Kwanini hukunambia mapema M?

5 years ni muda mrefu sana kutogusia suala la mwanae. Usikute mwanaume alishtuka kweli maana imekuwa ghafla bin vuu!

She messed up bigtyme!!
 
Duh! Miaka mitano hujamwambi kisha few days b4 engmnt ndo unasema lazima jamaa adate

aah wapi ni mfumo dume tu huo; na ujinga uliopitiliza haiajalisha unaambiwa lini ilimradi ni kabla ya kuingia kwenye fungamano!...............

Hapo mshkaji kaonyesha utoto uliopitiliza na ahafai kuwa mume wa mtu yeyote kwani yaonyehsa wazi kukosa kwake uvumilivu!
 
aah wapi ni mfumo dume tu huo; na ujinga uliopitiliza haiajalisha unaambiwa lini ilimradi ni kabla ya kuingia kwenye fungamano!...............

Hapo mshkaji kaonyesha utoto uliopitiliza na ahafai kuwa mume wa mtu yeyote kwani yaonyehsa wazi kukosa kwake uvumilivu!

no ni malengo yake, alipanga kutooa mwanamke mwenye mtoto. So angejua mapema, vilevile angejikataa na kutafuta wanaofanana.
 
just ampe tym ya mpnz wake kumaliza hasira.,kwa kawaida lazma m2 hareact hvyo coz ni mda mrefu sana wapo pamoja bt hakumwambia..,kama kwl the man loved her vry much he wil be back tena wiz engagement ring!,,pole m.
 
duh pole sana bidada, ila hii mbona nyepesi sana, hata hivyo bado nampongeza bidada kwa alichokifanya kumwambia mkaka kabda hata engagement. Kuna jamaa mpaka alioa na akazaa nae mtoto baadae bidada akaleta mtoto wake aliyezaa kabla.... ikawa kizaazaa kwenye ndoa, ilibidi wazee waingilie kati... mwisho wa siku maisha yaliendelea....
 
Kwanza amekosea sana kwa kutokusema ukweli mapema but bado anayo nafasi awaeleze wazazi wake na huyo mwanaume huenda wakamsaidia au marafiki zake na huyo mwanaume mpe pole sana
 
Kama ni ushamba wacha niwe mshamba! Na kama ndo upendo wacha nionekane sina! Kama yeye ana upendo mbona hakumwambia tangu mwanzo?! Kama unampenda mwenzako utamficha kuhusu mambo hata yasiyofichika?! Mwambie huyo bidada akubaliane na ukweli aendelee na maisha yake, kama huyo N ana mtazamo kama wangu hatarudi ng'o! Ninajichunga sana, sijawahi kumpa mtoto wa mtu mimba. Na msimamo wangu ni kuwa hata iweje sitaoa mdada mwenye mtoto, ndivyo nilivyochagua kwa utashi wangu. Hapa nilipo kuna wadada wa aina mbili 'ninaowaogopa' mke wa mtu na mdada aliyekwishazaa! Nikikutana na mdada wa hivyo hata kama nimemzimikia vipi akitaja mume au mtoto, kwa heshima kabisa atabaki kuwa best, mambo ya mapenzi asahau. Jamani watu tupo wa aina nyingi na kila mtu ana vigezo alivyojiwekea. Kuna mtu huko juu kauliza kama kuwa na mtoto ni dhambi! Jibu liko wazi, neno dhambi amelitoa wapi?! Kitendo kinachosababisha kupata mtoto kabla/nje ya ndoa kinaitwa dhambi. Ikiwa nina dhambi hainipi haki ya kuzihalalisha kuwa siyo dhambi, hata dhambi iliyozoeleka bado ni dhambi!
 
Atulie amlee mtoto wake. Kwenye mapenzi huwezi kufananisha situations A n B that kwa vile situation A inafanana na B basi solution itakuwa moja.

Kwenye mapenzi kila mmoja ana malengo na matarajio yake, above kila moyo unaathirika kwa namna yake. Mistake ya aina moja inaweza kuwa maumivu/uvumilivu usiofanana kwa watu wawili tofauti.

Alichokosea huyo mdada ni kutokuwa mkweli mapema, day 1 alipokutana na mume mtarajiwa. Mnaweza kumlaumu jamaa kwa kumtema dada wa wenyewe, think ni maumivu gani ya moyo aliyoyapata baada ya kugundua kuwa matarajio yake ya kuoa mmke ambaye hajazaa hayajatimia!
 
Back
Top Bottom