Kwanini hotuba za Rais Kikwete zinakosa mvuto?

Kwanini hotuba za Rais Kikwete zinakosa mvuto?

binafsi naonaga hotuba ya miaka mitano nyuma, na hiyo atakayosema mpya hazina tofauti.!
 
Habari zenu wanaJF, Mara nyingi nimekuwa nikipitwa na hotuba za kila mwisho wa mwezi za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania MHE.Jakaya Mrisho Kikwete tofauti na kipindi cha Mkapa ambapo watu walikuwa wanawahi majumbani kusikiliza hotuba zake.Usiku huu nimebahatika kuisikiliza hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka kupitia "starTV".... Nilishangaa ghafla nashikwa na usingizi na kulazimika kubadili "chanel". Je,ni kwa sababu umaarufu umeshuka au ni huku kusoma hotuba kuliko pitiliza?
tatizo haliko kwenye hutuba za kikwete bali kwenye ubongo wako.wakati flan mtu anaweza awe hata haoni kitu adhani hakipo; kumbe tatizo ni macho yake hayaoni.kwa hiyo wewe nakushauri umuone daktari.kama ni brain disoders;atakupatia dawa lakini kama ni matatizo ya kisaikolojia atakuelekeza kwa washauri wa saikolojia.wenzako tunamsikiliza rais na tunamuelewa vizuri.any way, ukiona huelewi hoja;wewe cheki burudani clauds tv.
 
haya anamaliza muda wake tusubiri hutuba za babu dr slaa aakapokuwa madarakani zitakuwa na mvuto kweli na watanzania wote tutakaa katika tv na radio na kusoma magazetini
tutafokewa mpaka bas.ila tutamsikiliza maana kama atakuwa kachaguliwa na walio wengi,basi itabidi tumsikilize.
 
Hana audience, anayoyasema hayahusiani na matatizo ya watanzania
 
Kweli akili ni nywele. Umeulizwa kwa nini hazivutii, unajibu kwa sababu hazivutii? teh teh teh.

n swali lakipuuz hlo,wote 2najua mshkaj hana haiba ya urais,atatoaje speech nzur kama rais.?kaulza swal ambalo jbu lakdd analjua kabsaa..
 
Nilidhani baada ya kuanza kujiita Dokta atabadilika. Ni Rais kilaza kuliko wote waliomtangulia. Boring stiff.
 
haya anamaliza muda wake tusubiri hutuba za babu dr slaa aakapokuwa madarakani zitakuwa na mvuto kweli na watanzania wote tutakaa katika tv na radio na kusoma magazetini

Nani kasema slaa atakuwa rais?
 
mwanamke akimchukia mtu hupenda hata bwana wake naye amchukie huyo mtu,acha kuleta wivu wakike.Kikwete amevutia sana watz kusikiliza speeech za kila mwezi na hapa JF ni ushahidi tosha.Kipindi cha mkapa watu hawakupenda kumsikiliza walishamuona miyayusho,kwa kuwaletea UKAPA.Alikuwa akitoa hotuba zinazochosha kusikiliza hata kusoma.Tuondoe chuki za kike hata kama humpendi lakini kuwa mkweli

wewe ni JK?
 
Hotuba za Kikwete hazina mvuto kwasababu anachokiongea hakina uhusiano na anachotenda.

Hajui anaowaongoza wanataka nini. Mwisho Rais Kikwete hasomi vitabu, viongozi wote unawajua kuanzia Mwl Nyerere na wengine waliokuwa mabingwa wa kutoa hotuba nzuri walikuwa wasomaji wazuri wa vitabu.
 
tatizo haliko kwenye hutuba za kikwete bali kwenye ubongo wako.wakati flan mtu anaweza awe hata haoni kitu adhani hakipo; kumbe tatizo ni macho yake hayaoni.kwa hiyo wewe nakushauri umuone daktari.kama ni brain disoders;atakupatia dawa lakini kama ni matatizo ya kisaikolojia atakuelekeza kwa washauri wa saikolojia.wenzako tunamsikiliza rais na tunamuelewa vizuri.any way, ukiona huelewi hoja;wewe cheki burudani clauds tv.
Mwenzetu unaona macho yako yanafanana naye
 
Habari zenu wanaJF,

Mara nyingi nimekuwa nikipitwa na hotuba za kila mwisho wa mwezi za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania MHE. Jakaya Mrisho Kikwete tofauti na kipindi cha Mkapa ambapo watu walikuwa wanawahi majumbani kusikiliza hotuba zake.

Usiku huu nimebahatika kuisikiliza hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka kupitia "starTV"....

Nilishangaa ghafla nashikwa na usingizi na kulazimika kubadili "channel".

Je, ni kwa sababu umaarufu umeshuka au ni huku kusoma hotuba kuliko pitiliza?

kweli kabisa unataka tuamini ati hotuba za Mh Kikwete zinakosa mvuto? Nafikiri inategemea anahutubia akina nani, endapo atahutubia wazee wa Dar es Salaam hapo ndio utaona sio tu mvuto wa hotuba, bali msisimko na bashasha toka kwa wasikilizaji...!
 
Back
Top Bottom