole Kutwa Nzima Mama Yupo Busy Na Kanisa Mara Semina, Mara Kuna Kazi Za BABA MCHUNGAJI. HATUKATAZI WATU KUSALI.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom