Kwanini hukunambia mapema M? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini hukunambia mapema M?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by FirstLady1, Jun 26, 2012.

 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Please nisaidie Dada! .ni kauli ya Meggy hiyo Kwangu.

  Jamani mie namsaidiaje huyu rafiki ?

  M & N Wamekuwa wapenzi for more than 5 years sasa long distance na wakikutana kila mmoja ana hamu na mwenzie.
  Dada yuko 29 yrs old
  Kabla ya hapo Bidada aliwahi kuzaa mtoto wake ana miaka tisa na alikuwa anajipanga ni lini amwambie mwenzie.
  Jamaa amekuja kutoka huko ovasizi na ilikuwa next jmos wafanye engagement tayari kwa mambo mengine.
  Meggy jmos ya tarehe 09 akamuomba mchumba wake watoke out kwa maongezi.
  Jamaaa kwa Furaha akaitikia wito..wakiwa wametawaliwa na vicheko vya upendo ndipo Meggy kavunja ukimya kwa kumwambia Mchumba wake
  Kuwa ana mtoto wa miaka 9 na alingoja tu wapate muda mzuri ili amwambie.
  Jamaa alinyanyuka kwa hasira na kusema Kwa nini hukunambia mapema ?
  it is over between us..naomba urudi nyumbani na unisahau milele.
  Baada ya hapo Kaenda kwa mchumba nyumba imefungwa..
  Toka hapo Meggy anapiga simu hapokei ..
  anatuma message hazijibiwi ni week ya pili sasa
  kabaki analia tu hata ukiongea nae ni machozi yanabubujika tu.

  Jamani akina kaka/baba afanye nini huyu dada maana amekuwa mgonjwa ghafla…
  Kina mama/dada mpeni mawazo huyu binti namuona kila siku anazidi kuchanganyikiwa..

  Nawasilisha....!
   
 2. condorezaraisi

  condorezaraisi JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mapenzi ya siku hizi mbona ya kuunga unga na gundi?:A S confused:
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Amefanya kile alichopaswa kufanya, kumwambia kabla ya engagement.

  Amtumie email au text, amuombe msamaha kwa kuchelewa kumwambia.

  Pia amwambie ni jinsi gani anampenda na anaelewa reaction yake, then amwambie anampa muda kwani ni kweli anahitaji muda na kuwa akiona bado wanaweza kuwa a couple she is there waiting kwani penzi lake si rahisi kulifuta kihivyo.

  Meanwhile she should do a lot of praying na asimsumbue kwa misimu au mails, one in a week ya kumjulia hali inatosha hata isipojibiwa.

  kuwa naye karibu, she needs a friend now more than before.
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hata mimi ningekasirika, nyie wanawake ndio mnapochemsha hapo, kama una mtoto inabidi ile siku ya kwanza mnakutana unamwambia ili hata ki akili aanze kujipanga unajua hivi vitu vina affect sana mental state ya mtu sasa wewe unamwambia mtu una mtoto a few days before the engagement day that's a mistake hata mimi nisingekubali. Hivi vitu ni very sensitive kwa maisha ya mtu kwa sababu yule mtoto atakua part of his life so inabidi umwambie toka mwanzoni kabisa ili ajue anasuka au kunyoa. Mpe pole imekula kwake
   
 5. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mapenzi ya kweli yako wapi?
   
 6. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,317
  Likes Received: 2,283
  Trophy Points: 280
  Dah...Kosa alishafanya (kutosema ukweli kabla kuhusu mtoto)..Lakini namwelewa najua ninyi (wasichana) mkipenda huwa wakati mwingine mnajenga hofu ya msingi juu ya yale mnayohisi yatamfanya mpenzi wako kukasirika au hata kuachana.

  Napata picha kwamba alikuwa tokea mwanzo anapata shida kumweleza ukweli, na si bahati mbaya ni hofu tu (nachukulia hili positively).

  Sasa maji yamemwagika na nikisimama kwenye viatu vya Jamaa naona ni ngumu sana kumrudia huyu binti angalau kwa kipindi hiki. La msingi amwache Jamaa atulie kwanza halafu kama jamaa hajaathiriwa na tamaduni za nje anaweza kutumia njia ya busara sana kumwomba radhi...Inaweza kuwa kwa njia ya mtu mzima ambaye jamaa anayemheshimu.
   
 7. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Kwanza nampongeza kwa kumwambia, kafanya vyema sana, na jamaa Ana haki ya kuwa na hiyo reaction, ila jamaa atalainika tu maana najua anampenda kutokana na text yako.

  Asimpigie Sana wala kumsumbua, awe mtulivu and strong kumngoja atulie kwa subira, jamaa atakurudi tu Nina uhakika, kuwa na mtoto is not the end of the world real.

  Na wanaume tuna tabia moja, the more you call and be upset the more they know you are around, sasa yeye akae Kimya Kidogo, apotezee, lijamaa litamtafuta tu, na yeye asiwe na kiburi.

  I will be happy to hear they are back together and this will happen for sure, mpe pole.   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kaunga naunga mkono hoja yako
  Kusema ukweli alifanya kosa sana (japo hofu yake inaweza ikawa na msingi sana maana wengi wanaogopa kusema ukweli angekataliwa mapema) ila kutosema nalo ni kosa jingine
  Atulie na atulize fikra na mawazo yake
  Kama kuna real love kwa huyo jamaa atarudi kama kweli alikuwa anampemnda kwa dhati kutoka moyoni mwake na alimpenda licha ya mapungufu aliyoyaona
  Atulie na kama kuna uwezekano aache mambo ya kumpigia simu au kutuma sms
  Ajipange na kama ni kutuma ujumbe may be kwa email kumweleza sababu za yeye kutotaka kulisema wazi jambo hilo na hofu aliyokuwa nayo na ndo maana aliamua kumwambia siku kabla ya engagement yake
  Je angelisema baada ya harusi ingekuwaje
   
 9. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Duu kazi kweli kweli,yah ni vizuri unapoingia kwenye mahusiano ujue malengo ya mwenzio na umweleze ABC za maisha yako mapema hasa kama mna lengo la kuishi kama mume na mke. kwani akijua baadaye hatajisikia vizuri ataona kama kasalitiwa vile, ila kikubwa huyo jamaa anaonekana hakuwa akimpenda huyo mdada kivile kwani kuwa na mtoto haibadilishi feeling za mtu (uswazi:ukipenda boga upende na ua lake)kwani mtoto mwenyewe alizaliwa longtime hata kabla hawaja anza relationship yao.

  Mshauri ajipange upya kwani jamaa harudi tena na hata akirudi haitakuwa kama mwanzo watakuwa wakiishi kimashaka mashaka na mwendo wa kutoaminiana.

  Pia atafute kitu cha kumfanya kuwa busy kama vile kurudi shule kusoma na kujiendeleza zaidi kielimu.

  Pia rafiki zake mumsadie kuwa nae karibu kutoka nae out na kumshirikisha mambo mengine mazuri yatakaoyomsaidia kupunguza machungu na mawazo.

  Nawasilisha
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mimi huwa sielewi unawezaje kaa na mtu kwa wiki nzima hujamtaja mwanao kama unaye.
  Hainiingii akilini sababu mwanangu ni part and parcel yangu.

  Yaani nikianza kumtamani tu mtu atajua nina watoto 3 kila mmoja na baba yake na hata majina ya baba zao atayajua.

  Sio fair hata kidogo kuficha, yaani mtu unalala naye 24hrs hajajua kama una watoto?

  Babu Dark City njoo unieleweshe hapa maana mie sioni kwa nini Meggy anashangaa kuachwa na kwa nini aendelee kumsumbua huyo kijana wa watu kwa mimeseji
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Duh! Miaka mitano hujamwambi kisha few days b4 engmnt ndo unasema lazima jamaa adate
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mie sielewi hapa kabisa hapa.

  Kama huna right information huwezi fanya right decisions.

  Ndo maana makampuni sasa yanahangaika na Management Informations Systems kuhakikisha tu availability ya right info zinapohitajika kwa maamuzi sahihi.

  Katika mahusiani kila mtu ana taboo zake, mwingine hawezi ishi na mtu mwenye mtoto, mwingine hawezi ishi na mwenye kifafa, kila mtu ana lake.

  Labda huyu kaka angejua Meggy ana mtoto wala asingeingia kwenye mahusiano hayo.

  Kaka kumsamehe Meggy ni A lakini Meggy kutosema ana mtoto ni B(ambayo kwangu huwa siielewi hata kidogo)
  Kinachoshangaza zaidi utasikia Meggy anasema 'nampenda sana'

   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kongosho, saa ingine najiogopa kwa kuona akili yangu inakaribia kufanana na yako, uwiii!

  Yaani on the first date na mtoto ataongelewa na kupigiwa simu,kha! Amemkosea sana huyu kaka. Tatizo ni moja, hii ameisema siku chache kabla ya engagement, mengine atayasema a day before harusi ama? Akaanze upya aisee, keshalikoroga. Otherwise ampe kaka wa watu space akijisikia atarudi mwenyewe!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Yako kwangu, nipe nafasi.
   
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  I know, mimi tumejuana maisha status kabla hata ya kuamua kuwa wapenzi. Hivyo tulivyoingia kwenye mahusiani kila mtu at least anajua what s/he is into. With my big mouth, sijui kuficha kuhusu my life ili ujue unapenda mtu wa namna gani.
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kongosho hata mimi napata shida sana kuelewa unakaa na mtu muda mrefu hivyo halafu hujasema kuwa una mtoto
  Yaani kwa namna unavyokaa na mtoto wako na unavyompenda na the way may be unamiss mtoto wako ukiwa mbali nae nafikiri hata wiki tuu ingekuwa ngumu kuacha kumsema au kumtaja
  may be alificha akaona sasa atakuja kuumbuka akaona bora aseme au aweke wazi
   
 17. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Hii naona ni janga la JF kama si la kitaifa! LOL
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kama umeanza kufanana na mie nabadili nabadili saplaya wa msuba aloo
  Hii ni hatari kwa afya.

  Asubiri tu huruma ya huyu kaka kama ataamua kurudi kwa hiari, but miaka 5? Khah!

   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Seriously, Meggy lazima ana issues na mwanae
  Sidhani kama ana mapenzi naye sababu anamuona ni 'aibu' au 'anguko' kwake
  ndo maana hana ujasiri kumtaja kwa watu anaodhani ni wa maana kwake.

  Unakumbuka ile stori ya mdada aliyenywesha sumu mtoto ili aolewe?
  Mi naona zinahusiana ila tofauti ni 'degree ya ukichaa' tu wa kutaka kuolewa ndio umetofautiana.

   
 20. N

  Neylu JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hilo ni tatizo kubwa tena sio kwa wanaweke peke yao bali hata kwa wanaume pia.. Ni vema kama una mtoto umueleze mpenzi wako mapema ili afanye maamuzi wakati huo huo.. Ona sasa anavyopata shida dada wa watu.. Kwa kweli aombe sana Mungu ili huyo mpenzi wake abadilishe mawazo..
   
Loading...