Kwanini Historia ya Wachagga inafichwa Sana?

Tembosa

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
3,938
3,204
Wakuu nimewahi kusoma vizuri Historia ya Wachagga kwenye kitabu kimoja kilichoandikwa na Msweden mmoja, akimzungumzia vyema Mangi Marriale Obe II, na Binti aliyekuwa anaitwa Sia,
Aliyesome udaktari huko Sweden,

Pia inaonekana Mangi Marriale Obe II alikuwa msomi, na Hadi mwaka 1954 alikuwa anakaribia kuhitimisha kuomba uhuru wa Wachagga waliokuwa wamefika mbali kimaendeleo bila msaada wa Wazungu, hicho kitabu kinaeleza vizuri kuwa Gavana wa Uingereza kipindi hicho alikuwa hachangii chochote kwenye maendeleo ya Wachagga, hawa walikuwa wanakatwa kodi kutoka kwenye zao la kahawa.

Mipango ya kibajeti ilikuwa inawekwa vizuri sana kupitia kodi hizo na nyingine mbalimbali.

Kulikuwa na mfumo mzuri wa Elimu, pamoja na Miundo mbinu. Niliona bajeti kuu yao iliyochapishwa mwaka 1954.
Na kila mwaka walifanya mkutano mkuu wa Wachagga, uliokuwa unafanyikia Moshi...

Najiuliza ni kwanini Historia hii haisemwi popote katika utaratibu wa Mafundisho ya Historia!

Mkuu Malcom Lumumba nakupa copy hapa...na wanahistoria wengine
 
Kama kitabu ni softcopy kiweke hapa na wengine wenye kutaka kujisomea wajisomee bandugu
 
Kwani nani anaificha na nani anatakiwa kuifichua.... Ni historia ya kabila gani ambayo iko wazi wazi ....ukisema sijui walikuwa wanaendesha mambo yao wenyewe hata sehemu nyingine walikuwa wanaendesha mambo yao wenyewe..... makabila zaidi ya 120 haiwezekani ukafundisha kila kitu mashuleni... nyie wachaga kama mnaijua historia yenu muweke utaratibu mzuri wa kufundisha vizazi vyenu
 
Historia pekee nayoikumbuka na niliyofundishwa shuleni ni ya ule unafiki na usaliti wa kati ya Mangi Sina na Mangi Meli waliposalitiana mbele ya wazu gu. Pengine hili ni muendelezo wa tunachokiona sasa kutoka huko Kaskazini jinsi wanasiasa wa huko wasivyo na msimamo. Wanaongoza kwa kuhama upinzani huku wakimwaga sifa kedekede kwa utendaji JP licha ya kubaguliwa na kukandamizwa waziwazi. Mengine ni mitazamo yao finyu ya ukabila, kisiasa,kikanda na kidini na utokuwa na misimamo thabiti mwishowe wanabeba majani kuomba msamaha (Sare sare?) kwa mtu asiyestahili.
 

Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom