JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Kimaendeleo: Wakoloni waliyapendelea maeneo fulani fulani ili yatofautiane na mengine na ili yasitamani kushirikiana na maeneo ya watu 'duni'. Mojawapo ya watu waliopendelewa na wakoloni kwa mtindo huo ni wachagga, hadi kufikia kujiona kuwa wao ni bora kuliko watanganyika wote, na hadi wakatamani wasiwe sehemu ya Tanganyika, na hiki ndicho kisa cha Marealle kutaka uhuru wa wachagga pekee! Mpango huu ungefanikiwa, ungewezesha wakoloni kuendelea kutawala kupitia uhuru bandia wa baadhi ya maeneo kama walivyokuwa wanafanya makaburu kule South Africa.
..Mkoloni hakuwapendelea Wachagga.
..mwanzoni Mkoloni alitaka kuwa-exploit Wachagga kwa kuwalimisha Kahawa kwa mtindo wa manamba.
..Wachagga wali-resist mpango huo ndipo Mkoloni akanywea na kuruhusu Wachagga kulima kahawa na kumiliki ardhi.
..Miundombinu iliyowekwa na Mkoloni haikuwa na lengo la kuwanufaisha Wachagga as a community zaidi ya kuwa njia ya kusomba mali toka maeneo ya uzalishaji na kusafirisha nje.
..Siyo kweli kwamba Marealle alidai Uhuru wa Wachagga peke yao. Ipo hotuba ya Nyerere aliyoitoa mbele ya Baraza la Makoloni ambapo amenukuliwa akisema anaunga mkono hoja iliyotolewa na mzungumzaji aliyemtangulia kuwa Tanganyika ipate uhuru. Mzungumzaji huyo alikuwa ni Chief Marealle.
..Pia Wachagga wenye elimu kama Solomon Eliufoo walikuwa wakimpinga Chief Marealle, na ndiyo waliofungua njia ya Tanu kuingia Uchaggani. Pia yupo Nsilo Swai ambaye alikuwa msomi na kiongozi wa chama cha Ushirika. Kwa hiyo siyo kweli kwamba Wachagga hawakuunga mkono harakati za Uhuru wa Tanganyika, au walitaka kujitenga.
NB:
..Uwekezaji mkubwa kuliko wote uliofanywa na Waingereza ktk koloni la Tanganyika ni mradi wa KARANGA maeneo ya mikoa ya Kusini. Bahati mbaya mradi huo ulifeli. Kama mradi huo ungefanikiwa huenda tungekuwa tunaongea habari nyingine sasa hivi.